Serikali iwekeze katika sekta ya kilimo na hasa Kilimo cha umwagiliaji

tramadol

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2015
Posts
5,383
Reaction score
4,323
Kilimo ndiyo sekta muhimu sana katika uchumi wa Tanzania na asilimia zaidi ya 75 wanajishughulisha na kilimo.

Muda wote tunategemea mvua za msimu katika kilimo chetu na mvua zenyewe zimekuwa zinabadilika badilika sana kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa duniani yaani climate change.

Serikali ingewekeza sana katika sekta hii ya kilimo hasa kilimo cha umwagiliaji kwa kujenga miundombinu yake imesaidia sana kufanya kilimo cha uhakika kuliko kilimo hiki cha kutegemea mvua za msimu.

Nchi ya Tanzania imebarikiwa sana kuwa vyanzo vya maji vya kutosha kila sehemu hivyo maji si tatizo kabisa.

Ardhi ya Tanzania kila kitu ikakubali ukilima kwahiyo sekta hii ingesaidia sana kuwainua watanzania kiuchumi kwa kuuza ndani na nje ya nchi mazao mbalimbali yenye ubora unaofaa kitaifa na kimataifa.

Nchi kama Japani wameweza kujenga miundombinu ya umwagiliaji katika ardhi kidogo waliyokuwa nayo na wanaitumia vizuri sana kuilisha Japani na hata kuuza nje na pia kutoa misaada ktk majanga ya kiasili yakitokea.

Waziri mwenye dhamana na sekta ya kilimo angalia jinsi ya kuboresha kilimo cha umwagiliaji,pembejeo bora, wataalamu kutumika ipasavyo wa SUA, masoko bora ya mazao nk.
 
Waziri mwenye dhamana na sekta ya kilimo angalia jinsi ya kuboresha kilimo cha umwagiliaji,pembejeo bora, wataalamu kutumika ipasavyo
kama unazungumzia Kilimo cha Tanzania, waziri mwenye dhamana Ya Kilimo hana dhamana Ya umwagiliaji.. bado una swali?
 
Waziri wa kilimo + waziri wa maji=.....?
 
kama unazungumzia Kilimo cha Tanzania, waziri mwenye dhamana Ya Kilimo hana dhamana Ya umwagiliaji.. bado una swali?
Elewa mada ndugu yangu mwenye dhamana ya kilimo Tanzania ni Waziri wa kilimo na kilimo cha umwagiliaji ni moja ya taratibu za kilimo hivyo dhamana hiyo anayo waziri wa kilimo.

Unapotoa maelezo ambayo hayaeleweki ni vizuri ukaacha tu. Matatizo ya shule za kukariri. Akili yako inakutuma kwa vile kuna wizara ya maji na umwagiliaji basi dhamani hiyo anayo waziri wa maj na umwagiliaji.

Mimi naongelea kilimo cha umwagiliaji elewa hilo ndugu.
 
Waziri wa kilimo + waziri wa maji=.....?
Hayo sasa mawaziri wahusika watashirikiana lakini kilimo cha umwagiliaji mwenye dhamana ni Waziri wa kilimo
 
Epuka kusema MAJI SI TATIZO wakati huna takwimu. Kama siyo tatizo nini chanzo cha mauaji ya baina ya wafugaji na wakulima wa morogoro.

Hayo maji siyo tatizo ilhali mito inakauka na wananchi tunaongezeka kwa kasi.

Chanzo cha hayo maji ni mvua. Unaposema mvua hazitabiriki je hayo maji yanatabirika?

Kilimo cha umwagiliaji kinawezekana baadhi tu ya maeneo kama kutajengwa mabwawa ya kuhifadhi maji.
 
Unapotoa maelezo ambayo hayaeleweki ni vizuri ukaacha tu.
Dogo, pole sana, unapingana mpaka na anayekusaidia?. hivi unajua Wizara /waziri anatekelezaje majukumu yake?, hivi unajua kazi Ya bajeti, fungu, kasma? unajua sera Ya maji?, unajua waziri mwenye dhamana ya matumizi Ya maji hata kama yametokana na kisima ulichochimba mwenyewe?, unajua ni waziri gani mwenye fungu/bajeti ya umwagiliaji!?

poor you..
 
Tofautisha dhana mbili hapo.Kilimo cha umwagiliaji na Umwagiliaji
 
Tofautisha dhana mbili hapo.Kilimo cha umwagiliaji na Umwagiliaji
unajiandikia tu bila kuwaza negative implications za Jambo unalowaza kusimamiwa na Wizara mbili, unamkimbia tu kama nyumbu
 
Wazo zuri sana, liko open Kila mtu anajua kwamba hili ndilo la msingi kwa uchumi wa nchi yetu kupita yote. Chakula ndo msingi wa kwanza wa ustawi wa Jamii ya viumbe vyote, nyani hawana nguo lakini furaha yao ni kuwa na uhakika wa kula tu. Ktk basic needs za mwanadamu chakula ni ya kwa kwanza, lakini ni bidhaa yenye uhakika wa soko. Viwanda vitakuja ktk kukibororesha na kuongezea tu thamani, cha msingi tu kwanza kiwepo, kiwepo cha kutosha surplus ndo itaingia viwandani. Ni ujinga kuwaza kwamba mkulima atauza debe mbili zake zikawe mali ghafi ktk kiwanda cha usindikaji ili aje anunue unga toka kiwandani.
 
Mito yenyewe sasa hivi inakauka!
Ni kiasi gani cha maji hutiririka tu bure kipindi cha masika? Dams zijengwe. Kila kijiji wawe nayo hata matano kama hawana mito ya uhakika.
 
Nimeiona hiyo mashine pale Iringa Kisolanza Farm jana on my way mbeya jamaa yuko vizuri nikajiambia same worlds hiki ndio kilimo tunapaswa kukiendea
 
Tanzania hatuna viongozi bali tuna watawala......

Viongozi Daima huwaonyesha njia wanaowaongoza......

Kiongozi anakuwa mbunifu katika kutatua kero na changamoto za jamii au sehemu anayoiongoza....

Kiongozi anapokea ushauri na maoni ya wale anaowaongoza katika kufikia Safari ya mafanikio ya jamii anayoiongoza

Kiongozi anatambua kuwa yupo hapo alipo kwa kuwatumikia anaowaongoza na sio kutumikiwa na anaowaongoza

Changamoto za kwenye kilimo na sekta nyingine zingeshashughulikiwa kama tungekuwa na VIONGOZI na sio WATAWALA

MTAWALA ANAWAZA JINSI YA KUENDELEA KUTAWALA

NA KIONGOZI ANAWAZA JINSI YA KUTAFUTA UFUMBUZI WA CHANGAMOTO ZA WALIOMCHAGUA......
 
Kilimo cha umwagiliaji kinawezekana baadhi tu ya maeneo kama kutajengwa mabwawa ya kuhifadhi maji.
Sijakubaliana na wewe unaposema maji tatizo nchini ila nimekipenda hicho kipande nilicho-qoute.
Ingawa ni ukweli kwamba wakulima wengi wanategemea convenient sources of water ambazo zitawapa urahisi wa kufanya shughuli za kilimo bila gharama za ziada. Na vyanzo hivi ni mito ambayo kama ulivyosema inategemea mvua hivyo kama hakuna mvua hakuna mito.
Potential and reliable sources of water nchini ni nyingi sana. Nafikiri Tanzania ni miongoni mwa nchi chache zinazoongoza kuwa na vyanzo vingi vya maji baridi. Tuna maziwa makuu matatu: Tanganyika, Nyasa na Victoria (kama wale jamaa wa jangwani wasipoleta figusu).
Ukiachana na nayo ingawa sina taarifa sahihi lakini nafikiri tuna moja kati ya aquifer kubwa sana zilizohifadhi maji ardhini. Nasema hivyo sababu almost everywhere Tanzania unaweza chimba na kukuta maji ingawa sehemu nyingine yanaweza yasifae kwa umwagiliaji kutokana na excess amount of salt contents.
Mfano hai. Katika jimbo la Nebraska, USA kila siku galoni bilioni 7.3 ambayo ni 94% ya maji yanayotoka ardhini yanatumika kumwagilia ekari milioni 8.5
Kwa kuhitimisha ni kwamba tuna vyanzo mbadala vingi vya maji isipokuwa kunahitajika uwekezaji mkubwa. Ni kama vile serikali au sekta binafsi itumie mabilioni kuvuta maji toka maziwa makuu hadi sehemu husika. Ndio, inawezekana kama ambavyo imewezekana kuvuta maji toka ziwa Victoria hadi shinyanga, tabora na maeneo ya jirani. Nina hakika hilo likifanyika its impact on agricultural sector will be astonishing.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…