Hivi ni kwanini tumeshindwa kujenga O'bey, Masaki, Ada Estate au Upanga nyingine?

Barbarosa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2015
Posts
22,583
Reaction score
27,838
Hayo maeneo yote yalianzishwa na Muzungu kwa ajili ya Muzungu na Muhindi, sisi maeneo yetu yalikuwa Magomeni, Temeke, na kwingineko, lkn mpaka leo hii tumeshindwa kabisa kuanzisha maeneo yetu mapya yenye hadhi na mazingira ya kuvutia kama vile ilivyo O'bey, Masaki au Upanga, sasa ni kwanini?

Nyerere alijaribu kuanzisha Sinza ambayo labda ingekuwa kama Upanga lkn matokeo yake uchafu tu. Akaanzisha Mbezi Beach ambayo ndiyo ilipaswa kuwa O'bey yetu alifanikiwa mwanzoni Mbezi Beach ilikuwa upscale lkn sasa hivi Mbezi beach haina tofauti na Mwenge, Magomeni au Kigogo, uchafu kila mahali, bodaboda wauza miwa mihogo barabarani, mvua zikinyesha ni maji hayapiti wamejenga kwenye mito, maeneo ya wazi yamejengwa yote hakuna parks, public beach kama Coco hakuna wamejenga hotels na mavila yao na kuziba kila kitu

Upanga, O'bey, Ada Estate bado yanabakia kuwa maeneo mazuri na tulivu yasiyo na kelele na ushenzi, kwa nini? Sasa hivi wamehamia sijui Mbweni, kunavutia kwa sasa muda si mrefu Wahamiaji kutoka Mikoani watajaa wataleta bodaboda, wauza juice chafu, Makanisa ya kilokole kelele usiku kucha na itageuka Kimara Baruti.

Kwa nini tunashindwa kujenga maeneo mazuri na tulivu ya kuishi kwa raha na amani?
 
Mitaa yenyewe unayoitaja haijajengwa kwa utaratibu, ni mitaa ya hovyo hovyo tu ila ina nyumba nzuri nzuri.

Kinachotofautisha masaki na mbagala ni thamani ya nyumba lakini sio mpangilio wa mitaa na ubora wa nyumba zilizoko huko.

Kwa mpangilio wa mitaa masaki, Ada estate na obey haina tofauti na gongo la mboto au mbagala.

Hii nchi kwenye mipango miji na mitaa ni sifuri, hakuna mahala tumefanikiwa. Dodoma wale cda walipaswa kupewa kesi za uhujumu uchumi.
 
Huwezi kuamini maeneo karibu yote yenye mpangalio mzuri wa mji pale wanaita CENTRAL BUSSINESS DISTRICT iwe ni Dar, Arusha, Mwanza, Tanga, Moshi, Dodoma, Mbeya, Tabora, Moro, Singida, Bukoba, etc palipangwa ama na Mjerumani au Mwingereza kuanzia mwaka 1880-1920 au 1920-1961.

Walipojenga wabongo ikiwa ni pamoja na mzee wa sifa ndio huko Manzese, Buguruni, Changanyikeni, Masika

Waafrika hatuna utaratibu na hatuthamini systematic process na planning. Huwezi kuamini mji ulioko katikati mahali pazuri kama Chalinze hauna mpango wowote, mji unakuwa tu kama kijiji cha huko porini.

Miji yote Tz inajengeka hovyo, ile mipango miji waliondoka nayo wakoloni na ni miaka 60 sasa baada ya uhuru, mambo ni hovyo.
 
Kwani huko mlijenga nyinyi mpaka mjue jinsi ya kuzijenga kwingine?
 
Shida ni maeneo mengi wananchi ndo wameachiwa wapange miji na mitaa.....sasa ndo unapokutana na viwanja vya 10x10.......mtu mwenye kiwanja cha namna hii ukimwambia toa mita moja ya njia hatoi!
 
Hiyo mitaa ya ada estate o bey na masaki.. tumejiuzia wenyewe wazawa. Tumeanza kuifanya kama temeke na mbagala.. vinyumba kibao
 
Kwa watu wa CCM mliopo humu ambao at least nawaonaga mna akili kidogo ni wewe na Johnthebabtist.

Nirudi kwenye mada yako! Jibu la hayo yote uliyoandika hapo ni Sera mbovu za Chama chako na kukosa kwa akili kwa watu wa Chama chako ambao wamekuwa wakiiongoza hii nchi miaka nenda rudi kulikosababisha haya yote.

Nashukuru Mungu nimetembea nchi nyingi na nimefanya research ya kutosha. Tanzania kwa kifupi ni takataka kwenye suala la kupangilia makazi na miji yetu.

Mara nyingine huwa nafikiria kuwa ni bora mzungu angetutawala muda mrefu at least angetupangia miji yetu na maeneo yetu na kutuacha tukiishi kistaarabu.

Hata ukipita masaki saivi ni uchafu mtupu. Majengo yanajengwa hovyo bila mpangilio. Sehemu za makazi zinakuwa za biashara alafu ni biashara kichaa cha pubs za restaurants. Hakuna tena ile decency ya zamani ya oysterbay na masaki.

Maeneo mengine ndo uchafu mtupu. Makazi yanejengwa hovyo na wala hatajapangwa. Kila mtu anajiamulia ajenge anavyoona yeye sawa. Kila nyumba kuna fremu, barabarani ni vibanda vya machinga kila kona, huyu anauza mahindi, huyu nguo , huyu kaweka vyombo barabarani.

Tanzania kwa kifupi imeoza, mfano dar tu, maeneo yaliyokuwa yamependezeshwa vizuri saivi yamejaa vibanda vya hovyo hovyo na hayatamaniki tena. Mpaka Mlimani City saivi kwa nje kuna uchafu wa vibanda vya wamachinga, nenda njia ya cocacola ambayo miaka ya nyuma ilikuwa inapendeza saivi ni vibanda kila kona na uchafu mtupu.

Nchi nyingi za Africa zimeanzisha projects za satellite cities. Rwanda wanajenga kama mbili na Kagame keshafungua moja juzijuzi. Senegal wanajenga yao kubwa balaa na ya kisasa kupindukia, Kenya pia wanajenga zao mbili na ziko vizuri na Madagascar pia.

Sie huku kazi yetu ni kusifu na kuabudu upuuzi tu. Hakuna lolote la maana tunalofanya. Hatuna project yeyote ile. Mtu kiongozi anasimama anasema Eti machinga ruksa kufanya biashara sehemu yeyote ile. Ndo mana Tanzania karibu kila sehemu ni takataka.

Kuanzia Songwe, Mbeya, Iringa, Morogoro,Pwani, Dar , Mwanza , Arusha,Dodoma, kigoma , Tabora na sehemu zingine zote ni uchafu tu.

Nilikuwa nakipenda sana na kukissuport Chama cha Mapinduzi hapo awali ila nilivyozidi kupata exposure nimekuja ku gundua kuwa tumefanya makosa sana kuwaacha waendelee kututawala. Wameifanya nchi hii na maisha ya watu wa nchi hii kuwa ya hovyo sana.

Jambo linaloniuma ni kuwa kwa CCM kushindwa kusimamia vizuri suala la makazi, imepelekea watanzania wengi hadi kuona kuwa wao kuishi vizuri sehemu zilizopangwa vizuri na kujengwa vizuri ni anasa.

Shame!!!
 
Mitaa yenyewe unayoitaja haijajengwa kwa utaratibu, ni mitaa ya hovyo hivyo tu ila ina nyumba nzuri nzuri.

Kinachotofautisha masaki na mbagala ni thamani ya nyumba lakini sio mpangilio wa mitaa na ubora wa nyumba zilizoko huko.

Kwa mpangilio wa mitaa masaki, Ada estate na obey haina tofauti na gongo la mboto au mbagala.

Hii nchi kwenye mipango miji na mitaa ni sifuri, hakuna mahala tumefanikiwa. Dodoma wale cda walipaswa kupewa kezi za uhujumu uchumi.
Lawama kwa Chama cha Mapinduzi
 
Huwezi kuamini maeneo karibu yote yenye mpangalio mzuri wa mji pale wanaita CENTRAL BUSSINESS DISTRICT iwe ni Dar, Arusha, Mwanza, Tanga, Moshi, Dodoma, Mbeya, Tabora, Moro, Singida, Bukoba, etc palipangwa ama na Mjerumani au Mwingereza kuanzia mwaka 1880-1920 au 1920-1961. Walipojenga wabongo ikiwa ni pamoja na mzee wa sifa ndio huko Manzese, Buguruni, Changanyikeni, Masika,....Waafrika hatuna utaratibu na hatuthamini systematic process na planning. Huwezi kuamini mji ulioko katikati mahali pazuri kama Chalinze hauna mpango wowote, mji unakuwa tu kama kijiji cha huko porini. Miji yote Tz inajengeka hovyo, ile mipango miji waliondoka nayo wakoloni na ni miaka 60 sasa baada ya uhuru, mambo ni hovyo.
Tilizoea kuishi maporini unategemea mambo ya planning ya miji tuijulie wapi haya mambo tuwaachie mabeberu wapange miji yao sisi tushazoea kukata pori tunajenga
 
Huwezi kuamini maeneo karibu yote yenye mpangalio mzuri wa mji pale wanaita CENTRAL BUSSINESS DISTRICT iwe ni Dar, Arusha, Mwanza, Tanga, Moshi, Dodoma, Mbeya, Tabora, Moro, Singida, Bukoba, etc palipangwa ama na Mjerumani au Mwingereza kuanzia mwaka 1880-1920 au 1920-1961. Walipojenga wabongo ikiwa ni pamoja na mzee wa sifa ndio huko Manzese, Buguruni, Changanyikeni, Masika,....Waafrika hatuna utaratibu na hatuthamini systematic process na planning. Huwezi kuamini mji ulioko katikati mahali pazuri kama Chalinze hauna mpango wowote, mji unakuwa tu kama kijiji cha huko porini. Miji yote Tz inajengeka hovyo, ile mipango miji waliondoka nayo wakoloni na ni miaka 60 sasa baada ya uhuru, mambo ni hovyo.
Usiseme waafrika, sema CCM. Botswana ni Africa lakini mipango miji ni top notch.
 
Kwa watu wa CCM mliopo humu ambao at least nawaonaga mna akili kidogo ni wewe na Johnthebabtist.

Nirudi kwenye mada yako! Jibu la hayo yote uliyoandika hapo ni Sera mbovu za Chama chako na kukosa kwa akili kwa watu wa Chama chako ambao wamekuwa wakiiongoza hii nchi miaka nenda rudi kulikosababisha haya yote.

Nashukuru Mungu nimetembea nchi nyingi na nimefanya research ya kutosha. Tanzania kwa kifupi ni takataka kwenye suala la kupangilia makazi na miji yetu.

Mara nyingine huwa nafikiria kuwa ni bora mzungu angetutawala muda mrefu at least angetupangia miji yetu na maeneo yetu na kutuacha tukiishi kistaarabu.

Hata ukipita masaki saivi ni uchafu mtupu. Majengo yanajengwa hovyo bila mpangilio. Sehemu za makazi zinakuwa za biashara alafu ni biashara kichaa cha pubs za restaurants. Hakuna tena ile decency ya zamani ya oysterbay na masaki.

Maeneo mengine ndo uchafu mtupu. Makazi yanejengwa hovyo na wala hatajapangwa. Kila mtu anajiamulia ajenge anavyoona yeye sawa. Kila nyumba kuna fremu, barabarani ni vibanda vya machinga kila kona, huyu anauza mahindi, huyu nguo , huyu kaweka vyombo barabarani.

Tanzania kwa kifupi imeoza, mfano dar tu, maeneo yaliyokuwa yamependezeshwa vizuri saivi yamejaa vibanda vya hovyo hovyo na hayatamaniki tena. Mpaka Mlimani City saivi kwa nje kuna uchafu wa vibanda vya wamachinga, nenda njia ya cocacola ambayo miaka ya nyuma ilikuwa inapendeza saivi ni vibanda kila kona na uchafu mtupu.

Nchi nyingi za Africa zimeanzisha projects za satellite cities. Rwanda wanajenga kama mbili na Kagame keshafungua moja juzijuzi. Senegal wanajenga yao kubwa balaa na ya kisasa kupindukia, Kenya pia wanajenga zao mbili na ziko vizuri na Madagascar pia.

Sie huku kazi yetu ni kusifu na kuabudu upuuzi tu. Hakuna lolote la maana tunalofanya. Hatuna project yeyote ile. Mtu kiongozi anasimama anasema Eti machinga ruksa kufanya biashara sehemu yeyote ile. Ndo mana Tanzania karibu kila sehemu ni takataka.

Kuanzia Songwe, Mbeya, Iringa, Morogoro,Pwani, Dar , Mwanza , Arusha,Dodoma, kigoma , Tabora na sehemu zingine zote ni uchafu tu.

Nilikuwa nakipenda sana na kukissuport Chama cha Mapinduzi hapo awali ila nilivyozidi kupata exposure nimekuja ku gundua kuwa tumefanya makosa sana kuwaacha waendelee kututawala. Wameifanya nchi hii na maisha ya watu wa nchi hii kuwa ya hovyo sana.

Jambo linaloniuma ni kuwa kwa CCM kushindwa kusimamia vizuri suala la makazi, imepelekea watanzania wengi hadi kuona kuwa wao kuishi vizuri sehemu zilizopangwa vizuri na kujengwa vizuri ni anasa.

Shame!!!
MUNGU akubariki mkuu umenena vema
 
Nina sababu nyingi sana za kutoipigia kura CCM na moja wapo ni hii. Tanzania tuna makazi na mpangilio wa miji mbovu sana . Na bahati mbaya kila siku ni bora ya Jana. Huyu magufuli ndo ameharibu kabisa. Saivi mpaka barabara za mitaa ya ikulu na karibia na ikulu kuna uchafu wa vibanda vya wamachinga. Posta iliyokuwa safi kipindi cha Kandoro saivi ni uchafu mtupu.
 
Back
Top Bottom