DOKEZO Serikali itusaidie Watumishi wa Kituo cha Afya Yombo Vituka, kuna mambo ya Uongozi hayapo sawa

DOKEZO Serikali itusaidie Watumishi wa Kituo cha Afya Yombo Vituka, kuna mambo ya Uongozi hayapo sawa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Vituka.jpg
Mimi ni mmoja wa watumishi wa Kituo cha Afya Yombo Vituka, na ninaomba kufikisha kilio chetu kuhusu mazingira ya kazi ambayo kwa muda mrefu yamekuwa magumu kutokana na mwenendo wa katibu wa kituo chetu.

Sisi watumishi tunafanya kazi kwa muda wa ziada (overtime), lakini malipo yake hayafanyiki kwa wakati. Hivi sasa tupo mwezi wa saba, lakini bado tunadai malipo ya overtime ya mwezi wa tatu, huku ya miezi ya nne, tano na sita nayo bado hatujalipwa.

Kinachotusikitisha zaidi ni kwamba fedha zinapokuja, baadhi ya watumishi wanadai hawalipwi kiwango kinacholingana na idadi ya saa walizofanya kazi. Ukijaribu kuuliza sababu ya kupunguziwa malipo, katibu anakuwa mkali na kukujibu kwa maneno kama, "Si unalipwa mshahara?" jambo ambalo linatukatisha tamaa na kutufanya tushindwe kudai haki zetu.

Mbali na hilo, tunahisi kuna mazingira ya vitisho kazini. Watumishi wengi wanaogopa kuzungumza kwa hofu ya kuchukuliwa hatua au kuhamishwa kituo. Hata kutofautiana naye kwa hoja au maoni kunaelezwa kunaweza kusababisha mtumishi kuhamishwa.

Tunafahamu kuwa uongozi wa kituo unalifahamu suala hili, lakini kwa namna moja au nyingine unaonekana kushindwa kulitatua. Aidha, tunafahamu kuwa katibu huyo aliwahi kupewa barua ya uhamisho kwenda kituo kingine, lakini uhamisho huo haukutekelezwa. Hali hiyo imezua maswali miongoni mwa watumishi, ambao wanahisi huenda ana ushawishi mkubwa katika ngazi za juu za halmashauri.

Kutokana na hali hiyo, tunaendelea kufanya kazi katika mazingira yenye hofu, msongo wa mawazo na kukosa motisha. Tunaomba mamlaka husika, hususan uongozi wa halmashauri na wizara yenye dhamana ya afya, kuchunguza kwa kina malalamiko haya, kuhakikisha malipo ya overtime yanafanyika kwa wakati na kwa kiwango stahiki, pamoja na kuboresha mazingira ya kazi ili watumishi waweze kutekeleza majukumu yao kwa haki, usawa na utu.

Tunatoa malalamiko haya kwa lengo la kutafuta suluhisho, si kuleta mgogoro, ili huduma kwa wananchi ziendelee kutolewa katika mazingira bora kwa manufaa ya wote.
 
Muombeeni huyo karibu Mungu ashughurike naye, ushasema alipewa barua haikuleta matokeo
 
Naona alfajiri ya Leo mmeaka kivingine na kero zenu watu wa ccm..ongezeni milio
 
Back
Top Bottom