Jamani eeeeh sio lazima wote tujipendekeze kwa mfalme ili tule. Wengine tukalime.
Intaneti ni nyenzo muhimu sana yenye matumizi makubwa kuliko hizo siasa zenu za kilevi.
Biashara, maswala mbalimbali ya kitaaluma, vyote vinategemea intaneti kwa kiasi kikubwa katika nyakati hizi.
Msiwafanye watanzania wote kuwa wahanga na mateka wa siasa zenu za kubabaisha na za kuunga unga kwa propaganda za kuokoteza.
Mara sijui tunapambana na maadui?
Maadui gani mnaopambana nao ninyi Tanganyika? Kanchi dhaifu kasikojulikana hata kwenye ramani ya dunia!
Hebu wacheni siasa za kitoto.