Serikali iwe makini, isikurupuke kurudisha mtandao wa intaneti

Mkuu, nimeandika nikafuta mara kadhaa, lakini itoshe kusema haujui unachokipigania. Swali dogo tu, ikiwa unaipongeza serikali kukata mawasiliano hayo, mbona upo hapa ? Mbona umefanya kila juhudi uwe kwenye mtandao ?.
Nafikiri hujasoma nilichoandika na kukielewa.
 
Dah! Happy
Biashara za kuuza kupitia mtandao bongo? Nyumba hazijapangiliwa na hao ndio huwa wa kwanza huko uswahilini kuuana kwa kusiliza uongo wa kwenye mitandao.

Kusoma kwa kutumia internet ni uvivu wa kusoma vitabu ndio maana ubongo wako unawaza uharo
Eti kusoma kwa kutumia internet ni uvivu! Dah! Bado upo mbali miaka ya 1942. Pole sana
 
Nadhani unapngelea ushabiki tu na sijui Kama unajua ni kiasi gani watu wamepoteza wakati mitandao.Na sidhani Kama unajua ni watu wangapi waliokuwa wanategemea Internet katika biashara,masomo,kupashana habari nk lkn wewe uko rigid na huoni what are the impacts hata kwa nchi ni kiasi imepoteza kiuchumi.Madhara yaliyopatikana kiuchumi ni makubwa Sana.Tafakari Sana.
 
Biashara za kuuza kupitia mtandao bongo? Nyumba hazijapangiliwa na hao ndio huwa wa kwanza huko uswahilini kuuana kwa kusiliza uongo wa kwenye mitandao.

Kusoma kwa kutumia internet ni uvivu wa kusoma vitabu ndio maana ubongo wako unawaza uharo
Wewe bado ni kilaza vitabu viko kwenye internet funguka nani anayetegemea hard copy huo ni usomaji wa stone age siyo Sasa.
 
Mkuu umefikiria athari zake kwa watu ambao hufanya biashara zao online? Applications za job na hata vitu vingine muhimu vinavyofanyika online ?
Yangetokea machafuko hizo biashara zingefanyika? Maduka na hasara kiasi gani ingetokea kwa vitu kuchomwa na kuibwa?
 
Yani kuna baadhi ya Watanzania ni wajinga kuliko hata huyo Bashite, Kila mtu anajipendekeza kwa Jiwe mpaka inakera
 
Mtandao wa internet 😁😂😂😂😂😁😁😁
 
Hahaha we genius sana, kwanini usiwashauri wakazima kwa miaka 10 kabisa.
 
Mleta maada katumia VPN. Moja kwa moja inaonesha hii hali ya net kukata hajaipenda
 
Biashara za kuuza kupitia mtandao bongo? Nyumba hazijapangiliwa na hao ndio huwa wa kwanza huko uswahilini kuuana kwa kusiliza uongo wa kwenye mitandao.

Kusoma kwa kutumia internet ni uvivu wa kusoma vitabu ndio maana ubongo wako unawaza uharo
Usidhani mtazamo wako ni sawa na uhalisia ulivyo,kuna Biashara nyingi sana hifanyika online, hata Vitabu na majarida na pia updates mbalimbali kuhusu vitu vilivyoandikwa na vikafanyiwa research tena kwa umakini utavikuta online kila sku sasa wewe unapinga hili dah sijui ww ni kiumbe wa namna gani
 
Hanijui, uzalendo na mapenzi kwa taifa langu ndio maana nasema ukweli.
Unamawazo mgando sana,
Hivi pia huwa mnaelewa kweli nini maana ya UZALENDO au huwa mnaropokarokapo tuu?
 
Ww kwa vile unamkono serikalini waambie wasirudishe kabisa ili kuhakikisha kwanza Tanzania inakua km ulaya, zanzibar ubar inakua km Dubai, tanga inakua km Singapore na arusha unakua km calfornia....
 
Hofu ya nini nchi hii kama Tanzania, kwani watu tunapata huduma za kimtandao kama kawaida
 
Hii nchi ina maadui wengi sana wa kiuchumi na kisiasa ambao hawaitakii mema. Hivyo serikali iwe makini...
Mimi ni mwana CCM Mwenzako na Shabiki 'tukuka' kabisa wa Rais Dk. Magufuli na hata 'Kura' yangu nimempa Yeye, ila kwa hili lililofanywa na TCRA siliungi mkono tena kwa 100% kwani ni la 'Kipumbavu / Kipopoma' mno. Nimesikitia umekuja na huu Uzi wako huku ukiwa na 'Hoja' za 'Kitoto' na 'Dhaifu' kabisa huku ukinipa 'Mashaka' kama huko Chuo Kikuu ulikosoma ulistahili kweli Kusoma.

Kwa Kukutaarifu tu sasa ni kwamba GENTAMYCINE nimebahatika kupita katika Taasisi kadhaa za Serikali hapa Mkoani Dar es Salaam na hata kukutana na Watendaji baadhi na wote 'wamechukizwa' na 'kusikitishwa' na huu 'Upumbavu' unaoutetea hapa uliofanywa na hawa TCRA. Watafute Watu wa TRA wakupe 'Mrejesho' mzima wa 'Hasara' ambayo nchi imeipata kutokana na huu 'Upumbavu' wa waliotuzimia.

Najua kwakuwa 'Kichwani' Kwako ni 'Mtupu' hili hulijui na sasa nakupa kwamba baada ya hawa TCRA 'Kuamuru' haya Makampuni ya Simu yarudishe 'Huduma' za Mtandao 'yamegoma' na wanachofanya ni Kuwasha tu 'Kimtindo' kisha 'wanazima' au kufanya Mtandao uwe 'Slow' ili tu na Wao 'Kuwakomoa' hawa TCRA wako. Na nasikia kuna Kampuni Kubwa tu ya Kimarekani inataka ilipwe ndiyo ibonyeze Kitufe cha Internet.

Namalizia kwa Kukuuliza je, umeshajua ni kwanini hivi sasa kuna Ulinzi mkubwa, mkali na umakini mwingi pale Kijitonyama katika Ofisi za Posta? Kwakuwa Kichwani mwako ni 'Mtupu' siwezi Kukupa Kinachoendelea na Kilichosababisha. Sasa kama hawa TCRA wako 'unaowatetea' hapa wamezima Mtandao mbona Watanzania wenye 'Akili' kuliko wao bado tunaendelea tu Kutumia Mtandao kutoka nchi zingine Duniani?

Amani au Ustawi wa nchi hauletwi kwa 'Wapumbavu' kadhaa Kuamua 'Kipumbavu' tu 'Kuzima' Mtandao bali ni kwa wenye Mamlaka Kuongoza au Kutawala kwa Haki huku wakikubali 'Kukosolewa' ili wawe 'imara' zaidi. Na kama kuna Serikali ambayo ilipaswa iheshimu sana Mitandao na Maoni yetu Sisi 'Keyboard Warriors' basi ni hii ya sasa kwani 'tunaisaidia' kuliko vile inavyodhani kwa 'Kuwaibulia' mengi tu wasiyoyajua.

Na usichokijua Mitandao hii hii unayosema inaleta 'Vita' ndiyo hii hii ikitumika vyema ndiyo 'Kinara' wa Kuleta Amani hapa Duniani. Amekera sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…