Serikali iwapandishe madaraja Walimu wenye Shahada ya Pili (Masters Degree) mara tu baada ya kumaliza masomo yao

Serikali iwapandishe madaraja Walimu wenye Shahada ya Pili (Masters Degree) mara tu baada ya kumaliza masomo yao

Kwani watumishi wote wanalipwa mshahara uniform au sjaelewa unamaanisha nn
Sijui idara yenu Sisi idara yetu Kama mko daraja moja mshahara ni uniform ila pesa ya elimu inaongezeka kulingana na elimu ya mtu.
Mfano mshahara 1000 wote mtalipwa 1000 ila mwenye diploma atalipwa 1000+allowance ya diploma mwenye degree pia hivyo hivyo 1000+allowance ya degree..
Kwahyo mshahara unakua mmoja ila allowance ndio inaongezeka ya elimu(certificate hana allowance ya elimu)
 
Mnachokosea na ambacho hakiwezi kuwapandisha madaraja au mshahara ni kwenda au kusomea Masters ya kozi tofauti na masuala ya Ualimu, hivyo unakosa muendelezo. Iko hivi,waalimu wengi niliowahi kuwaona wanakimbilia kusoma kozi za Utawala na masuala ya Utumishi jambo ambalo haliwaongezei chochote kwenye ukuaji wa kitaaluma ya Ualimu wao labda tu pale watakapopata nafasi za uteuzi za kiuongozi kama vile Mkuu wa shule au Afisa Elimu kwenye ngazi ya Halmashauri.
Hebu soma tena ulichoandika. Unajichanganya sana.

Sent from my M10_Max using JamiiForums mobile app
 
Sijui idara yenu Sisi idara yetu Kama mko daraja moja mshahara ni uniform ila pesa ya elimu inaongezeka kulingana na elimu ya mtu.
Mfano mshahara 1000 wote mtalipwa 1000 ila mwenye diploma atalipwa 1000+allowance ya diploma mwenye degree pia hivyo hivyo 1000+allowance ya degree..
Kwahyo mshahara unakua mmoja ila allowance ndio inaongezeka ya elimu(certificate hana allowance ya elimu)
SHUKRAN KWA UFAFANUZI MKUU🙏🏼
 
Nnachojua,
Mwalimu mwenye
Certificate, anafundisha primary
Diploma, anafundisha olevel
Degree, anafundisha advance
Masters-anafundisha vyuoni

Sasa Kama hutaki kuhama idara,
Unataka ulipwe mshahara wa masters ili ukae bure TU?
Sio kweli Dog.
 
Tunaomba huu Uzi uwafikie viongozi wetu utumishi & Tamisemi
kwasabu
Kama serikali itaitambua Shahada ya Pili ya ualimu hii itakuwa njia mojawapo ya kuupa hadhi zaidi ualimu, Kuna ndugu zetu wapo mashuleni huko Wana masters lakini hawajatajwa popote kwenye hv vyeo😄 Basi serikali iwape walau daraja moja Mara baada ya kuwasilisha vyeti vyao.
 
POLE mwalimu mleta uzi, kimsingi serikali yako haina uwezo wa kuongeza hata buku kwa watumishi wake achilia mbali nyie walimu, chakufanya pambana na ujasiriamali wa pembeni tu vinginevyo ukitegemea hiyo ajira yako tu ya kushika chaki hutoboi
 
Nnachojua,
Mwalimu mwenye
Certificate, anafundisha primary
Diploma, anafundisha olevel
Degree, anafundisha advance
Masters-anafundisha vyuoni

Sasa Kama hutaki kuhama idara,
Unataka ulipwe mshahara wa masters ili ukae bure TU?
hivi unavyojua mambo ni tofauti na uhalisia.
 
Nnachojua,
Mwalimu mwenye
Certificate, anafundisha primary
Diploma, anafundisha olevel
Degree, anafundisha advance
Masters-anafundisha vyuoni

Sasa Kama hutaki kuhama idara,
Unataka ulipwe mshahara wa masters ili ukae bure TU?
Kwenye Ualimu kama umeanza na certificate primary hata ukipata masters utaendelea baki primary, labda upate usimamizi au kazi halmashauri
 
Kwenye Ualimu kama umeanza na certificate primary hata ukipata masters utaendelea baki primary, labda upate usimamizi au kazi halmashauri
Kubaki kufundsha shule ya msingi syo shida, shida Ni pale unapokuwa na masters ambayo haitambuliki kimuundo na Wala haina nyongeza ya mshahara. Mwl kuwa na masters/PhD ni anasa🤣, tunaposema kipaumbele Ni elimu Basi iwe na kwa Elimu za walimu pia
 
Kubaki kufundsha shule ya msingi syo shida, shida Ni pale unapokuwa na masters ambayo haitambuliki kimuundo na Wala haina nyongeza ya mshahara. Mwl kuwa na masters/PhD ni anasa[emoji1787], tunaposema kipaumbele Ni elimu Basi iwe na kwa Elimu za walimu pia
Sasa uwe na masters halafu uendelee kufundisha shule ya msingi, sasa kazi ya masters ni nini hapo?

Watu hawalipwi kwa level ya elimu tu wanalipwa na production/tija wanayoongeza.
 
Nnachojua,
Mwalimu mwenye
Certificate, anafundisha primary
Diploma, anafundisha olevel
Degree, anafundisha advance
Masters-anafundisha vyuoni

Sasa Kama hutaki kuhama idara,
Unataka ulipwe mshahara wa masters ili ukae bure TU?
Siku hizi mpaka hao wa masters wapo Primary mkuu.
 
Serikal kwenye scale za mshahara huwa wanatambua mwisho degree ya kwanza tu ukiwa na masters haitambuliki kwa wote walio chini ya tamisem labda kwenye mataasisi ya utafit so hata huko afya haitambulik iyo masters kwenye mshahara labda kwenye ishu ya taaisis ya utafit mfano NIMR,TAFIRI na kama hayo huko wanaangalia masters mpk phd ila sio uwe tamisemi sisi tupo huku tunajua sn tu
 
Ni miaka mingi Sasa walimu Hawa wenye Shahada ya Pili ya ualimu na wale wenye PhD ya ualimu, wamekuwa hawapati ongezeko lolote la mshahara mara baada ya kumaliza elimu zao za juu, tofauti na ilivyo kwenye idara zingine Kama afya nk. Ambapo Shahada ya Pili huwa inatambuliwa.

Ombi: TUNAOMBA serikali walau iweke utaratibu wa kuwapa hata Daraja moja la mshahara Hawa walimu wenye Shahada ya Pili Mara tu baada ya kumaliza masomo yao. Hii itapunguza kuhangaika kutafuta kujiunga na idara zingine kwa lengo la kupata kipato kinachoendana na taaluma Yao.

Najua Kuna wahusika humu naomba kuwasilisha.
Hivi mwalimu unaenda kusoma masters, ama phd ili iweje, inasaidia kitu gani serikali maana sifa ya mwisho kwa mwalimu ni first degree. Na huwa hakuna mshara wa mwalimu wa masters ila kuna posho tu. Mfano ukiwa headmaster unalipwa posho
 
Unaposema masters ya ualimu unamaanisha nini? Au unamaanisha Master's in Education? Nijuavyo, wengi wa walimu wanaoenda kuchukua masters ni wale wanaochukua one of major teaching subjects. Kwa mfano: kama anafundisha Advanced Mathematics na Physics, akienda kuchukua masters, ataenda kuchukua moja kati ya hayo mawili. Tuchukulie amechukua master's ya Physics, huyu atakuwa na options mbili; either arudi kufundisha au anaweza kwenda kufanya kazi kwenye institutions zinazotumia applied Physics. Kwa hiyo hawafungwi!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa uwe na masters halafu uendelee kufundisha shule ya msingi, sasa kazi ya masters ni nini hapo?

Watu hawalipwi kwa level ya elimu tu wanalipwa na production/tija wanayoongeza.
Aisee we jamaa kumbe kupambanua Mambo sifuri kabisa, unapimaje tija na hyo production, unahoja hopeles kabisa🤣
 
Back
Top Bottom