Serikali iunganishe Dar na Pwani uwe mkoa mmoja uitwe Dar ili watu wazidi kusogea nje ya mji

Hakuna sehemu nimesema Dar imejaa hoja yangu ya kuongeza ukubwa siyo kwa sababu eti Dar imejaa, Dar bado haijajaa hoja yangu ni Dar ndio mkoa mdogo kuliko yote, yet ndio mkoa wenye idadi kubwa ya watu kuliko yote hii sidhani kama ni sawa
Mkuu mimi nimekuelewa vizuri sana,hoja yangu iko na mashiko sana.
Ikifanyika hivyo maendeleo yatagawanyika kwa usawa kuliko hali ya sasa ya watu kurundikana na kufanya maendeleo sehemu moja na sehemu zingine zinabaki mapori miaka na miaka.
Ukitembelea hata hapo Kenya kuna utofauti unaona kwenye mikoa yao yote ina mgawanyo sawa wa kimaendeleo na watu hawarundikani sehemu moja.
 
Ndivyo ilikuwa hapo swali kabla ya kugawanywa.

Naunga mkono hoja.Hata hivyo eneo linapokuwa kubwa ndio maendeleo yanachelewa tofauti na eneo la Utawala likiwa dogo.
 
Mawazo kama haya wangekuwa nayo wabunge wetu tungewaona wa maana lakini wao kazi yao ni kugonga meza na kuitikia tu ndiyooooo..!!
 
Wazo zuri.. kijiografia dar ni ndogo sana
 
Wazo la kijinga sana

Baada ya miaka 100 utaunganisha Morogoro na Tanga iwe tena Dar es Salaam maana kote pakua pamejaa?

Solution hapa ni kuendeleza miji mingine nayo iwe mizuri kama Dar watu wahamie au kubaki huko wasilazimike kuja Dar ili Dar isijae ipumue

Cha msingi ndio hicho,lazima kuwe na miji mizuri pembeni across ya country ili kupunguza traffic ya watu kuja Dar
 
H
Kwani ilivyo hivi sasa inakuzuwia nini kuishi Pwani ukafanya kazi Dar au Kuishi Dar ukafanya kazi Pwani?

Mbona wapo wengi sana wanafanya hivyo?


Dar yote ilikuwa Mkoa wa Pwani mpaka ilivyokatwa na kuwa mkoa wa pekee.
Huyo aliyekata ali angalia mahitaji na huduma kwa kipindi hiko, watu walikuwa wachache dar, sasa watu ni wengi ila jiji liko pale pale halija tanuka, ofisi zote yaani kila kitu ni dar, sasa imefika muda serikali kutanua hili jiji kwa maana ya kwamba Kupeleka miundombinu nje ya dar, mfano hii barabara ya njia 4 kutoka kibaha mpaka chalinze, ilitakiwa kila sehemu ijengwe barabara ndefu kama hiyo, mfano kule tegeta piga barabara njia nne mpaka bagamoyo huko mbele kabisa, hivyo hivyo gongolamboto iwe barabara ndefu mpaka kibiti mbele huko... Basi hapo kutakuwa na mwamko mkubwa sana wa watu wataenda kuishi huko
 
Ukifanya hivi huo mkoa wa pwani utakufa sasa, maana pwani yenyewe ina tegemea mapato toka kwenye hizo sehemu maana tayari zime changamka.
 
Ukifanya hivi huo mkoa wa pwani utakufa sasa, maana pwani yenyewe ina tegemea mapato toka kwenye hizo sehemu maana tayari zime changamka.
N kwa sababu hizo sehemu ndizo zilizopakana na Dar
 
Sifahamu hayo unayoyasema yanahusiana nini na kufanywa mkoa mmoja.

Kuwa mkoa zaidi ya mmoja ni kugawa madaraka ya utawala.

Hata Dar yenyewe kuna baadhi ya idara za serikali zimeugawa mkoa kuwa mikoa maalum kiutawala.
 
Kuhusu hiyo aya yako ya mwanzo nilishatoa ufafanuzi kuunganisha Dar na Pwani hakuhusiani na maendeleo ya miji mingine hiyo ni mada nyingine, hoja yangu ni kwamba Dar ndio mkoa mdogo kuliko yote kijiografia ila ndio mkoa mkubwa kuliko yote kidemografia, hivyo kuuunganisha na Pwani kuna afadhali kuliko kuuacha hivi ulivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…