Serikali iweke uzio katika Shule ya Msingi Minga (Singida), kuna Watu wanawafanyia ukatili Watoto

Mliogwa

Member
Joined
Jun 6, 2024
Posts
37
Reaction score
37
Suala la Watoto wadogo kukumbana na changamoto mbalimbali za kikatili kwenye taasisi za elimu limekuwa ni jambo ambalo linajitokeza mara kwa mara sehemu tofauti.

Wadau wa sekta tofauti nao wamekuwa wakipiga kelele juu ta matukio ya aina hiyo kwa kuwa yamechangia pia kuharibu ndoto za Watoto na wakati mwingine kuwaharibia mwelekeo wa Maisha yao pamoja na afya za Watoto husika.

Kutokana na matukio mengi ya ukatili kujitokeza ngazi ya shule, moja ya sehemu ya ulinzi ni kuwa Jamii kushauriwa kuweka mazingira ya ulinzi kwa Watoto ambao asilimia kubwa hawana uelewa wa jinsi ya kujilinda.

Shule ya Msingi Minga iliyopo Kata ya Minga, Manispaa ya Singida Mkoani Singida imekuwa ikitajwa kuwa na matukio kadha wa kadha kuhusu Watoto kufanyiwa ukatili.

Baadhi ya matukio hayo ya ukatili wa kijinsia ni ulawiti ambao umekuwa ukifanywa na wahalifu wanaokuwa maeneo hayo kwa kuwavizia Wanafunzi wa shule hiyo.

Nimefika eneo hilo mara kadhaa baada ya kusikia juu ya taarifa hizo na mazingira ya shule hayaridhishi, kwanza hakuna uzio hali ambayo imekuwa ikichangia au kusababisha Watoto kukosa uangalizi maalum.

Uzio uliopo ni ule wa miti ya Minyaa hauwazuii wao kutoka au hauzuii wahalifu kufika maeneo hayo kwa urahisi.

Uchunguzi wangu umeonesha kuwa wahalifu wengi huwasubiri Watoto hao barabarani kisha wale Wanafunzi waliozoea kufanya michezo michafu nao wanapewa ishara wanapita kwenye matobo ya minyaa hiyo ya uzio na kuwafuata Watu wanaoharibu.

Nasema hivyo kwa kuwa imefikia hatua baadhi ya Watoto nao wanashiriki katika michezo hiyo michafu kwa ridhaa yao wenyewe huku Wazazi na Walimu wakiwa hawana taarifa.

Sisi Wadau tunaoona kinachoendelea tunaomba Serikali iweke uzio shuleni hapo ili Watoto wawe wanapita mlango mmoja tu kuingia na kutoka ili iwe rahisi kuthibiti hali hiyo na pia wanaoshiriki kuwaharibu Wanafunzi wanahitaji kutafutwa na kuchukuliwa hatua haraka.
 
Unaonaje wazazi wakijipanga wenyewe wafanye hiyo kazi ili kulinda usalama wa watoto wao........watanzania wamezoea kufanyiwa kila kitu kwanini?
 
Kwanini jitu zima lifanye huu ushenzi Kwa watoto wa wenzao
Serikali ifanyie kazi hii taarifa, iwakamate hao wahuni, wanyongwe hadharani
 
Back
Top Bottom