Hayo maeneo yote yalianzishwa na Muzungu kwa ajili ya Muzungu na Muhindi, sisi maeneo yetu yalikuwa Magomeni, Temeke, na kwingineko, lkn mpaka leo hii tumeshindwa kabisa kuanzisha maeneo yetu mapya yenye hadhi na mazingira ya kuvutia kama vile ilivyo O'bey, Masaki au Upanga, sasa ni kwa nini? Nyerere alijaribu kuanzisha Sinza ambayo labda ingekuwa kama Upanga lkn matokeo yake uchafu tu, akaanzisha Mbezi Beach ambayo ndiyo ilipaswa kuwa O'bey yetu alifanikiwa mwanzoni Mbezi beach ilikuwa upscale lkn sasa hivi Mbezi beach haina tofauti na Mwenge, Magomeni au Kigogo, uchafu kila mahali, bodaboda wauza miwa mihogo barabarani, mvua zikinyesha ni maji hayapiti wamejenga kwenye mito, maeneo ya wazi yamejengwa yote hakuna parks, public beach kama Coco hakuna wamejenga hotels na mavila yao na kuziba kila kitu, Upanga, O'bey, Ada estate bado yanabakia kuwa maeneo mazuri na tulivu yasiyo na kelele na ushenzi, kwa nini? Sasa hivi wamehamia sijui Mbweni, kunavutia kwa sasa muda si mrefu Wahamiaji kutoka Mikoani watajaa wataleta bodaboda, wauza juice chafu, Makanisa ya kilokole kelele usiku kucha na itageuka Kimara Baruti.
Kwa nini tunashindwa kujenga maeneo mazuri na tulivu ya kuishi kwa raha na amani?