Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Dean
Huwezi kuwa na uhakika kwasababu wanaohusika kukueleza wewe ukweli wamekudanganya ili kupata maslahi yao binafsi ya kukutawalaeni kama wanyama pori tu
Angalia na hizi sasa, kumbuka tu ramani za duni azilichorwa na wazungu na sio sisi
![]()
Wananchi Wezangu,
Nami leo ninapenda kutowa maoni yangu, ingawaje sidhani kwamba jaji Warioba na kundi lake watayasikia maoni haya.
Kwanza ningependa kuyapa uzito maoni yangu kwa kuweka hii map ya Zanzibar ya mwaka 1886, kabla ya mile 10 za fukwe ya Tanganyika na Kenya kukodishwa kwa miaka 99 kwa wajerumani na waingereza.
Kabla ya wazungu kuifanya ramani hii, tanganyika ilikuwa ni sehemu ya Zanzibar, mjerumani ikaipora sehemu hiyo na kuifanya koloni lake.
Mimi ninaamini moyoni kwamba sisi wazanaibari na watanganyika ni wamoja kidamu na tulikuwa raia wa nchi moja, sulatanate of zanzibar,
Kwa mtazamo huo na tufanye tu nchi moja lakini iitwe zanzibar na capital city yake iwe znz town, na musiseme znz town ni mji mdogo kuwa capital, kwani dodoma hakuna kitu chochote cha kuifanya iwe capital ya tz, hata airport hakuna.
Tujikombowe kutoka makucha ya wakoloni na turejeeni katika asili yetu ya Dola ya zanzibar
Ahsanteni
![]()
Gefu
Ni nani alomtuma Mwalimu Nyerere afanye Muunganio na zanzibar?
Ni nani alomtuma Mwalimu Nyerere Alifute taifa la Tangayika kwa kutumia kichaka cha Muungano?
Kwanini Watanganyika mundaendelea kukubali Nchi yenu kuwa behind the scene?
Ikiwa mulikubali kuungana na zanzibar kwa sababu zozote zile shauri lenu ......sasa kila kitu kigaiwe sawa sawa ....mafuta yenu, dhahabu na almasi yenu, copper na gas, na mapato ya TRA na Central Bank yenu, ndio mara nyengine mutashika adabu yenu na kujuwa munataka nini na nini ndio muhimu kwa Mtanganyika wa kwaida.
Ikiwa hamuwezi wachieni ngazi, zanzibar haina haja ya muungano na tanganyika
ahsante
Highlander,
katika kujibu swala ujuwe kuna nafasi ya muulizaji na kuna nafasi muulizwa, swala linajibika kwa mujibu lilivoulizwa, ikiwa mtu anaanza kufanya kejeli na kafsha fulani inabidi tufanye ile kazi....SAMAKI MKAANGE KWA MAFUTA YAKE