Highlander
JF-Expert Member
- Feb 12, 2012
- 3,093
- 1,075
Highlander
Ahsante sana kwa nasaha na kauli zako njema. Nakushukuru sana kwa kutoa ahadi hiyo ya kuweza kunipa kiwanja cha kujenga msikiti mbeya. Na nakuahidi kwamba nitaitikia wito wako, muda ukifikia nitawasiliana na wewe.
Ninahakika kwamba wewe ni mkiristo mwema na msomaji mzuri wa bibilia kwahivo unajuwa wazi kwamba uislamu ni dini ya mitume wote waliomo ndani ya bibilia akiwemo Yesu mwenyewe. Pia ninajuwa unajuwa kwamba Mtume wetu Muhammad SAW katajwa kwa jina katika Songs of solomon 5:16 hebu funguwa ikiwa hukuliona jina Muhammad nitakuonesha.
Dini ni chaguo la mtu na hakuna mtu nayewekea gunduki kulazimishwa kutembea uchi au kuvaa kiheshima au kukatazwa kuingia msikitini au kanisani. Ni chaguo binafsi.
Labda kinachowatisha wazanzibari zaidi ni kuona idadi ya makanisa yanayojengwa huko hayana proportional balance na idadi ya wakiristo walioko zanzibar.
Ahsante
Ni kweli mimi ni mkristo ingawa sijaenda kanisani kwa muda sasa. Utakapokuwa tayari kutaka kiwanja cha Msikiti Mbeya nipe PM humu ujue sitanii. Uislamu umejengwa juu ya msingi wa dini ya Kiyahudi ya Judaism ndiyo maana mitume wote waliopo katika Biblia wanapokelewa na dini ya Kiislamu. Waislamu wanafuata torati ya musa kwa sababu hiyo; wanavaa bargashia kwa sababu hiyo, wanavaa kanzu kwa sababu hiyo, hakuna kuvaa viatu msikitini kwa sababu hiyo. Wakristo wanawakubali mitume wote hao ambao waislamu wanawakubali. Tunaunganishwa na torati ya Musa. Waislamu wanapokea mafundisho mengi ya Kristo, ingawa si yote. Kwa hiyo tunaunganishwa pia na hayo machache katika Kristo ambayo Waislam wanayapokea. Tatizo ni kwamba Wakristo wanamkataa Mtume Muhammad (SAW). Mgogoro wetu upo hapo. Lakini mimi sipendi kuuita mgogoro kwa sababu kila mtu anatakiwa kuwa huru kuamini anavyotaka.
Tukiwapa watu wetu uhuru wa imani, tukawapa wahubiri wa pande zote uhuru wa kuuza mawazo pasipo kubeza, kutukana, kudharau mitazamo ya watu wengine nchi yetu haina tatizo. Tazama upumbavu wa kupita kwenye majumba ya ibada kubeza dini za watu wengine linakotupeleka!