Serikali iuangalie mji wa Kahama kwa jicho la tatu

Buzwagi haina mchango kiviiile kwenye maendeleo ya mji wa Kahama!!

Migodi midogo ndiyo kila kitu,Barrick wameikuta Kahama inakimbiza na wameiacha.

NB:Hayo mashimo unayoyaona barabarani (Tabora Rd-Ngaya Rd) ni uchomaji matairi 29/10/2025!!
Thibitisha hayo mashimo yametokana na vurugu za Oktaba 29
 
Umri wa barabara sasa unahusika vipi. Kama barabara ina umri mkubwa na imechakaa si inapaswa iwe refurbished au? Kwani wewe unaona ni sahihi barabara kubaki hivyo?
Kwa nini Watanzania tunapenda kupinga hoja za maendeleo? Kuna ubaya gani kuzi refurbish hizo barabara? Maana hata ukizisafisha rangi zimeshafutika hapo, ni lazima tu kufanya refurbishment, kisha baada ya kurefurbish ndio tuanze kuzitunza. Kwa sasa tumechelewa, zimeshachakaa
 
Kwa upande wangu naona serikali iimarishe huduma za kijamii hasa vijijini,ni vema pawepo na kituo cha afya kila kijiji,maji safi angalau ya visima kwa kila kijiji,umeme sina malalamiko,huduma ya usafiri na usafirishaji vijijini ni shida,serikali iimarishe miundombinu hiyo. Kabla haijaimarisha miji ya kiuchumi ni muhimu kuimarisha huduma za jamii pia,kwani ni heri ukose ajira kuliko kushuhudia milipuko ya magonjwa itakanayo na unywaji wa maji machafu,kuliko kushuhudia vifo vya wananchi waliokosa huduma. Lakini kwa wilaya yangu japo kijijini huduma za jamii zote zipo
 
Serikali inatarajia kupanga bajeti zaidi ya Trilioni Moja Kwa ajili ya kuiendeleza kahama itakapofika 2030.Kwa Sasa pesa zote zinajenga mahoteli ya kifahari kizimkazi na sehemu zingine za zanzibar
 
Tunakosa watu wenye akili serkalini miji yetu ingekuwa mizuri sana na biashara zingekuwa kubwa na ajira tele.
 
Kwani ukisema wewe ni wa Kahama hivyo Serikali itazame Kwa ukaribu hasa kwenye miundombinu utakuwa umefanya kosa?

Pili miundombinu ni Changamoto ya miji yote Tanzania ni Kilimo Cha Taifa kasoro Dar & Dom pekee.

Kuhusu Stendi , Serikali inajenga stendi 2 hapo Kahama so mwisho wa mwaka huu zitakuwa tayari.

Mwisho Miji yote Tanzania inakuaje Kwa sehemu kubwa ila huko Kanda ya ziwa Miji ya Geita,Katoro,Tarime na Kahama ndio inakua zaidi.
 
Huu ni uongo
 
Kwanza mimi sio mkazi wa Kahama, na wala sio kwetu kwa namna yoyote ile
Pili sioni ubaya kwenye uzi wangu kwa hiyo sielewi povu lote hili linatoka wapi
 
Kwanza mimi sio mkazi wa Kahama, na wala sio kwetu kwa namna yoyote ile
Pili sioni ubaya kwenye uzi wangu kwa hiyo sielewi povu lote hili linatoka wapi
Ulijituma sana kupiga picha mji mzima hakika wewe ni mzalendo wa Kahama.
 
Ulijituma sana kupiga picha mji mzima hakika wewe ni mzalendo wa Kahama.
Hizo picha ni screenshots kutoka kwenye video ya Bertin, YouTube
Angalia juu kushoto kwa kila picha utaona phrase "Explore with Bertin"
Mimi niko Mbeya, picha pekee ninazoweza kupiga na kutuma ni za Mbeya na ndio zimejaa kwenye Gallery yangu
Hata nimezipost humu mara nyingi. Mfano nilipost picha za Mbeya humy
.
Pia nilipost picha za Mbeya nyingine humu
.
Kwa hiyo kama ni picha za kupiga mwenyewe ni hizo za Mbeya ambazo huwa nazipost mara nyingi humu JF. Kahama sikuwa na picha zake kwa hiyo ilibidi nitafute video ya Bertin nianze kuscreenshot. Mimi huwa nafurahi sehemu zote za Tanzania zikiendelea. Sio kwamba nataka Kahama tu iendelee. No
Napenda jinsi miji kama Makambako, Chalinze, Mafinga, Katoro, Kahama, Kasulu na mingine mingi ya mikoani inavyokua kwa kasi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…