Hivi ni kwanini tumeshindwa kujenga O'bey, Masaki, Ada Estate au Upanga nyingine?

Hayo maeneo yote yalianzishwa na Muzungu kwa ajili ya Muzungu na Muhindi, sisi maeneo yetu yalikuwa Magomeni, Temeke, na kwingineko, lkn mpaka leo hii tumeshindwa kabisa kuanzisha maeneo yetu mapya yenye hadhi na mazingira ya kuvutia kama vile ilivyo O'bey, Masaki au Upanga, sasa ni kwanini?

Nyerere alijaribu kuanzisha Sinza ambayo labda ingekuwa kama Upanga lkn matokeo yake uchafu tu. Akaanzisha Mbezi Beach ambayo ndiyo ilipaswa kuwa O'bey yetu alifanikiwa mwanzoni Mbezi Beach ilikuwa upscale lkn sasa hivi Mbezi beach haina tofauti na Mwenge, Magomeni au Kigogo, uchafu kila mahali, bodaboda wauza miwa mihogo barabarani, mvua zikinyesha ni maji hayapiti wamejenga kwenye mito, maeneo ya wazi yamejengwa yote hakuna parks, public beach kama Coco hakuna wamejenga hotels na mavila yao na kuziba kila kitu,

Upanga, O'bey, Ada estate bado yanabakia kuwa maeneo mazuri na tulivu yasiyo na kelele na ushenzi, kwa nini? Sasa hivi wamehamia sijui Mbweni, kunavutia kwa sasa muda si mrefu Wahamiaji kutoka Mikoani watajaa wataleta bodaboda, wauza juice chafu, Makanisa ya kilokole kelele usiku kucha na itageuka Kimara Baruti.

Kwa nini tunashindwa kujenga maeneo mazuri na tulivu ya kuishi kwa raha na amani?
Watabuni na kujenga Masaki na O’bay kwa mtaji gani wa uzoefu?
Mtu katoka bush, halafu ndio mkurugenzi wa mipango miji, unategemea nini hapo.
Hata huko Masaki, O’bay anakusikia tu, hajawahi kuishi huko, naye anakaa Bonyokwa!
 
In other words GPA ifanye ku include ubunifu/creativity...na pia wawe exposed na jinsi nchi nyingine zinavyotengeneza miji yao..
Sure my dear I wonder huku watu wamekumbatia GPA kuliko ubunifu, hata elimu kwa wenzetu ni very simple inayo encourage ubunifu na ku solve changamoto za jamii husika while huku kwetu tuna cremisha sijui Keynesian theory, Rostows development theory wakati applicability yake huku kwetu ni tofauti kabisa
 
Singida wanajitahidi kwa kuupanga mji,,tatizo wakazi wamekomaa na nyumba za 1947
 
Kwa watu wa CCM mliopo humu ambao at least nawaonaga mna akili kidogo ni wewe na Johnthebabtist.

Nirudi kwenye mada yako! Jibu la hayo yote uliyoandika hapo ni Sera mbovu za Chama chako na kukosa kwa akili kwa watu wa Chama chako ambao wamekuwa wakiiongoza hii nchi miaka nenda rudi kulikosababisha haya yote.

Nashukuru Mungu nimetembea nchi nyingi na nimefanya research ya kutosha. Tanzania kwa kifupi ni takataka kwenye suala la kupangilia makazi na miji yetu.

Mara nyingine huwa nafikiria kuwa ni bora mzungu angetutawala muda mrefu at least angetupangia miji yetu na maeneo yetu na kutuacha tukiishi kistaarabu.

Hata ukipita masaki saivi ni uchafu mtupu. Majengo yanajengwa hovyo bila mpangilio. Sehemu za makazi zinakuwa za biashara alafu ni biashara kichaa cha pubs za restaurants. Hakuna tena ile decency ya zamani ya oysterbay na masaki.

Maeneo mengine ndo uchafu mtupu. Makazi yanejengwa hovyo na wala hatajapangwa. Kila mtu anajiamulia ajenge anavyoona yeye sawa. Kila nyumba kuna fremu, barabarani ni vibanda vya machinga kila kona, huyu anauza mahindi, huyu nguo , huyu kaweka vyombo barabarani.

Tanzania kwa kifupi imeoza, mfano dar tu, maeneo yaliyokuwa yamependezeshwa vizuri saivi yamejaa vibanda vya hovyo hovyo na hayatamaniki tena. Mpaka Mlimani City saivi kwa nje kuna uchafu wa vibanda vya wamachinga, nenda njia ya cocacola ambayo miaka ya nyuma ilikuwa inapendeza saivi ni vibanda kila kona na uchafu mtupu.

Nchi nyingi za Africa zimeanzisha projects za satellite cities. Rwanda wanajenga kama mbili na Kagame keshafungua moja juzijuzi. Senegal wanajenga yao kubwa balaa na ya kisasa kupindukia, Kenya pia wanajenga zao mbili na ziko vizuri na Madagascar pia.

Sie huku kazi yetu ni kusifu na kuabudu upuuzi tu. Hakuna lolote la maana tunalofanya. Hatuna project yeyote ile. Mtu kiongozi anasimama anasema Eti machinga ruksa kufanya biashara sehemu yeyote ile. Ndo mana Tanzania karibu kila sehemu ni takataka.

Kuanzia Songwe, Mbeya, Iringa, Morogoro,Pwani, Dar , Mwanza , Arusha,Dodoma, kigoma , Tabora na sehemu zingine zote ni uchafu tu.

Nilikuwa nakipenda sana na kukissuport Chama cha Mapinduzi hapo awali ila nilivyozidi kupata exposure nimekuja ku gundua kuwa tumefanya makosa sana kuwaacha waendelee kututawala. Wameifanya nchi hii na maisha ya watu wa nchi hii kuwa ya hovyo sana.

Jambo linaloniuma ni kuwa kwa CCM kushindwa kusimamia vizuri suala la makazi, imepelekea watanzania wengi hadi kuona kuwa wao kuishi vizuri sehemu zilizopangwa vizuri na kujengwa vizuri ni anasa.

Shame!!!
Umeongea ukweli mtupu Tz ni Takataka,miji yetu ni hovyo nenda Harare uone mji ulivyopangika tunashindwa kwenda kujifunza kwa wenzetu?
 
Wacha watu wajitafutie chakula Mzee, wewe unaita uchafu mwenzio ndo anapokula na kuvaa sababu ya hivyo vibanda unvyoita uchafu.
 
Na nyie ndo mnaofanya hii nchi iwe ya kishenzi. Polee sana.

Soma mada kwa kutulia alafu ndo toa mawazo yako. Hakuna mtu anayepinga watu kujitafutia. Suala ni hao watu wapangiwe maeneo maalum yaliyojengwa vizuri na kisasa, yenye miundombinu Bora inayopendeza.

Tatizo CCM imewafanya mfikiri kuwa kuishi vizuri katika maeneo mazuri ni kama bahati tu kumbe ndo hivyo mnavyotakiwa kuishi.
 
Huwezi kuamini maeneo karibu yote yenye mpangalio mzuri wa mji pale wanaita CENTRAL BUSSINESS DISTRICT iwe ni Dar, Arusha, Mwanza, Tanga, Moshi, Dodoma, Mbeya, Tabora, Moro, Singida, Bukoba, etc palipangwa ama na Mjerumani au Mwingereza kuanzia mwaka 1880-1920 au 1920-1961.

Walipojenga wabongo ikiwa ni pamoja na mzee wa sifa ndio huko Manzese, Buguruni, Changanyikeni, Masika

Waafrika hatuna utaratibu na hatuthamini systematic process na planning. Huwezi kuamini mji ulioko katikati mahali pazuri kama Chalinze hauna mpango wowote, mji unakuwa tu kama kijiji cha huko porini.

Miji yote Tz inajengeka hovyo, ile mipango miji waliondoka nayo wakoloni na ni miaka 60 sasa baada ya uhuru, mambo ni hovyo.
Alafu cha kusikitisha kuna wataalam wanazalishwa kila mwaka na vyuo kama Ardhi University. Kuna maprofesa kabisa wa haya mambo ila ndo hivyo wanabaki kujisifu tu na PhD zao
 
Na nyie ndo mnaofanya hii nchi iwe ya kishenzi. Polee sana.

Soma mada kwa kutulia alafu ndo toa mawazo yako. Hakuna mtu anayepinga watu kujitafutia. Suala ni hao watu wapangiwe maeneo maalum yaliyojengwa vizuri na kisasa, yenye miundombinu Bora inayopendeza.

Tatizo CCM imewafanya mfikiri kuwa kuishi vizuri katika maeneo mazuri ni kama bahati tu kumbe ndo hivyo mnavyotakiwa kuishi.
Mtazamo wako ndo wenye changamoto, tunaishi vizuri tu. Mimi binafsi sikwaziki na kuwepo kwa vibanda kila mahali.
 
Idara ya ardhi, mipango miji haijielewi. Viwanja vinagawiwa bila ya kupimwa, na hakuna utaratibu wa nyumba za eneo au mtaa fulani ziwe vipi kimuonekano unaofanana au mpangilio.
 
Tilizoea kuishi maporini unategemea mambo ya planning ya miji tuijulie wapi haya mambo tuwaachie mabeberu wapange miji yao sisi tushazoea kukata pori tunajenga
Hiu ni Kweli mkuu,hapa niko na mdogo wangu tukicheza cheza cheza juu ya miti huku tukila matunda na asali na baadae tutaenda kuiba mahindi ya wanakijiji,na jua likipoa tunarudi zetu kulala huko mtini.
 
Kule kuna sewerage system, pia mpangilio wa nyumba ilikuwa mzuri, miti ilipandwa ikapendezesha maeneo yale.
Sidhani kama huko mbweni wamejenga sewerage system, au kuna vyoo na matanki ya maji machafu.
 
Hio ilikua enzi hizo siku hizi kule kumejaa baa za kutosha na maduka ya mangi.
 
Back
Top Bottom