Serikali iuangalie mji wa Kahama kwa jicho la tatu

Buzwagi haina mchango kiviiile kwenye maendeleo ya mji wa Kahama!!

Migodi midogo ndiyo kila kitu,Barrick wameikuta Kahama inakimbiza na wameiacha.

NB:Hayo mashimo unayoyaona barabarani (Tabora Rd-Ngaya Rd) ni uchomaji matairi 29/10/2025!!
Thibitisha hayo mashimo yametokana na vurugu za Oktaba 29
 
Unajua umri wa hiyo barabara?

Mara ya mwisho kufika kahama ni lini?

Muhimu ni kuzihudumia hizo barabara kwa kuzifanyia usafi, McFerrin iwe Safi, wananchi watimize wajibu wao wa kulinda na kutunza miundombinu.

Mahitaji ni mengi, sasa hivi Kuna ujenzi mkubwa wa hospital kubwa hapo kahama, kwenye hiyo video haujaoneshwa hilo pia?

Fika kahama kaka ukapate viwanja vinavyo uzwa na halmashauri ya Manispaa
Umri wa barabara sasa unahusika vipi. Kama barabara ina umri mkubwa na imechakaa si inapaswa iwe refurbished au? Kwani wewe unaona ni sahihi barabara kubaki hivyo?
Kwa nini Watanzania tunapenda kupinga hoja za maendeleo? Kuna ubaya gani kuzi refurbish hizo barabara? Maana hata ukizisafisha rangi zimeshafutika hapo, ni lazima tu kufanya refurbishment, kisha baada ya kurefurbish ndio tuanze kuzitunza. Kwa sasa tumechelewa, zimeshachakaa
 
Kwa upande wangu naona serikali iimarishe huduma za kijamii hasa vijijini,ni vema pawepo na kituo cha afya kila kijiji,maji safi angalau ya visima kwa kila kijiji,umeme sina malalamiko,huduma ya usafiri na usafirishaji vijijini ni shida,serikali iimarishe miundombinu hiyo. Kabla haijaimarisha miji ya kiuchumi ni muhimu kuimarisha huduma za jamii pia,kwani ni heri ukose ajira kuliko kushuhudia milipuko ya magonjwa itakanayo na unywaji wa maji machafu,kuliko kushuhudia vifo vya wananchi waliokosa huduma. Lakini kwa wilaya yangu japo kijijini huduma za jamii zote zipo
 
Serikali inatarajia kupanga bajeti zaidi ya Trilioni Moja Kwa ajili ya kuiendeleza kahama itakapofika 2030.Kwa Sasa pesa zote zinajenga mahoteli ya kifahari kizimkazi na sehemu zingine za zanzibar
 
Picha zote nilizotumia kwenye uzi huu ni za Kahama
View attachment 3529560Mimi sio mkazi wa Kahama ila huu mji unahitaji attention
Kahama ni mji unaokua kwa kasi na mzunguko wa hela upo vizuri kwa level za Kitanzania
View attachment 3529551

View attachment 3529557
Population inakua kwa kasi na sababu kuu ni shughuli za uchimbaji madini
Lakini hivi karibuni tumeona mgodi wa Buzwagi umefungwa, inaonekana madini yameisha au yamebaki kidogo
Serikali ikasema itajenga viwanda katika eneo ambapo mgodi huo ulikuwepo, ni idea nzuri lakini viwanda ni heri viwe vingi sana, sio tu mnajenga viwanda kumi. Viwepo viwanda hata zaidi ya 100 huko
View attachment 3529561View attachment 3529562

View attachment 3529552
Mtazamo wangu ni kwamba kuna umuhimu mkubwa wa kuanzisha Industrial park kubwa Kahama, ikiwezekana iwe kama ile ya SINO-TAN inayojengwa Kibaha
View attachment 3529558View attachment 3529559
Kwa nini? Kama mji umeweza kukua kwa kasi vile bila mchango mkubwa wa serikali na sio hivyo tu, bado unaendelea kukua hadi sasahivi maana yake serikali inapaswa ichangamkie mji wa Kahama kutumika kutengeneza ajira. Kwa mkono wa serikali Kahama itaendelea zaidi tena kwa kasi ya juu.
View attachment 3529552

Miji inayokua kwa kasi ina faida sana Tanzania, kwa mfano mji kama Kahama ndani ya muda wake wa ukuaji umesaidia vijana wengi sana kujikwamua kiuchumi. Wengi wameenda kuwekeza biashara zao Kahama na matunda yake wameyaona
View attachment 3529553
Tanzania inapaswa kuhakikisha miji yote yenye watu wengi inapewa support na kuongeza mzunguko wa hela ili isizidi kukua.
View attachment 3529556 Inasikitisha kuona miji inakua kwa kasi halafu serikali inaangalia tu mpaka baadae inaanza kujifia au maendeleo yanakuwa ya konokono, kama Moshi tungekuwa nayo serious ungekuwa mji mkubwa wenye fursa nyingi za kiuchumi, badala yake umebaki kuwa mji mdogo wa watu laki 2 sijui, na maendeleo yake ni yale yaliyofanywa miaka ya nyuma
View attachment 3529553View attachment 3529554
Kwa upande wa Kahama serikali inapaswa kuhakikisha inaboresha miundombinu. Barabara za Kahama zina mashimo, na zimejaa michanga. Zinahitaji kuwa refurbished au zijengwe upya katika viwango vya juu
View attachment 3529550View attachment 3529549
Pia stendi ya mabasi ya Kahama ni duni, inapaswa kuboreshwa au ijengwe stand mpya lakini isijengwe mbali na makazi ya watu kama tulivyofanya maeneo mengine. To make the town more alive stand kuu ijengwe ndani ya mji
Kwa sasa stendi ya Kahama ndio hii
View attachment 3529547View attachment 3529548

My take: Serikali haiwezi kutoa ajira kwa kila mtu lakini tunajua inaweza kuandaa mazingira mazuri ya kujiajiri. Ukiondoa kilimo na ufugaji ambavyo hufanywa zaidi vijijini, ukija mijini ili mtu ajiajiri na kupata pesa kunafaa kuwe na mzunguko wa hela

Serikali inapaswa kujenga viwanda, vyuo vikuu, miundombinu bora na kualika wawekezaji waje kuwekeza kwenye miji hii ili pesa izunguke. Inakuwa rahisi kwa Watanzania kujiajiri na kupata maisha mazuri

Sio tu Kahama, Tanzania tuna miji ambayo hatujui kuitumia. Miji yetu ina watu ambao wengi wao ni vijana, na watu ndio utajiri mkubwa kwenye nchi yoyote ile, ili kuuona utajiri wa watu ni lazima tutengeneze mazingira ya kuingiza hela kiurahisi.

View attachment 3529555
Sio tu Kahama, serikali inapaswa ianze kuja na mipango ya kuifanya miji ya Tanzania kuwa alive zaidi kibiashara. Miji kama
1. Morogoro
2. Moshi
3. Mbeya
4. Mtwara mjini
5. Kigoma mjini
6. Iringa
7. Katoro
8. Geita
9. Makambako
10. Bukoba
11. Songea
12. Njombe
13. Sumbawanga
14. Masasi
15. Babati
16. Kibaigwa
17. Gairo
18. Tunduma
19. Tunduru
20. Tandahimba
21. Ikwiriri
22. Mkuranga
23. Buseresere
24. Kasulu
25. Chalinze
26. Songwe
Na mingine mingi ina watu wengi lakini kinachokosekana ni mzunguko wa hela wa kutosha.

Tufikirie, tutafute namna ya kuiamsha miji yetu kibiashara

Si mnaona jiji la Dar lilivyo. Dar es Salaam ni one of Tanzania's biggest success. Licha ya kuwa jiji lenye matatizo mengi lakini ni kitovu cha biashara kwa Tanzania. Ni jiji lililosaidia watu wengi sana kufanikiwa kimaisha kupitia biashara. Naliheshimu sana jiji la Dar
Sasa haya mambo yasiishie Dar tu, tusambaze maendeleo na kuongeza mzunguko wa hela ili vijana wajitafute kimaisha kwenye maeneo mengi kupitia biashara. Isiwe Dar tu
Tunakosa watu wenye akili serkalini miji yetu ingekuwa mizuri sana na biashara zingekuwa kubwa na ajira tele.
 
Kwani ukisema wewe ni wa Kahama hivyo Serikali itazame Kwa ukaribu hasa kwenye miundombinu utakuwa umefanya kosa?

Pili miundombinu ni Changamoto ya miji yote Tanzania ni Kilimo Cha Taifa kasoro Dar & Dom pekee.

Kuhusu Stendi , Serikali inajenga stendi 2 hapo Kahama so mwisho wa mwaka huu zitakuwa tayari.

Mwisho Miji yote Tanzania inakuaje Kwa sehemu kubwa ila huko Kanda ya ziwa Miji ya Geita,Katoro,Tarime na Kahama ndio inakua zaidi.
 
Serikali haina mchango wowote.
Kahama wananchi Wana maji yao binafsi
Kahama wananchi wqna umeme wao binafsi
Kahama wananchi wanajijengea mabarabara ya lami

Kwa mujibu wa picha hizo ofisi za umma kahama hakuna kabisa, wananchi ni kama wapo katika nchi yao kivyao vyao...

Maandiko mengine ni mazuri ila..
Huu ni uongo
 
Kwani ukisema wewe ni wa Kahama hivyo Serikali itazame Kwa ukaribu hasa kwenye miundombinu utakuwa umefanya kosa?

Pili miundombinu ni Changamoto ya miji yote Tanzania ni Kilimo Cha Taifa kasoro Dar & Dom pekee.

Kuhusu Stendi , Serikali inajenga stendi 2 hapo Kahama so mwisho wa mwaka huu zitakuwa tayari.

Mwisho Miji yote Tanzania inakuaje Kwa sehemu kubwa ila huko Kanda ya ziwa Miji ya Geita,Katoro,Tarime na Kahama ndio inakua zaidi.
Kwanza mimi sio mkazi wa Kahama, na wala sio kwetu kwa namna yoyote ile
Pili sioni ubaya kwenye uzi wangu kwa hiyo sielewi povu lote hili linatoka wapi
 
Ulijituma sana kupiga picha mji mzima hakika wewe ni mzalendo wa Kahama.
 
Hizo picha ni screenshots kutoka kwenye video ya Bertin, YouTube
Angalia juu kushoto kwa kila picha utaona phrase "Explore with Bertin"
Mimi niko Mbeya, picha pekee ninazoweza kupiga na kutuma ni za Mbeya na ndio zimejaa kwenye Gallery yangu
Hata nimezipost humu mara nyingi. Mfano nilipost picha za Mbeya humy
.
Pia nilipost picha za Mbeya nyingine humu
.
Kwa hiyo kama ni picha za kupiga mwenyewe ni hizo za Mbeya ambazo huwa nazipost mara nyingi humu JF. Kahama sikuwa na picha zake kwa hiyo ilibidi nitafute video ya Bertin nianze kuscreenshot. Mimi huwa nafurahi sehemu zote za Tanzania zikiendelea. Sio kwamba nataka Kahama tu iendelee. No
Napenda jinsi miji kama Makambako, Chalinze, Mafinga, Katoro, Kahama, Kasulu na mingine mingi ya mikoani inavyokua kwa kasi
 
Back
Top Bottom