Serikali izuie mfumo wa Pre Form 1 hadi Novemba. Watoto wapate muda wa kupumzika baada ya safari ndefu ya elimu ya msingi

Ndio maana serikali ikaweka ratiba za mihula kwa mwaka mzima. Kazi ya serikali ni kusimamia utoaji wa elimu nchini.

Unaamini kwenye uhuru wako ndio, ila serikali lazima iweke mifumo na kila mtu aifuate. Kama unakumbuka kina nyakati shule zilikuwa zinafungwa na kufunguliwa hovyo tu, walau sasa hivi kuna uniformity kwenye ratiba za mwaka kwa shule za binafsi na za serikali.

Namuunga mkono mleta mada kwa asilimia zote. Watoto wanakuwa watumwa badala ya kuifurahia elimu yao.
 
wakimaliza mtihani wenye maamuzi na watoto ni wazazi
 
Kama mtoto wako ana uwezo mdogo darasani kubaliana na hali, unamchanganya zaidi akiunganisha bila mapumziko.
Ila msimamo ni ule ule
Unaweza kumpumzisha mwanao asiende pre form one mpaka mwakani atakapojiunga form one.

Acha wengine wanaotaka waende.
 
Pre form one ni muhimu kwa wanafunzi waliomaliza shule za serikali.

Wale wa english medium hakuna umuhimu wowote wa kusoma pre form one.
 
Wewe ndio wale wazazi wanaodhani mtoto ni shule tu, unamuamsha mtoto saa kumi kwenda shule, likizo hapumziki ni matuisheni, kupeleka watoto wadogo boarding, n.k.

Elimu ni muhimu lakini sio kila muda ni kusoma tu,
Kila mzazi ana namna yake ya kumlea mtoto wake kwa uhuru kama ikiwa tu havunji sheria za nchi.
 
Wazo zuri,
hivi una amini kuna serikali?.
Samahani lakini
 

Umetambua tunachokikataa ni optional? Kwani kuna lazima ya kwenda tution?

Tofautisha hilo na mihula rasmi iliyopo ambayo si optional na haiwezi kukaidiwa.

Kwamba muhula unaanza Jan 1 hilo huwezi kukataa. Ila kuwa kipindi cha likizo gapo ni utawala binafsi m, na bado mnataka mnyapara nyuma yenu kuwamulia la kufanya? Loo! Si mpange kuhamia jela?
 
hilo mpaka serikali iseme ama ni mzazi mwenyewe
 
Siyo lazima wala hamna anaye force upeleke mtoto
 
Pre form one ni utapeli uliohalalishwa. Mtoto anakaa mwezi tu lakin analipa kuanzia laki 4 kuendelea Hivi hiyo shule hata akija kwenda January si ataizoea tu?

Na ni lazima pia,
 
Sahihi mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…