Viol
JF-Expert Member
- Dec 15, 2009
- 25,419
- 18,372
Huo mtaa upo wapi
Umemaliza, tufunge mjadala ili wenzetu waendelee kumsifu "mungu" wao ambaye ni mfano wa kuigwa duniani.Kwa watu wa CCM mliopo humu ambao at least nawaonaga mna akili kidogo ni wewe na Johnthebabtist.
Nirudi kwenye mada yako! Jibu la hayo yote uliyoandika hapo ni Sera mbovu za Chama chako na kukosa kwa akili kwa watu wa Chama chako ambao wamekuwa wakiiongoza hii nchi miaka nenda rudi kulikosababisha haya yote.
Nashukuru Mungu nimetembea nchi nyingi na nimefanya research ya kutosha. Tanzania kwa kifupi ni takataka kwenye suala la kupangilia makazi na miji yetu.
Mara nyingine huwa nafikiria kuwa ni bora mzungu angetutawala muda mrefu at least angetupangia miji yetu na maeneo yetu na kutuacha tukiishi kistaarabu.
Hata ukipita masaki saivi ni uchafu mtupu. Majengo yanajengwa hovyo bila mpangilio. Sehemu za makazi zinakuwa za biashara alafu ni biashara kichaa cha pubs za restaurants. Hakuna tena ile decency ya zamani ya oysterbay na masaki.
Maeneo mengine ndo uchafu mtupu. Makazi yanejengwa hovyo na wala hatajapangwa. Kila mtu anajiamulia ajenge anavyoona yeye sawa. Kila nyumba kuna fremu, barabarani ni vibanda vya machinga kila kona, huyu anauza mahindi, huyu nguo , huyu kaweka vyombo barabarani.
Tanzania kwa kifupi imeoza, mfano dar tu, maeneo yaliyokuwa yamependezeshwa vizuri saivi yamejaa vibanda vya hovyo hovyo na hayatamaniki tena. Mpaka Mlimani City saivi kwa nje kuna uchafu wa vibanda vya wamachinga, nenda njia ya cocacola ambayo miaka ya nyuma ilikuwa inapendeza saivi ni vibanda kila kona na uchafu mtupu.
Nchi nyingi za Africa zimeanzisha projects za satellite cities. Rwanda wanajenga kama mbili na Kagame keshafungua moja juzijuzi. Senegal wanajenga yao kubwa balaa na ya kisasa kupindukia, Kenya pia wanajenga zao mbili na ziko vizuri na Madagascar pia.
Sie huku kazi yetu ni kusifu na kuabudu upuuzi tu. Hakuna lolote la maana tunalofanya. Hatuna project yeyote ile. Mtu kiongozi anasimama anasema Eti machinga ruksa kufanya biashara sehemu yeyote ile. Ndo mana Tanzania karibu kila sehemu ni takataka.
Kuanzia Songwe, Mbeya, Iringa, Morogoro,Pwani, Dar , Mwanza , Arusha,Dodoma, kigoma , Tabora na sehemu zingine zote ni uchafu tu.
Nilikuwa nakipenda sana na kukissuport Chama cha Mapinduzi hapo awali ila nilivyozidi kupata exposure nimekuja ku gundua kuwa tumefanya makosa sana kuwaacha waendelee kututawala. Wameifanya nchi hii na maisha ya watu wa nchi hii kuwa ya hovyo sana.
Jambo linaloniuma ni kuwa kwa CCM kushindwa kusimamia vizuri suala la makazi, imepelekea watanzania wengi hadi kuona kuwa wao kuishi vizuri sehemu zilizopangwa vizuri na kujengwa vizuri ni anasa.
Shame!!!
Amina mkuu. Kuishi Tanzania tunavumilia mengi sana kwa kweli. Hii nchi sijui Kwa nini bado tunaendelea kuiamini CCMMUNGU akubariki mkuu umenena vema
Botswana ni mabeberu?Tilizoea kuishi maporini unategemea mambo ya planning ya miji tuijulie wapi haya mambo tuwaachie mabeberu wapange miji yao sisi tushazoea kukata pori tunajenga
Nimepita Dodoma juzi kumeshakuwa hovyo, watu wengi kuliko uwezo wa mjiTunaijenga Dodoma
Wanasikitisha kwa kweli. Hii nchi inabidi ipate kiongozi kama yule mfalme wa Dubai ambaye atabomoa mitaa na kuijenga upya. Ni aibu kwa kweli ukitembea TanzaniaUmemaliza, tufunge mjadala ili wenzetu waendelee kumsifu "mungu" wao ambaye ni mfano wa kuigwa duniani.
Tofauti kati yetu na wenye miji iliyopangwa ni kuwa wakati wao miji inajengwa na taasisi sisi inajengwa na watu binafsiSerikali iingilie,mtu akitaka kununua na kujenga kitu lazima aombe permission na akionyesha hataleta madhara kwenye mipango mji ndio aruhusiwe...
Second, ni kuimpose structer rules,kwa wanaodump uchafu iwe mtu mmoja au familia..walipishwe fines za kutosha
Watanzania wengi ni wajinga bado mkuu mpaka kizazi hiki kifutike mkuu .Amina mkuu. Kuishi Tanzania tunavumilia mengi sana kwa kweli. Hii nchi sijui Kwa nini bado tunaendelea kuiamini CCM
Nenda Gaborone tu pale uone tofauti. Unapita mitaa unaona ilivyopangwa vizuri. Makazi yanaeleweka. Sehemu ya makazi ni makazi na sehemu ya biashara ni biashara.Hata huko Masaki kuko hovyo, obey kunatia aibu Bora hata bunju kwa Sasa kuko vizuri kidogo
Inawezekana walikaa na mabeberu kwa muda mrefuBotswana ni mabeberu?
Sahihi kabisa ujinga ni tatizo kuu kwa watanzania wengi. Ni upuuzi unaokera na kusikitisha sanaW
Watanzania wengi ni wajinga bado mkuu mpaka kizazi hiki kifutike mkuu .
Wasomi wetu wa mipango miji wanachozingatia ni kupata gpa kubwa basi.Huwezi kuamini maeneo karibu yote yenye mpangalio mzuri wa mji pale wanaita CENTRAL BUSSINESS DISTRICT iwe ni Dar, Arusha, Mwanza, Tanga, Moshi, Dodoma, Mbeya, Tabora, Moro, Singida, Bukoba, etc palipangwa ama na Mjerumani au Mwingereza kuanzia mwaka 1880-1920 au 1920-1961.
Walipojenga wabongo ikiwa ni pamoja na mzee wa sifa ndio huko Manzese, Buguruni, Changanyikeni, Masika
Waafrika hatuna utaratibu na hatuthamini systematic process na planning. Huwezi kuamini mji ulioko katikati mahali pazuri kama Chalinze hauna mpango wowote, mji unakuwa tu kama kijiji cha huko porini.
Miji yote Tz inajengeka hovyo, ile mipango miji waliondoka nayo wakoloni na ni miaka 60 sasa baada ya uhuru, mambo ni hovyo.
Hawa watu ni ovyo kabisa sijafaham wanapangilia nini jamani kama kwa arusha hali ni mbaya kuna wengine hawana hata njia za kupita kurudi makwao pia kwanzia uhuru mpaka leo kuna viwanja havijahakikiwa wala kujulikana na huezi pangilia kitu usichokifaham kiukweli tz tupo tupo tu .....lakini tusiishie kulaumu nini kifanyike ?Waulize watu wa halmashauri. Watu hawana upeo wala maono. Ni moja ya sababu naunga mkono MAGU kutowaongezea mishahara wafanyakazi wa serikali -tena ikiwezekana wapunguziwe- hawa watu hawafanyi kazi zao.
Nchi yetu inahitaji mabadiliko makubwa ya kifikra na kiuongozi hata na mifumo ili wataalamu watumike effectively, huku bongo nyumba za makazi, hapo hapo biashara nyumba zimebanana hamna hata garden au miti kupo kupo tu hovyo, very shame, na Sasa hivi nchi nzima imekuwa takataka kila mahali vibanda vya machinga na maturubali kila sehemu zimekuwa soko waweza ingia bank pembeni ukakuta muuza vitunguu na nyanya inasikitisha Sana, jamani viongozi wenye dhamana tumieni vizuri nafasi zenu kuleta mabadiliko chanya.Nenda Gaborone tu pale uone tofauti. Unapita mitaa unaona ilivyopangwa vizuri. Makazi yanaeleweka. Sehemu ya makazi ni makazi na sehemu ya biashara ni biashara.
Ukipata barabarani Gaborone huoni mavibanda vibanda. Barabara ziko nyeupe na safi hadi miundombinu inapendeza.
Sie tumejenga fly-over Ubungo ila hata huoni uzuri wake. Pembeni tu na chini ni mavibanda ya machinga yamejazana hovyo hovyo.
Tunajenga njia sita sijui nane kimara hadi Kibaha ila hata haipendezi. Ni mavibanda tu ya machinga yamejaa pembeni. Sehemu za makazi unakuta mabiashara na sehemu za biashara ndo kumewekwa hoehae.
Nawaambia nchi hii ikitaka mabadiriko ya kweli na chanya hii CCM ni kuitoa kabisa madarakani