Hivi ni kwanini tumeshindwa kujenga O'bey, Masaki, Ada Estate au Upanga nyingine?

Wacha watu wajitafutie chakula Mzee, wewe unaita uchafu mwenzio ndo anapokula na kuvaa sababu ya hivyo vibanda unvyoita uchafu.
Wew unaonekana mmachinga, kwani kwa wenzetu hakuna hao watu lakin wanafanya kwa mpangilio na ustaarabu wa hali ya juu.. bongo hatuna ustaarabu
 
Kuwa na nyumba za zamani au nyumba za miti sio tatizo, tatizo ni mpangilio wa miji na mitaa. Nyumba itazamwe wapi na geti liwe wapi hata kama nyumba ni ya miti
Singida viongozi wao wanajua nini wanafanya,barabara lami,mkandarasi walipatia sana,,taa za barabarani karibu mitaa yote ya mjini kati,wamejitahidi sana.
 
"Mipango Miji" Ni sayansi na Sanaa ya kutumia physical infrastructure kuinfuence human and social behaviour. Miji kwa maana ya majengo, barabara, bustani shule, vyuo nk ni hardware.. mifumo ya kuongozi, kiulinzi, kiuchumi inakuwa software na kazi ya vyote hivi Ni kufanya maisha ya mwanadamu rahisi na Bora.

Mtaalamu wa Mipango Miji yeye anakuwa kiungo katika jitihada za kukamilisha azma hii. Mosi anakusanya taarifa, anakusanya mahitaji, anajua rasilimali zilizopo na namna zinavyoweza kutumika kuleta tija kwa kila sekta inayohusika bila upotevu mkubwa.

Kwa kifupi haiwezekani kufanya Mipango ya kimaendeleo ndani ya mji au nchi Kama hauna taarifa Muhimu za kimipango miji. Mfano utajiuliza tangu Uhuru hatujawahi kuwa na sensa ya nyumba na makazi, Sasa tunajuaje mahitaji ya umeme, maji barabara..au tunajuaje hali ya uhitaji wa makazi Bora nchini!?

Pamoja na umuhimu mkubwa Bado Kuna shida maana Mipango Miji haijawa kipaumbele nchini. Jitihada za Mwl. Nyerere na Vijiji vya ujamaa ilikuwa Ni moja kati ya initiative kubwa kabisa ambazo hazikusimamiwa kuona matunda yake. Na huenda hii inatokana na kile Hayati Mzee Mkapa alichowahi kusema "We are more concerned of here and now...." Tunapenda majibu rahisi na njia za mkato Hilo ni tatizo kubwa Kama nitakavyoeleza huko mbeleni.

Kwanza kabla ya yote naomba tuondoke kichwani na hiki "Mipango Miji ni mfumo was kusimamia rasilimali na haijalishi hizi rasilimali ni za nani." Mipango Miji hodari itashughulika mpaka na namna unavyotumia pesa zako mf. Namna utajenga, wapi utawekeza kwa kiwango gani nk. Pili, ufanisi wa Mipango Miji utauona katika machaguo ya watu.. afya zao nk. Hushangai kwann watu kutoka nchi zilizoendelea kamwe hawajengi kwenye mazagazaga!? Sababu kinachopangwa Ni akili(machaguo) mitaa na barabara navinginevyo Ni matokeo ya machaguo tu (Garbage in Garbage Out)

Sasa tuendelee kwa nn tumeshindwa kutengeneza Masaki nyingine. Jibu ni rahisi tu, rasilimali watu haijaandaliwa kuishi mjini. Kwa kifupi Miji yetu ni Vijiji vikubwa tu. Ni makusanyiko makubwa ya wanavijiji na ndio maana inabehave kiajabu ajabu. Kukaa Dar es salam hakukufanyi kuwa wa mjini automatically. Kuna namna unapaswa kubehave ili uwe was mjini.

Ndugu zangu kinachoyafanya maeneo haya tajwa kuwa Bora Ni ubora wanaoishi ndani yake (kwa maana ya tabia za kimjini) lakini uendelevu wake unakuwa matatani maana warithi wapya wa maeneo haya ni wauza dagaa kutoka mwaloni Magu na matokeo yake uhitaji wa magenge, wauza miwa na vibanda vya hovyo hovyo unaanza kushamiri.

Wapendwa hapa ndipo ukweli mchungu unapoanza kujitokeza. Usipokuwa na utaratibu wa kupanga mambo yako basi kubangaiza ndio inakuwa njia ya maisha. Na Japo wengi tumekuzwa na maisha ya namna hii na wengi Bado tunaishi bila kupanga, lakini ukweli wa mambo huu sio mfumo rafiki sana wa kujiendesha. Maana utaishi kwa kudra za Mwenyezi Mungu tu, upate ukose ili mradi siku zinasonga tu ufe au upige bubaa.

Unapokuwa na wananchi sehemu kubwa ikiishi chini ya mfumo huu lazima utazalisha viongozi na uendeshaji nchi watakaokuwa na akili na Mawazo ya namna hiyo hiyo. Nchi itabehave hivyo hivyo. Kujiendesha kwa matukio na uwekezaji usiokuwa na muendelezo (continuation). Na matokeo ndio mfumo huu unaouna tunaoutumia kujenga Miji.

Sasa kujibu swali lako kwa Nini tumeshindwa kujenga Miji ya mfano wa Capri-point (mwanza), Shanty town (Moshi), Gangilonga (Iringa) Masaki (Dsm) sababu zinaweza kuwa nyingi lakini nitajitahidi kuangazia chache.

Kwanza kabisa ni kukosekana kwa uthubutu wa kisiasa. Wanasiasa kutokana na mambo mengi ila sana kukosa nia ya dhati ya Kuongoza na kugeukia kuwapendeza wananchi ili wapewe "kula" wamejikuta mambo yote yenye maana ya kujenga wanakimbia wanageukia kuwa maadvocate wa wananchi dhidi ya mfumo. Wamegeuka madalali na masterminds wa kupoka maeneo ya wazi na maeneo mengine Muhimu kuwafaa marafiki wao matajiri. Waliouza maeneo ya wazi ni wanasiasa/viongozi na wamewezeshwa na watumishi/wataalamu we waaminifu.

Pili ni kuongezeka kwa wimbi la wananchi wanaojichukulia sheria mkononi pamoja na udhaifu ya mifumo ya usimamizi. Hivi vyote vinakwenda bega kwa bega, Kama yai na kuku, Ni ngumu kusema kipi kilianza ila Ni wazi vyote vinamchango mkubwa sana kupelekea hali iliyopo. Hebu tujiulize wauza miwa na mama ntilie wote ukitoa kuiona kesho wanania na Malengo gani ya baadae!? Tungeweza kusimamia Miji vizuri Hawa katika umoja wao wangeweza kukua na kuwa biashara kubwa au kupata ajira rafiki na salama katika biashara kubwa na zilizokua tayari.

Tatu Kama taifa kushindwa kuwa na dira ya Taifa kwa namna inayotekelezeka. Mkoloni alipofika alifanya survey Kisha akapanga kwa namna iliyo suit matakwa yake. Akajenga reli, barabara na bandari kwa namna ambayo ingesaidia kudrain resources za nchi hii kirahisi. Na sisi Kama tuna nia ya kunyanyua maisha ya kila mtu nchini lazima tuanzia chini kabisa Kisha tuichambue nia yetu kuona kila mtu anashiriki vipi na mchango wake unalindwa. Mf. Lazima wawekezaji walindwe sawa sawa na mlaji, mahusiano yao yawe symbiotic. Kwa namna hiyo muwekezaji anakuwa na uwezo was kupata soko, mlaji anauhakika wa kupata bidhaa au Huduma, mkopeshaji(benki Kama ipo) inapata Kurejesha fedha zake na Serikali inapata Kodi. Mmoja akiacha kulindwa kinachotokea ni ukwapuaji na kufilisika na Biashara kufungwa Kisha tunarudi kwenye kubangaiza just to get by.

Naomba nieleweke pamoja na kila mmoja wetu kuwa na makosa yake kwenye hili, kuanzia wajumbe wanaotupa wagombea wasio mahiri😂🇹🇿 mpaka watendaji wasio kuwa committed Bado Kuna Yale ya sisi wanamipango Miji na kilio changu Ni kuona tunakuja na namna Bora ya kuyachuja Mawazo na mapendekezo ya wananchi Kisha kuyatengenezea mifumo ya utekelezaji unaohusisha kila mtu kwa maendeleo endelevu.

Poleni nimejaribu kwenda kila Kona pamoja na upana wa mada hii na majibu ya wanajanvi, swala Hili ni pana sana na lingependeza kama TOT Bonanza ijayo litapata round table tujadiliane kwa upana.

Wenu Mtiifu Mnyeyekevu
Mwana Mipango Miji.
0752415293
 
Sisi hatuna Urban Planning. Tunayo "world wild west".
Tumejikombia kwa baadhi ya mambo to some extent, lakini hili limetushinda kabisa na kwa sasa wapiga kura kuruhusiwa kufanya biashara mahali popote ndio kabisa.
 
Basi wewe Ni binaadamu wa ajabu au mbinafsi kupindukia. Haupendi order(utaratibu) kitu kinachoweza kukuweka katika kundi la watu wenye tabia wasiostaarabika mbaya!
Mtazamo wako ndo wenye changamoto, tunaishi vizuri tu. Mimi binafsi sikwaziki na kuwepo kwa vibanda kila mahali.
 
Dodoma ndo habari ya mjini kwa sasa , ila naiona ikikosewa kabisa kuwa na mpango mji, baadaye itakuja kubomolewa ili ipangwe ,
kuna nyumba zinajengwa bila mpangilio na zipo ndani ya radius ya km Kumi kutoka centre. mamlaka kama hazioni
Dodoma Hakuna la maana kule juu ya pestana club Kuna mji ukipita hapa unatokea chooni kwa mtu
 
"Mipango Miji" Ni sayansi na Sanaa ya kutumia physical infrastructure kuinfuence human and social behaviour. Miji kwa maana ya majengo, barabara, bustani shule, vyuo nk ni hardware.. mifumo ya kuongozi, kiulinzi, kiuchumi inakuwa software na kazi ya vyote hivi Ni kufanya maisha ya mwanadamu rahisi na Bora.

Mtaalamu wa Mipango Miji yeye anakuwa kiungo katika jitihada za kukamilisha azma hii. Mosi anakusanya taarifa, anakusanya mahitaji, anajua rasilimali zilizopo na namna zinavyoweza kutumika kuleta tija kwa kila sekta inayohusika bila upotevu mkubwa.

Kwa kifupi haiwezekani kufanya Mipango ya kimaendeleo ndani ya mji au nchi Kama hauna taarifa Muhimu za kimipango miji. Mfano utajiuliza tangu Uhuru hatujawahi kuwa na sensa ya nyumba na makazi, Sasa tunajuaje mahitaji ya umeme, maji barabara..au tunajuaje hali ya uhitaji wa makazi Bora nchini!?

Pamoja na umuhimu mkubwa Bado Kuna shida maana Mipango Miji haijawa kipaumbele nchini. Jitihada za Mwl. Nyerere na Vijiji vya ujamaa ilikuwa Ni moja kati ya initiative kubwa kabisa ambazo hazikusimamiwa kuona matunda yake. Na huenda hii inatokana na kile Hayati Mzee Mkapa alichowahi kusema "We are more concerned of here and now...." Tunapenda majibu rahisi na njia za mkato Hilo ni tatizo kubwa Kama nitakavyoeleza huko mbeleni.

Kwanza kabla ya yote naomba tuondoke kichwani na hiki "Mipango Miji ni mfumo was kusimamia rasilimali na haijalishi hizi rasilimali ni za nani." Mipango Miji hodari itashughulika mpaka na namna unavyotumia pesa zako mf. Namna utajenga, wapi utawekeza kwa kiwango gani nk. Pili, ufanisi wa Mipango Miji utauona katika machaguo ya watu.. afya zao nk. Hushangai kwann watu kutoka nchi zilizoendelea kamwe hawajengi kwenye mazagazaga!? Sababu kinachopangwa Ni akili(machaguo) mitaa na barabara navinginevyo Ni matokeo ya machaguo tu (Garbage in Garbage Out)

Sasa tuendelee kwa nn tumeshindwa kutengeneza Masaki nyingine. Jibu ni rahisi tu, rasilimali watu haijaandaliwa kuishi mjini. Kwa kifupi Miji yetu ni Vijiji vikubwa tu. Ni makusanyiko makubwa ya wanavijiji na ndio maana inabehave kiajabu ajabu. Kukaa Dar es salam hakukufanyi kuwa wa mjini automatically. Kuna namna unapaswa kubehave ili uwe was mjini.

Ndugu zangu kinachoyafanya maeneo haya tajwa kuwa Bora Ni ubora wanaoishi ndani yake (kwa maana ya tabia za kimjini) lakini uendelevu wake unakuwa matatani maana warithi wapya wa maeneo haya ni wauza dagaa kutoka mwaloni Magu na matokeo yake uhitaji wa magenge, wauza miwa na vibanda vya hovyo hovyo unaanza kushamiri.

Wapendwa hapa ndipo ukweli mchungu unapoanza kujitokeza. Usipokuwa na utaratibu wa kupanga mambo yako basi kubangaiza ndio inakuwa njia ya maisha. Na Japo wengi tumekuzwa na maisha ya namna hii na wengi Bado tunaishi bila kupanga, lakini ukweli wa mambo huu sio mfumo rafiki sana wa kujiendesha. Maana utaishi kwa kudra za Mwenyezi Mungu tu, upate ukose ili mradi siku zinasonga tu ufe au upige bubaa.

Unapokuwa na wananchi sehemu kubwa ikiishi chini ya mfumo huu lazima utazalisha viongozi na uendeshaji nchi watakaokuwa na akili na Mawazo ya namna hiyo hiyo. Nchi itabehave hivyo hivyo. Kujiendesha kwa matukio na uwekezaji usiokuwa na muendelezo (continuation). Na matokeo ndio mfumo huu unaouna tunaoutumia kujenga Miji.

Sasa kujibu swali lako kwa Nini tumeshindwa kujenga Miji ya mfano wa Capri-point (mwanza), Shanty town (Moshi), Gangilonga (Iringa) Masaki (Dsm) sababu zinaweza kuwa nyingi lakini nitajitahidi kuangazia chache.

Kwanza kabisa ni kukosekana kwa uthubutu wa kisiasa. Wanasiasa kutokana na mambo mengi ila sana kukosa nia ya dhati ya Kuongoza na kugeukia kuwapendeza wananchi ili wapewe "kula" wamejikuta mambo yote yenye maana ya kujenga wanakimbia wanageukia kuwa maadvocate wa wananchi dhidi ya mfumo. Wamegeuka madalali na masterminds wa kupoka maeneo ya wazi na maeneo mengine Muhimu kuwafaa marafiki wao matajiri. Waliouza maeneo ya wazi ni wanasiasa/viongozi na wamewezeshwa na watumishi/wataalamu we waaminifu.

Pili ni kuongezeka kwa wimbi la wananchi wanaojichukulia sheria mkononi pamoja na udhaifu ya mifumo ya usimamizi. Hivi vyote vinakwenda bega kwa bega, Kama yai na kuku, Ni ngumu kusema kipi kilianza ila Ni wazi vyote vinamchango mkubwa sana kupelekea hali iliyopo. Hebu tujiulize wauza miwa na mama ntilie wote ukitoa kuiona kesho wanania na Malengo gani ya baadae!? Tungeweza kusimamia Miji vizuri Hawa katika umoja wao wangeweza kukua na kuwa biashara kubwa au kupata ajira rafiki na salama katika biashara kubwa na zilizokua tayari.

Tatu Kama taifa kushindwa kuwa na dira ya Taifa kwa namna inayotekelezeka. Mkoloni alipofika alifanya survey Kisha akapanga kwa namna iliyo suit matakwa yake. Akajenga reli, barabara na bandari kwa namna ambayo ingesaidia kudrain resources za nchi hii kirahisi. Na sisi Kama tuna nia ya kunyanyua maisha ya kila mtu nchini lazima tuanzia chini kabisa Kisha tuichambue nia yetu kuona kila mtu anashiriki vipi na mchango wake unalindwa. Mf. Lazima wawekezaji walindwe sawa sawa na mlaji, mahusiano yao yawe symbiotic. Kwa namna hiyo muwekezaji anakuwa na uwezo was kupata soko, mlaji anauhakika wa kupata bidhaa au Huduma, mkopeshaji(benki Kama ipo) inapata Kurejesha fedha zake na Serikali inapata Kodi. Mmoja akiacha kulindwa kinachotokea ni ukwapuaji na kufilisika na Biashara kufungwa Kisha tunarudi kwenye kubangaiza just to get by.

Naomba nieleweke pamoja na kila mmoja wetu kuwa na makosa yake kwenye hili, kuanzia wajumbe wanaotupa wagombea wasio mahiri😂🇹🇿 mpaka watendaji wasio kuwa committed Bado Kuna Yale ya sisi wanamipango Miji na kilio changu Ni kuona tunakuja na namna Bora ya kuyachuja Mawazo na mapendekezo ya wananchi Kisha kuyatengenezea mifumo ya utekelezaji unaohusisha kila mtu kwa maendeleo endelevu.

Poleni nimejaribu kwenda kila Kona pamoja na upana wa mada hii na majibu ya wanajanvi, swala Hili ni pana sana na lingependeza kama TOT Bonanza ijayo litapata round table tujadiliane kwa upana.

Wenu Mtiifu Mnyeyekevu
Mwana Mipango Miji.
0752415293
Asante sana
 
Jamani, Hebu waacheni wapigakura wangu wafanye biashara kokote, serikali yangu ni kwaajili ya wanyonge, hata ukitaka kufanya biashara katikati ya barabara , kaweke kibanda chako pale, ha ha kwakweli Mimi naipenda ccm lakini kwa mipango miji imefeli sana, Tena sana
 
Hayo maeneo yote yalianzishwa na Muzungu kwa ajili ya Muzungu na Muhindi, sisi maeneo yetu yalikuwa Magomeni, Temeke, na kwingineko, lkn mpaka leo hii tumeshindwa kabisa kuanzisha maeneo yetu mapya yenye hadhi na mazingira ya kuvutia kama vile ilivyo O'bey, Masaki au Upanga, sasa ni kwanini?

Nyerere alijaribu kuanzisha Sinza ambayo labda ingekuwa kama Upanga lkn matokeo yake uchafu tu. Akaanzisha Mbezi Beach ambayo ndiyo ilipaswa kuwa O'bey yetu alifanikiwa mwanzoni Mbezi Beach ilikuwa upscale lkn sasa hivi Mbezi beach haina tofauti na Mwenge, Magomeni au Kigogo, uchafu kila mahali, bodaboda wauza miwa mihogo barabarani, mvua zikinyesha ni maji hayapiti wamejenga kwenye mito, maeneo ya wazi yamejengwa yote hakuna parks, public beach kama Coco hakuna wamejenga hotels na mavila yao na kuziba kila kitu

Upanga, O'bey, Ada Estate bado yanabakia kuwa maeneo mazuri na tulivu yasiyo na kelele na ushenzi, kwa nini? Sasa hivi wamehamia sijui Mbweni, kunavutia kwa sasa muda si mrefu Wahamiaji kutoka Mikoani watajaa wataleta bodaboda, wauza juice chafu, Makanisa ya kilokole kelele usiku kucha na itageuka Kimara Baruti.

Kwa nini tunashindwa kujenga maeneo mazuri na tulivu ya kuishi kwa raha na amani?
Hahaa eti wahamiaji kutoka mikoani
 
Back
Top Bottom