Serikali iwe makini na suala la Ngorongoro. Tunaweza tukaharibu umuhimu wa kufanya filamu ya Royal Tour na tukaathiri sekta ya utalii

Serikali iwe makini na suala la Ngorongoro. Tunaweza tukaharibu umuhimu wa kufanya filamu ya Royal Tour na tukaathiri sekta ya utalii

mazaga one

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2015
Posts
2,514
Reaction score
4,042
Serikali kuweni makini sana na Hili Jambo.Mimi kama mwana CCM na Mtanzania,naweza kusema hili jambo mlimalize kwa ustaarabu Mkubwa.

Mnaweza mkawapa maadui wetu kutusemea vibaya,na mwishoe Watalii wakaogopa Kuja Tanzania.Serikalini kuweni makini sana nawahusia.

Tumetumia gharama kufanya Filamu ya Royal tour. Basi tutumie pia nafasi hii kuwahakikishia Watalii ya kuwa Tanzania hakuna hayo ambayo yanaripotiwa kuhusu Ngorongoro tutajiharibia na kuharibu Sekta ya Utalii wetu tunaotumia nguvu Kubwa kuutangaza.
 
Sio iwe makini wakati watu wanakufa iache mambo ya kifara na ndio ijitafakari na kuacha upumbavu Nchi inawatu wa ovyo kabisa hii [emoji35][emoji35][emoji35][emoji35][emoji2959][emoji2959][emoji2959][emoji2959]
 
Waangalie negative impacts kuliko haya yanayoendelea...Unajua Kuna watu huja kutalii kwa kusikia Tanzania Kuna Mbuga Wamasai na Wanyama wanaishi kwa pamojaa.Sijui serikali yetu inawaza nini
 
Kwenye filamu yao ya royal tour wameonekana wamasai na imetajwa ni moja ya vivutio vya utalii..

Ghafla tu tunaambiwa na hao hao hao wamasai hawatakiwi kuishi huko mbugani na wanafukuza wanyama..!

Hii ndiyo bongo bwana,wizi wa nje nje
 
Kweli kabisa.

Na wanapaswa kujua kwamba wamasai na wanyama n kama ndg.

Wanyama nao wakikasirika itakuwa balaa. (Hapa sio utani) Utashangaa hata hao watalii wanajeruhiwa.

Hizo bicon kwanini huko tu? Waweke na kwenye mapori mengine huko tabora. Ambayo Hata hayakaliwi na watu.

Au wanaogopa koboko??
 
Back
Top Bottom