Serikali iunganishe Dar na Pwani uwe mkoa mmoja uitwe Dar ili watu wazidi kusogea nje ya mji

Ninavyojua mimi ni kwamba serikali ikiona mkoa unakuwa mkubwa inaugawa na sio kuunganisha na mkoa mwingine,
Kwa hiyo kama dar inakuwa na population kubwa ni kuwagawa tu hao watu kuwahamishaia pwani😞 wasisumbue watu wengine 😁😁.
 
Mosi, mkoa wa Pwani umekaa shaghala baghala mno, hata ikitokea inabidi kuungwa na mkoa wa Dar basi italazimu baadhi tu ya maeneo na sio yote...

Pili, serikali imeshashindwa kwenye suala la mipango miji, Dar es Salaam ya leo 90% imejengwa holela. Dar ingekuwa imepangiliwa vizuri mji ungekuwa haujatanuka kama ilivyo kwa sasa...

Hitimisho, kubanana kwa Dar ni matokeo ya serikali hiyo hiyo unayoishauri iunge Dar na Pwani...

Kama wameshindwa control kilometa za mraba za Dar, je wataweza ku control eneo lenye mjumuiko wa Pwani+Dar?
 

Hapo kwenye mipango miji upo sahihi kabisa. Dsm ingepangwa kama ilivyopangwa Lindi mjini na Newala mjini, ingevutia sana.
 
Namuunga mkono mtoa mada ila nadhan kabla ya kuunganisha tungeanza kwanza kwa kuplan kujenga miundombinu na miradi mikubwa nje ya mji mfano Arena, Uwanja wa Mpira bandari kavu, pia kuliko watu wote tuende kariakoo tuache kariakoo iwe soko la nguo na electronics na ijengwe kariakoo nyingine iwe vyombo vya nyumbani labda bagamoyo na kariakoo nyingine kibaha iwe ya home appliance mafridge, washing mashine, generators, microwave.
Mitaa ijengwe either Bagamoyo au Kibaha kulingana na kipato ambapo kipato fulani cha juu wawe na barabara zao ambazo inatoka mfano kuanzia mlandizi, mloganzila hadi katikati ya jiji ambayo inakuwa inalipiwa kwa mwezi licha ya kuwepo kwa mwendo kasi njia ya Bagamoyo na Chalinze
 
Watu tunakaa Mlandizi hata hatujalalamika.
 
Mimi napendekeza jina la Daresalaamu lifutwe.
Badala yake uwe mkoa mmoja tu wa Pwani.
Sababu mojawapo Neno Daresalaam sio la Kibantu.
Daresalaam unaweza kuwa ni mji kama Kinshasa.
Mkoa uitwe PWANI.
 
...Ni vyema TU Ukumbuke kwamba Mpaka Miaka ya 70 Dar na Pwani ulikuwa ni Mkoa mmoja unaoitwa Mkoa wa Pwani.
Wanasiasa ndio wakaugaws ikawa mikoa Miwili tofauti ya Dar na Pwani.
Unachosema ni kuwa turudi Tena huko ila Mkoa uitwe Sasa Dar es Salaam na Sio Pwani Tena. Wazo Zuri. Mikoa imezidi, Watu wanatafutiana vyeo ! [emoji57]

Sent from my TECNO BD4j using JamiiForums mobile app
 
Sisi watu wa Pwani HATUTAKI CONTAMINATIONS
 
Unataka wandengereko wakata miuno wajione wanaishi Dar hapana
 
Mkoa wa Pwani siyo mkubwa kijiografia unaingia mara mbili kwa Morogoro, na pia kuna mikoa mingine mikubwa zaidi kama Lindi na Tabora ila haigawanywi na haileti shida kiutawala, so hata wakiunganisha Dar na Pwani bado haitakuwa kubwa kulinganisha na hiyo mikoa niliyotaja
 
Mimi napendekeza jina la Daresalaamu lifutwe.
Badala yake uwe mkoa mmoja tu wa Pwani.
Sababu mojawapo Neno Daresalaam sio la Kibantu.
Daresalaam unaweza kuwa ni mji kama Kinshasa.
Mkoa uitwe PWANI.
Sahihi kabisa hata mimi hili nimelifikiria pia mkuu, tungeachana tu na hilo jina Dar es salaam hii mikoa iungane halafu uitwe either Pwani au urudie jina la Mzizima, Dar si kiswahili wala kibantu kama ulivyosema
 
Daah hapa nimecheka..nimefikiria, na ikiendelea kujaa t, yoote iitwe pia DAR??

KUNA WATU KAMA NYIE MPO TOFAUTI SANA JMNI, SIJUI MNAWAZAGA NINI,

HONGERA SANA..NIMEKUKUBALI
Tupo Pamoja boss.
 

Mkuu, unafikiri ni kwanini idadi ya mikoa na wilaya zimeongezeka? Ambazo ukitathmini kiundani baadhi hakukuwa na haja ya kufanya hivyo.
SIASA.

Ongezeko la wakuu wa mikoa, wilaya, na wengineo.
Sidhani kama itawezekana. Badala yake utashangaa ndani ya mkoa wa Pwani zinamegwa baadhi ya wilaya kutengeneza mkoa mpya.
 
Wazo zuri. Muhimu serikali kabla ya kuunganisha iweke huduma za msingi kama barabara, shule,masoko,hospital, vituo vya mabasi, daladala, huduma za polisi karibu nk

Viwanja muhimu vipimwe, at least vianzie 30 x 20. Mitaa ta kueleweka.
Serikali ikifanya hivo vitu hata bila kupaita huko sehemu kuwa ni Dar, watu wataenda

Tatizo ni huduma, sio jina
 

Mawazo mazuri sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…