Ukana Shilungo
JF-Expert Member
- Apr 17, 2012
- 3,041
- 2,422
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nina ekari sita za miti niliyopanda mwenyewe miaka 8 iliopita,lakini sehemu tofauti na huko.Mh mkuu wa Kaya,why not you!
Hivi miradi mikubwa naya kimkakati ni ipi na huo umkakati wake ni upi?Subiri miradi mikubwa ya kimkakati ikamilike. Vinginevyo tuone uwezekano baada ya 2025
Ya kitu gani?Weka picha
Hayo maji mkuu si ndiyo yanaenda kulisha bwawa la Mtera? Au unataka likauke?Mpango Kama huo ,inawezekana zaismdi njia ya kwenda Mvumi kupitia Ntyuka ,Kuna vilima na mspromoko mengi yanayopitisha maji kutoka maeneo ya Mtera ,Mlowa kwa ujumla Iringa Road .
Dogo weka namba za simu kabisa mbona Lesilie Mbunda "Chakubanga" pamoja na mashudu anayotoa hapa huwa anaweka namba za simu kabisa? Wewe umetoa point sana mkuu!Kupitia Jukwaa Tukufu,
Nawasilisha ushauri na maoni yangu kupendekeza kwa serikali ya Jamhuri wa Tanzania kujenga bwawa/lambo kubwa linalotokana na uvunaji wa maji ya mvua (rainfall water catchment dam).
katika eneo lolote litakalobainishwa na wataalamu kati ya wilaya za Kongwa, Chamwino na Mpwawa ambako kuna utambarare unaozungukwa na vijilima na makorongo hatarishi pindi mvua inyeshapo.
Bwawa pendekezwa ligawanywe mara mbili kwa matumizi tofauti
1. Sehemu ya kwanza ya lambo hilo itahudumia Kilimo cha mboga mboga, zabibu, alizeti, karanga, korosho na ufugaji wa kisasa wa mifugo ya ng'ombe. mbuzi na kuku (matumizi bora ya maji kwa njia ya dripu yataelekezwa vizuri na watalaamu)
2. Sehemu ya pili itahudumia wananchi kwa ajili ya mapumziko, kuogelea na uvuvi mdogo wa ndoana (maji haya yatatengenezewa mfumo wa kutembea kupitia vyumba maalum ambavyo vitayafanya kujirejesha kwa usafi kama ilivyo kwenye mabwawa ya maji machafu
3. Eneo hilo la bwawa ambalo halitahitaji kuchimba chini ardhini badala yake eneo lenye uwezo wa kupokea maji kutoka pande zote kisha matuta makubwa yenye upana wa kupita gari juu yatajengwa kwa kuzingatia taratibu za ujenzi na uimara wa udongo.
4. Eneo hilo la bwawa linatakiwa kupandwa miti isiyotumia kiwango kikubwa cha maji na rafiki wa utunzaji mazingira.
5. Eneo la bwawa linatakiwa angalau liwe na ukubwa wa kilomita za mraba kati ya (20*25) sawa na 500 Km2 au (20*30) sawa na 600 Km2.
6. Mibuyu yote iliyotamalaki maeneo ya Chamwino, Kongwa na Mpwawa isikatwe ila itunzwe na tunda na magome yatumike kwa matumizi ya binadamu ya asili na ya viwandani kama utengezaji wa sabuni ya mbuyu, nk
Endapo serikali itaridhia na kuweka ksenye mpango iwa utekelezaji manufaa yatakayopatikana itakuwa ni kumbukumbu isiyofutika vizazi na vizazi kwa kuchochea utayari wa kila mtu kuishi na kuwekeza Dodoma maana palipo na maji kwa matumizi ya kibinadamu, mimea, shughuli za kiuchumi na kijamii migogoro hupungua.
Nawasilisha kwa mjadala kutoka kwenye tanuru la fikira chanya.
Chato kwanza, hayo mengine mtajiju wenyewe.Je Dodoma ikigeuka Jangwa patakalika kweli na hili ongezeko la watu?
Kikubwa ameandika inabaki kama kumbukumbu.. Hata alieandika na kushauri kuhusu Stiegler's Gorge huenda hakutegemea kuwa 2020 bwawa lingejengwaWazo zuri, nasikitika litabaki humu jamii forum kwa ajil ya kusomwa tu.
This was supposed to be my question. Thanks for asking earlier 👍🏽Unaota ndoto mchana kwani hapo ni Chatto?
Mkuu,Hongera kwa wazo zuri.
Kulikuwa na mpango wa kuleta maji kwa bomba za DI Ductile Iron za ukubwa wa 600mm kutoka Mwanza, sijui mpango uliishia wapi.
Kwa wazo la bwawa la ukubwa huo japo hujatoa kina
20 km x 30km = 600 square kilometer ni kubwa sana.
Maana hata kama kina ni 3 meters hii ina maana kuwa
20000m x 30000m x 3m = 180,000,000 cubic mtrs.
Hata kama kuna water catchment nzuri bado huwezi kuvuna maji mengi kiasi hicho.
Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Sijasikia mkuu wa kaya akiimiza upandaji wa miti kwa wingi katika mikoa ya kati Tanzania, Wala sijasikia mkuu wa kaya akiwezesha matumizi ya nishati mbadala badala ya kukata kuni.