Serikali iwe moja na iitwe Zanzibar, capital iwe ZNZ Town kama ilivokuwa 1700s

Serikali iwe moja na iitwe Zanzibar, capital iwe ZNZ Town kama ilivokuwa 1700s

Bin Faza

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2013
Posts
502
Reaction score
191
Wananchi Wezangu,

Nami leo ninapenda kutowa maoni yangu, ingawaje sidhani kwamba jaji Warioba na kundi lake watayasikia maoni haya.

Kwanza ningependa kuyapa uzito maoni yangu kwa kuweka hii map ya Zanzibar ya mwaka 1886, kabla ya mile 10 za fukwe ya Tanganyika na Kenya kukodishwa kwa miaka 99 kwa wajerumani na waingereza.

Kabla ya wazungu kuifanya ramani hii, tanganyika ilikuwa ni sehemu ya Zanzibar, mjerumani ikaipora sehemu hiyo na kuifanya koloni lake.

Mimi ninaamini moyoni kwamba sisi wazanaibari na watanganyika ni wamoja kidamu na tulikuwa raia wa nchi moja, sulatanate of zanzibar,

Kwa mtazamo huo na tufanye tu nchi moja lakini iitwe zanzibar na capital city yake iwe znz town, na musiseme znz town ni mji mdogo kuwa capital, kwani dodoma hakuna kitu chochote cha kuifanya iwe capital ya tz, hata airport hakuna.

Tujikombowe kutoka makucha ya wakoloni na turejeeni katika asili yetu ya Dola ya zanzibar

Ahsanteni

EAFR1886.gif
 
we may call it so,

but, maybe, it is the thoughts of those who know the truth of Tanganyika & Zanzibar's true history and reality of their possible future.
 
Fikira mbadala na yenye mshiko wa kihistoria! Usilopenda kulitaja ni kwa jinsi ya wapogoro na wazaramo walivyopigana kishujaa kukataa utawala huo wa kipwani, na hapa sijazungumzia mashujaa kama wale wa kule Iringa, Unyanyembe, Usukumani na Uchagani na hata hapo karibu na Zanzibar kwa Wazigua/Usambarani!

Kama ni dola ndiye kitambulizi cha utaifa basi pengine tungekwenda ndani ya historia tuangalie ni dola gani ilikuwa kubwa zaidi kabla ya ukoloni ndio tuibebeshe utaifa wetu, taifa moja, serikali mmoja.
 
Mh! Mbona umeleta jipya

Anatukumbusha machungu ya Biashara ya Utumwa huyu! Huoni huo mshale unaoonyesha to Saudi Arabia and the Americas?

Kwa maana hiyo kwa ramani hii tunatakiwa turudi Germany East Africa tuwe na warundi na wanyarwanda?
 
Laahaula! Tunasema hivi muungano hatuutaki. Unbelievable ,sijui baadhi ya watu viziwi au basi jeuri tu.
 
Kikombe1,

sina la kukujibu zaidi ya hili,

inategemea sana na vitabu ulivosoma, au ulivosomeshwa mashuleni kwenu.

Lakini ukweli ni kwamba Tanganyika ilikuwa ni sehemu ya zanzibar hadi alopofika mjerumani.

Ukweli wa pili ni kwamba fukwe za tanganyika na kuingia ndani mile 10 ni sehemu waliyokodishwa wajerumani kwa muda wa miaka 99 na kwa taarifa yako nyaraka zipo. Ilikuwa ni mwaka huo wa 1886, bahati nzuri map hiyo nimekuonesheni, ilichorwa map hiyo kabla ya mkataba wa kukodishwa eneo hilo.

Tatu, siku yoyote zanzibar ikikomboka kutoka katika makucha ya tanganyika na kuwa taifa kamili na huru, fukwe za tanganyika walizokodishwa wajerumani zitadaiwa kisheria huko UN, usiifute email hii kama kumbukumbu yako.

Kumbuka Hong Kong na Macau, wazungu na wareno walibidi wazirejeshe kwa wachina baada ya muda wa kodi wa miaka 99 kumalizika.

Pia nakuomba ujuwe kwamba ndio maana Malimu Nyerere akauhamisha mji mkuu kutoka Dar hadi Dodoma, akijuwa wazi kwamba ipo siku Zanzibar itakomboka na itaidai sehemu yake na hakuna budi ila kutolewa tu.

ahsante
 
Simplemind,

Waswahili tuna misemo mizuri sana, mojani huu

MKKANGE SAMAKI KWA MAFUTA YAKE

nadhani tumefahamiana
 
Mcheza karate,

Hili si jipya, huu ni ukweli uliosahaulika, au ni ukweli uliofichwa katika kijivuli cha uhuru kwa miaka nenda miaka rudi.

Historia huwa haibadiliki wala haifutiki, wachia mbali wanasiasa wanavoweza kupaka matope wasichokiona ni sehemu ya maslahi yao.

Biashara ya utumwa ilikuwa ni biashara ya wazungu, soko kuu katika east afrika lilikuwa zanzibar town. kama vile leo mafuta ni biashara ya waarabu lakini soko kuu liko London na New York,

lakini siasa za kukandamiza watu wenye asili na kabila fulani ndio liloleta kusema waarabu walikuwa wanauza watu huko east afrika.

Kwa mujibu wa ramani hii tunatakiwa turudi pale pale tulipafikia kabla kuja wajerumani...dola ya Zanzibar, yaani mmasai alieko juu kule aseme na kujijuwa na kujiamini kwama yeye ni mzanzibari, walioko kigoma waseme sisi ni wanzibari na walioko mtwara waseme sisi ni wazanzibari kama watakavosema walioko pemba

ahsante
 
Rayan,

Kwani ndio kweli hawaujui ukweli huu, wanajipumbaza tu
 
sina uhakika kwanza kama raman yenyewe ndio hiyo
 
Wananchi Wezangu,

Nami leo ninapenda kutowa maoni yangu, ingawaje sidhani kwamba jaji Warioba na kundi lake watayasikia maoni haya.

Kwanza ningependa kuyapa uzito maoni yangu kwa kuweka hii map ya Zanzibar ya mwaka 1886, kabla ya mile 10 za fukwe ya Tanganyika na Kenya kukodishwa kwa miaka 99 kwa wajerumani na waingereza.

Kabla ya wazungu kuifanya ramani hii, tanganyika ilikuwa ni sehemu ya Zanzibar, mjerumani ikaipora sehemu hiyo na kuifanya koloni lake.

Mimi ninaamini moyoni kwamba sisi wazanaibari na watanganyika ni wamoja kidamu na tulikuwa raia wa nchi moja, sulatanate of zanzibar,

Kwa mtazamo huo na tufanye tu nchi moja lakini iitwe zanzibar na capital city yake iwe znz town, na musiseme znz town ni mji mdogo kuwa capital, kwani dodoma hakuna kitu chochote cha kuifanya iwe capital ya tz, hata airport hakuna.

Tujikombowe kutoka makucha ya wakoloni na turejeeni katika asili yetu ya Dola ya zanzibar

Ahsanteni

EAFR1886.gif

na Baba yenu wa Taifa awe John Okelo.
 
kumbe tatizo letu ni majina tu (yaani Tanganyika, Zanzbar na Tanzania) na sio yaliyomo ndani ya muungano? Hii ni concept mpya sasa nadhani!
 
John Okelo alikuwa Mganda,

Usihau kwamba Uganda ilikuwa ni sehemu katika maeneo ya Zenj Empire, utawala wa Kizanzibari shupavu uliokuwa ukiongozwa direct from Zanzibar Town.
 
Kinachonifurahisha ni kuwa baada ya Wazenji kuona kuwa hata Tanganyika wamechoka kwa Ulalamishi na Ukupe wao wanaanza kuja na vingine. Nyie si mlitaka Serikali yenu yenye Madaraka na katiba ya Zanzibar yasema hivyo ikitaja eneo lenu basi anzeni. Sisi Bara hatutaki Muungano (According to Warioba kuwa watu wengi wa bara walisema hawataki Muungano huo)
 
Tatizo kubwa kuna watu wameiwekea majani historia kwa makusudi ili kuwadanganya watanzania wa leo. Wao wanaujuwa ukweli juu chini

ndio maana nikapendekeza kuwe na dola moja lakini iitwe Dola ya zanzibar kwasababu ndani ya vitabu vya historia ya ukweli tanganyika ilikuwa ni sehemu ya znz, na tukitaka zaidi hata mji wa dar es Salaam, umejengwa kwanza na kiongozi wa dola ya zanzibar, si mjerumani wala muengereza bali ni sultan wa znz, ambae alikuwa pia ndie sultan wa tanganyika kwa wakati ule.
 
Bin Faza,

Ngoja nikusome huku nakunywa zangu gahawa na faluda.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom