Serikali iwaangalie broiler breeders wanaoshindana na wafugaji wadogo

Serikali iwaangalie broiler breeders wanaoshindana na wafugaji wadogo

Mimi ni mfugaji mdogo so naelewa sana unachomaanisha mkuu.. . Lakini tuko kwemye ulimwengu wa mbwa kala mbwa.... hata serikali ikiingilia bado tu utakuwa na changamoto nyingi.. cha msingi ni kukomaa na wewe uingie kwenye ligi ya wakubwa...
Achana na mambo ya kufuga kuku buku weka target upige hata 2000 au 3000 lakino make sure una system nzuri ya kuuza kabla hujaingiza kuku bandanj....
Kufuga kuku wachache ni stress tu
Mkuu wapo 2200 kwa sasa ila kuna uwoga wa kuexpand zaidi kutokana na hali ya soko.
 
hiyo ni hasara. mathalani chukulia una kuku elfu mbili, itakuchukua muda gani kumaliza kuuza kwa rejareja mfano kuku kumi kwa siku?
Wakifika wiki tano wachinje wahifadhi kwenye freezer.Utaepuka gharama ya chakula.
 
Do you think yote hayo hatufikirii. ni bora atleast iwe kuna katazo na watu wafanye hivyo, kuliko kutokuwa na katazo kabisa
Think bigger bro, Kama mimi ni kampuni x na ukanizuia nisiuze kuku kama wewe, Kesho naenda kufungua kampuni nyingine alafu natumia hiyo kuuza hao kuku..hiyo itakuwa fair au sio? The most adaptive wins always! na its non sense kama kumwomba referee kila ukifungwa magoli mawili lihesabiwe moja kwa sababu timu unayocheza nayo ina wachezaji wakubwa!
ki kweli inaua biashara na hapo ndo innovation inapotakiwa kutumika kushindana nao.
 
Wkifika wiki tano wachinje wahifadhi kwenye freezer.Utaepuka gharama ya chakula.
kuku elfu mbili utawachinja na uanze kuuza rejareja, watakudodea mzee. wengi wanataka fresh chickens
 
Yule jamaa wa Mbezi serikali inabidi imtupie jicho vinginevyo biashara ya kuuza kuku wake awe ana export nje. Kuna jamaa yangu mmoja na yeye ni mfugaji na aliniambia alipoteza mteja wake kutokana na kuingiliwa soko lake na huyo breeder muuza vifaranga na chakula
Kule Mbezi beach sio?
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Imebidi nicheke tu!

Kwahiyo nawewe ukitoka kwenye huo ufugaji mdogo serikali ikudhibiti kuokoa waliopo chini yako?

Acha kufuga kutegemea serikali itakubeba ndio utafika mbali!

Maana tukiendelea hivi wauza maandazi wa mtaani nao watasema serikali imdhibiti bakhresa asiuze maandazi ili kuwa na fair competition!
Duuh umemjibu vyema kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu wapo 2200 kwa sasa ila kuna uwoga wa kuexpand zaidi kutokana na hali ya soko.
Tukomae mkuu mi mwenyewe ndo biashara yangu hii.... hivi huyo jamaa wa mbezi anafugaga kuku wa ngapi maana nshamsikia sana na anauzaga bei gani
 
Mkuu usiwe mkali. Hayo ni mawazo ya watu uliowaletea thread. Sidhani hata asilimia moja ya members humu ni wafugaji. Sasa kwanini umeleta uzi humu? Unless umekosea hadhira.

Kuna mijitu inaropoka matapishi ilihali hata Kuku wa nyama alivyo hawamjui. Stupid Kabisa!!
 
Mkuu ukishasema serikali iliangalie hilo na unasema Hao wafugaji wakubwa wawe breeders tu huko tayari ni kuwadhibiti Hao wafugaji wakubwa Mkuu!
Labda niwe sielewi kiswahili!

Anyway humu jukwaani tupo wengi hebu Uzi ufike page kama tatu hivi tuone mawazo ya wenzetu wengine kama watakuunga mkono
Mtoa mada amesema breeder abaki kuwa breeder na kuuza vifaranga.
 
Rafu kwenye biashara hizi ni kawaida sana. Ila nadhani unaweza kuangalia a different market niche au a different way ya kuuza kuku. Si lazima kuuza kuku mzima. Unaweza ukaamua kufanya some processing kwa kujiunga na wafugaji wengine. Hii ya kila mtu kujifanyia lwake inafaya wafugaji wasiwe na nguvu sokoni. Mfano wafugaji wanaweza kujiunga kwenye vikundi na kuwa na kama abattoir (machinjio) qambapo kuku wanachinjwa na kuwa packed kama ni paja paja, kama ni firigisi ni firigiri, na kama ni miguu ya kuku ni miguu ya kuku. Then you do some cool packaging +branding. That way unaweza ukawa unafanya kitu tofauti kidogo. Ninajua kule uswahili mtu anaweza asiwe na uwezo wa kununua kuku mzima lakini uwezo wake ukaishia kwenye vipapatio. May be ukauza vipapatitio hadi kwenye packaging ya buku. Miguu na vicwwa ukauza kwa packaging ya hadi mia tano tano. Unaweza jikuata unamaximize profit ukilinganisha na kusubiri kuuza kuku mzima. Umoja ndo silaha muhimu kama mnataka kushindana na hawa breeders
 
kuku elfu mbili utawachinja na uanze kuuza rejareja, watakudodea mzee. wengi wanataka fresh chickens

Afu mtu anafikiria kuchinja kuku elfu2 ni kazi ndogo. Afu hata kama ingewezekana hiyo freezer ya kuwajaza hao wote kwa mfugaji kuwa nayo ni shughuli pia. Plus na umeme wetu ghafla ukakatika lazima ule short ya kutisha kwa kuku wote hao
 
Unawadhibiti vp? Ni ngumu sana anaweza kutumia ndugu zake akafuga we utajuaje? Kikubwa pambana na hali yako,pia kumbuka tuko kwenye free market
😂😂😂
Nadhani kama ni kesi umeshaitolea maamuzi mkuu..
 
Kimsingi haiwezekani hapo..
Utetezi utakuwepo ila sio rahisi kudhibiti hilo abadani
 
Back
Top Bottom