Uchafu wote huu unaandika na mifano isiyo na kichwa wala miguu. Www ina umuhimu gani zaidi ya usalama wa nchi yetu? Maana huyo Www watu wanatumia vibaya na inaleta madhara kwa jamii. Mfano Usa mpaka sasa kuna tatizo la watu kutengeneza chuki baina ya matabaaka kupitia mitandao. Unadhani hakuna censorship?
Usidhani watu wote humu wanatoa maoni yao wanapinga serikali kufungia mitandao.Serikali haijafunga internet unavyofikiri wewe labda imedhibiti mitandao ya kijamii ambayo ndio
www.Ingefunga internet usingeweza kwenda kuchukua hela crdb acha kuichafua serikali kwa kutojua kwako na ushabiki.Tatizo ni wewe mtoa mada maneno unayotoa.Mtu atajiuliza uko sayari gani dunia hii.Elewa wanao comment humu wengi ni wazalendo wa nguvu pengine kuliko wewe na tena wana CCM tatizo unavo comment inawatia hasira mtu wanayejaribu kumuelimisha una mawazo ya kizamani mno how come uongelee hardcopy ya vitabu shuleni kwanza shule zingine havipo lakini mtandaoni mtu anasoma.How come mtu akuambie mambo ya e-commerce wewe unaongelea mambo ya kununua mihogo na nyanya gengeni hivi unafikiri kila mtu anaishi uswahilini.Mimi sijapinga wazo lako ila nilichogundua ulikuwa hujui kutofautisha kati ya internet na mitandao ya kijamii ni sawa na kulinganisha bahari na maziwa na mito vyote uviite bahari kisa tu vina maji ndani yake.Ila nimekugundua ifuatavyo:-
1.Kwa vyovyo utakuwa una elimu flani otherwise usingeweza kutoa baadhi ya comment ninazoona ila elimu yako kuhusu internet sio kubwa na ndo maana mimi mtaalamu wa IT nikaona sio kukuelimisha wewe mtoa mada ni kuchangia ili wana JF wengine wafahamu mtu hawezi kuwa mtaalamu wa kila fani.
2.Hata kama umesoma au hujasoma huna discipline au kwa kifupi huna hekima na busara kutokana na maneno machafu unayotumia nashangaa kwanini JF wasikupe ban.Hivyi unajua wako wasomi lakini ni wabwiya unga na bangi.
3.Kama ni well educated na muelewa unafanya makusudi kukoroga mada ili uone reaction za watu zitakuwaje kuhusu hili sakata la mambo ya mitandao kama ni hivyo basi utakuwa ni mtu muelewa mno.Unajua unachofanya
4.Huna ufahamu humu wachangiaji wengine si vijana wadogo unavyofikiria mtandao huu na mingine kuna watu wazima pengine wengine wanaweza kuwa mama au baba zako lakini hujui.Unapomtusi mtu ikatokea siku moja ukaona mfano AVATAR ni baba yako mzazi au mama yako mzazi utajisikia vibaya sana
Mtu akitumia muda wake mwingi kuelimisha jamii kwa lugha staha usimjibu kijeuri na matusi otherwise huo uzalendo wako utakuwa bendera fuata upepo tafuta kitabu cha shaban Robert kuna shairi linaitwa Mfua bati kisha soma
Ajabu unaongelea serikali ifikirie kuhusu kurudisha internet wakati unatumia JF ambayo ni sehemu ya hiyo internet unayoongelea