Serikali izuie mfumo wa Pre Form 1 hadi Novemba. Watoto wapate muda wa kupumzika baada ya safari ndefu ya elimu ya msingi

Mkuu kwani ukiacha kumpeleka mwanao, si fresh tu? Au vp ndugu mkata switch?
Anakusaidia hata wewe ambaye hujitambui, ukimuona kipofu anaelekea kutumbukia shimoni ni wajibu wa kiraia kumwambia mbele kuna shimo. Sijui umenielewaaa?
 
Mm niliwahi kusoma pre form one, Ila Kwa kweli binafsi naona haina umuhimu wowote kwenye elimu ya mtoto, n bora atulie nyumbani asubiri kuanza form one rasmi.
 
Mm niliwahi kusoma pre form one, Ila Kwa kweli binafsi naona haina umuhimu wowote kwenye elimu ya mtoto, n bora atulie nyumbani asubiri kuanza form one rasmi.
Na mimi niliwahi kusoma,

Walimu wanafosi sana kufundisha vitu vingi ndani ya miezi michache, niliambulia vitu vichache sana
 
Sema hii siku hizi imegeuzwa dili
Zamani mimi nilisoma Jitegemee miaka ya 90, tulianza mwezi kabla shule haijafunguliwa na ilikuwa bure...
Lakini tukaja kugundua kumbe tulianzishwa ili tujenge madarasa na kufanya gwaride kwa sana, hakuna kusoma....
Lakini ilikuwa poa sana kwa kijana wa kiume.....
 
Huwa inaitwa orientetion na hata vyuoni ipo, wanafunzi wa mwaka wa kwanza wanakuja wiki moja kabla ya chuo kufunguliwa wazoee kidogo mazingira,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…