Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE JANEJELLY NTATE - SERIKALI IWAANGALIE WATOTO WALIOSITISHA MASOMO KWA SABABU YA VITA UKRAINE 🇺🇦
"Waziri wa Fedha umekubali kupunguza mipaka ya Utawala wako, kukubali Idara ya Mipango irudi kuwa tume ya Mipango. Rasilimali watu iliyopo pale walikuwa hawatumiki ipasavyo sasa hawa Wataalam watakwenda kutumika vizuri na kuongeza uchumi wa Tanzania" - Mhe. Janejelly James Ntate, Mbunge wa Viti Maalum (Wafanyakazi)
"Mliyofanya kwa watumishi watanzania, Mmeorodhesha vitu mlivyofanya. Lakini nashauri sehemu ya madeni au malipo ya watumishi yasiyo ya kimishahara. Naomba ongezeni juhudi hasa kulipa likizo za Walimu, watumishi wa Afya walio kwenye Halmashauri zetu Tanzania" - Mhe. Janejelly James Ntate, Mbunge wa Viti Maalum (Wafanyakazi)
"Niwapongeze, mmeamua wakuu wa Idara stahiki zao zilipwe na Serikali kupitia TAMISEMI. Bajeti iliyopita mliweka posho ya Laki Moja kwa Watendaji wa Kata, posho hii badala ya kujenga imeenda kubomoa. Watumishi hawa posho hii hawalipwi ipasavyo, wengine wanadai mwaka wengine wanadai miezi mitano. Serikali njoni na utaratibu mzuri wa kuwalipa stahiki zao" - Mhe. Janejelly James Ntate, Mbunge wa Viti Maalum (Wafanyakazi)
"Kabla mtumishi hajastaafu hupewa barua ya miezi sita kwamba unaenda kustaafu. Kwanini Serikali msichukue jukumu la kuangalia ni nini kinachodaiwa kwenye mifuko mkakipeleka kuliko mstaafu kashastaafu ndiyo anaanza kuhangaika kufuatilia makato yake na malipo yake kwenye mifuko. Hilo tuliangalie kwa ufasaha zaidi" - Mhe. Janejelly James Ntate, Mbunge wa Viti Maalum (Wafanyakazi)
"Tumeruhusu wanafunzi kutoka Sudan 🇸🇩 kuja kumalizia masomo Tanzania 🇹🇿. Niombe Wizara ya Elimu na Serikali, tuna watoto wetu ambao walirudi kwaajili ya vita Ukraine 🇺🇦 mpaka sasa hatujafanya utaratibu warudi kwenye Vyuo. Hawa watoto wetu wanajisikiaje? Niombe Serikali muwaangalia Wazazi ambao watoto wao walikuwa Ukraine ambao wengine ni madaktari, Wahandisi na taaluma mbalimbali waliokuwa wanakuja kuisaidia nchi. Na wao warudishwe kwenye Vyuo wakaendelee na masomo" - Mhe. Janejelly James Ntate, Mbunge wa Viti Maalum (Wafanyakazi)
"Vituo vya Afya mmejenga kweli kweli lakini hakiwezi kuwa kituo cha Afya bila Wafanyakazi na vitendea kazi. Serikali imeendelea kuajiri lakini tujikite kuajiri Wataalam wa Afya ili vile Vituo visije kugeuka kuwa magofu" - Mhe. Janejelly James Ntate, Mbunge wa Viti Maalum (Wafanyakazi)