Serikali iunganishe Dar na Pwani uwe mkoa mmoja uitwe Dar ili watu wazidi kusogea nje ya mji

Pwani nayo ikijaa Tanga iitwe Dar ili watu waende.
Pwani pakijaa na Morogoro iitwe Dar ili watu waamie
Hakuna sehemu nimesema Dar imejaa hoja yangu ya kuongeza ukubwa siyo kwa sababu eti Dar imejaa, Dar bado haijajaa hoja yangu ni Dar ndio mkoa mdogo kuliko yote, yet ndio mkoa wenye idadi kubwa ya watu kuliko yote hii sidhani kama ni sawa
 
Kwahio unaamini kabisa Mkuranga kukiitwa Dar tutaenda kuishi huko?
Absolutely mkuu trust me vijana wengi siyo kwamba hawataki kujenga Pwani eti sababu ni mapori bali sababu ni nje ya Dar, wewe unaweza kuwa hupapendi tu bila kujali panaitwaje ila kuna watu kwao jina la mahali anapoishi matters the most, hata hivyo hoja yangu ya Dar kuunganishwa na Pwani ni kwa sababu Dar ni mkoa mdogo kuliko yote yet ndio the most populous
 
Soon Dar itaungana na hio Pwani kama bado hazijaungana,maanake Dar na Bagamoyo zishaungaba,Kibaha na Dar zishaungana huku kusini sijapita siku nyingi
 
Wazo lako limekuja wakati mwafaka sana hata mm nilikuwaga nawaza hivihivo ingawa kuna baadhi ya wilaya ama kata zipelekwe mikoa ya jirani kwa mfano baadhi ya kata za mkuranga ziende mkoa wa lindi na baadhi za kata za wilaya ya bagamoyo ziende tanga chalinze ziende morogoro na wilaya nzima ya Mafia iende lindi au ipimwe urefu wa mzunguko wa kilomita sitini ndio iwe mpaka wa mkoa wa Daresalaam
 
Hoja yako ina mashiko makubwa sana jiografia yenyewe ya mkoa wa pwani ni mbovu sana mfano;

Upo mkuranga unataka huduma mkoani inakulazimu urudi dar es salaam then uende Kibaha mkoani hiyo sio sawa

Pia kilomita chache tuu kitoka mbande maeneo ya mipeko na singbad pale sio zaidi ya kilomita 6 ila kwenda mkoani ni kibaha wilayani mkuranga kwann pale pasiwe wilaya ya Temeke?
Hili liangaliwe upya kwa sasa
 
Kwani ilivyo hivi sasa inakuzuwia nini kuishi Pwani ukafanya kazi Dar au Kuishi Dar ukafanya kazi Pwani?

Mbona wapo wengi sana wanafanya hivyo?


Dar yote ilikuwa Mkoa wa Pwani mpaka ilivyokatwa na kuwa mkoa wa pekee.
 
Ujinga tu et,, waunge pwan iwe dar kisa tu watu hawataki kuonekana wapo pwan Bali dar,, tena mamlaka washike hapo hapo hakuna kuunganisha mkoa et uitwe dar kisa watu wanataka wasomeke dar,,, hahahahaha Hawa ni wanadaslam ujinga mtupu,,, goja ijae na walundikane tu,, watanunua tu pwan automatic,, bila kulazimishwa hutak nunua kiwanja juu ya nyumba Jenga,,, pia ni ujinga wa darasa la kwanza Yani unalundikana kisa jina darslam duuu,,,,, ujinga hautaisha bongo..Cha msing nikuomba miundombinu iboleshwe huko kama maji, barabara,,hospitality na vtu vingne vya msingi ila sio jina dar,,
 
Kwani ilivyo hivi sasa inakuzuwia nini kuishi Pwani ukafanya kazi Dar au Kuishi Dar ukafanya kazi Pwani?

Mbona wapo wengi sana wanafanya hivyo?


Dar yote ilikuwa Mkoa wa Pwani mpaka ilivyokatwa na kuwa mkoa wa pekee.
Pendekezo lake sio kwa maslahi binafsi ni kwa maslahi ya maendeleo ya taifa

Vijana wengi wamekremu dar ndio kila kitu

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Ndo ile daily watu wataendelea kuuziana viwanja katika makaburi, si wataka uishi dar bana

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…