Serikali: January 27,28 watumishi wafanyie kazi nyumbani

Serikali: January 27,28 watumishi wafanyie kazi nyumbani

PureView zeiss

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2016
Posts
10,786
Reaction score
35,916
Kufuatia Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati utakaofanyika Januari 27 na 28 hapa nchini, Serikali imeelekeza watumishi wa umma katika Mkoa wa Dar es Salaam wafanyie kazi nyumbani isipokuwa watumishi ambao mazingira ya kazi yanawataka kuwepo katika vituo vya kazi.

Watumishi hao ni kama vile vyombo vya ulinzi na usalama, sekta ya afya na sekta ya usafiri na usafirishaji. Vilevile benki, hoteli na migahawa hazitafungwa, pia biashara katika soko la Kariakoo zitaendelea kufanyika.

Aidha, taarifa hiyo iliyotolewa na Ofisi ya Rais Ikulu kupitia Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka imesema waajiri katika Sekta binafsi wanashauriwa kuruhusu watumishi wao katika Mkoa wa Dar es Salaam kufanyia kazi zao nyumbani au kuweka utaratibu ambao hautasababisha changamoto ya usafiri kutokana na kufungwa kwa baadhi ya barabara muhimu.
20250126_161721.jpg
 
Tangu wakati wa ugonjwa mbaya sana wa mlipuko wa COVID nchi nyingi Duniani wafanyakazi wake wanafanyia kazi majumbani hadi leo.
Wameona faida nyingi kwa upande wa waajiri na wafanyakazi kufanyia kazi majumbani kuliko ofisini .
Wameweka roster mzunguuko wa zamu wa wafanyakazi wachache kuwa wanaenda ofisini labda 10% tu.
Na kumekuwa na commitment za hali ya juu ktk kufanyia kazi nyumbani na kutoa taarifa ya kazi kwa wakati.
Na mwajiri amekuwa akifanya regular performance measurements na kuona kuongezeka kwa tija ya utendaji ukilinganisha na ilivyokuwa ofisini 100%
 
Taarifa ya utafiti wa kisayansi wa hivi karibuni imeonesha kuwa kufanyika kazi majumbani (working from home) kumekuwa na manufaa makubwa kiafya kwa wafanyakazi sababu wanaweza kula na kunywa vyakula vyenye lishe na wavipendavyo na kuviandaa vyema kiafya na ustawi wa familia na jamii,

Tulifikirie tulifanyie kazi , tubadili namna zetu za kufikiri , tuache kuwa conservatives na waoga wa kuthubutu mambo mapya na kuamua kwa usahihi.
 
Kufuatia Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati utakaofanyika Januari 27 na 28 hapa nchini, Serikali imeelekeza watumishi wa umma katika Mkoa wa Dar es Salaam wafanyie kazi nyumbani isipokuwa watumishi ambao mazingira ya kazi yanawataka kuwepo katika vituo vya kazi.

Watumishi hao ni kama vile vyombo vya ulinzi na usalama, sekta ya afya na sekta ya usafiri na usafirishaji. Vilevile benki, hoteli na migahawa hazitafungwa, pia biashara katika soko la Kariakoo zitaendelea kufanyika.

Aidha, taarifa hiyo iliyotolewa na Ofisi ya Rais Ikulu kupitia Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka imesema waajiri katika Sekta binafsi wanashauriwa kuruhusu watumishi wao katika Mkoa wa Dar es Salaam kufanyia kazi zao nyumbani au kuweka utaratibu ambao hautasababisha changamoto ya usafiri kutokana na kufungwa kwa baadhi ya barabara muhimu.View attachment 3214810
Mi baada ya J5 basi alhamis nitaumwa nitatibiwa ijumaa, tuonane j3
 
Wafanyie kazi kutoka nyumbani kwa mitandao gani?

Kuna matayarisho yoyote yamefanywa? Mifumo iko digitized? Kuna VPNs za kuhakiki usalama? Wafanyakazi wamepewa mafunzo na vifaa vya kufanyia kazi kutoka nyumbani?

Sipingi wazo, wazo ni zuri. Mimi nimefanya kazi nyumbani kwa zaidi ya miaka 10 (US), najua uzuri na ubaya wale. Lakini hiki si kitu cha kukurupuka, kinahitaji maandalizi.

Serikali imefanya maandalizi hayo?

Kwa nini serikali imesubiri mpaka wamekuja wageni ndiyo imeruhusu hili jambo, wakati tushajifunza wakati wa COVID kuwa kulikuwa na haja kubwa ya kujiandaa kwenye hili?
 
Ni kweli limiting factors kubwa kwa mazingira ya Bongo ni upatikanaji wa mtandao majumbani kama hizi VPN n.k na vitendea kazi kama vile laptops , simu desktops n.k
Inabidi waanze kulifikiria hilo iwapo ikitokea kuhitajika wafanyakazi kufanyakazi majumbani.
 
Back
Top Bottom