Serikali kama imeshindwa kutengeneza ajira kwa vijana, ijiandae kujenga magereza mengi

Mingendeu

Senior Member
Joined
Aug 26, 2019
Posts
115
Reaction score
237
Unakuta kijana ana miaka 30+, ametumia miaka 28 au zaidi shuleni hadi kuhitimu shahada yake ya udaktari.

Anarudi nyumbani bila ajira. Hana mtaji na hana ujuzi zaidi ya alichosomea. Wazazi nao hawakuwa na ajira rasmi, walikuwa wanaungaunga tu ili mtoto wao apate elimu aje kuwaokoa. Kijana anaamka anakuta baba na mama hawana nguvu tena ya kumsapoti na yeye hana nguvu ya kuwasapoti. Kila akiwaangalia wazazi anapata stress.

Kijana huyo akienda kwenye vibarua vya kusaidia mafundi anaonekana hajui lolote hivyo watu wanamkwepa.

Akisema aende mjini kama kariakoo, kutafuta cha kufanya. Anaishia kuzurula na anakosa hata 500 ya maji. Anaishia kutamani hata kuomba maji kwa mtu.

Hawezi kuuza simu ili aanze biashara maana kwenye simu ndipo ajira zinatangazwa. Na kuna muda anapitwa na fursa kwasababu ya kukosa bando.

Siku akipata elfu 1 yake anunue kifurushi, anakutana na kelele za motivational speaker wakimwambia kuwa kukaa kutegemea ajira ni uzembe. Utakufa masikini.
Anazidi kuchanganyikiwa.

Kijana huyu alikuwa na girlfriend wake, lakini ameachwa kwasababu future yake haionekani. Kijana huyu anahisia na mwili wake pia kuna muda unahitaji tendo la ndoa. Pesa ya kununua dada poa haipo, pesa ya kumpeleka mdada lodge haipo.Anaishia kujichua.

Akiangalia waliofeli darasa la saba, wapo mtaani na viduku na vidread kichwani wanaendesha bodaboda zao kwa furaha na kutamba elimu sio kitu.

Ndugu yangu; Ukipata nafasi ya kumshika kijana mmoja mkono na kumuinua juu, usisite. Vijana tunapitia mengi. Mungu atakulipa.

Kuna vijana wengi wasomi ila watoto wao hawatakwenda shule. Hawaamini tena kwenye elimu, kwa uelekeo wa vijana wasomi wanavyoongezeka na kuaminishwa kwenye kazi za ujanja ujanja taifa litaanza kujenga magereza mengi sana siku zijazo.
 
Umedescribe very clear mfumo mzima wa maisha ya kijana wa tanzania. Hizo ndio sababu za kweli zinazomuweka mbali na mafanikio kijana kutoka kaya maskini. Safari ni ndefu na ngumu sana, kila mtu abebe msalaba wake na kila mtu aokoe nafsi yake.
 
Ww ulipata ajira ukiwa na umri gani mzee uliyeandika uzi?
Na bundle unawekaga la shilingi ngapi?
Uliwezaje?
Tuanzie hapo
27 lakini naelewa misoto niliyopitia. Kuna maisha Kama hujawahi kuishi huwez kuelewa hayo maandishi. Bahati mbaya pia sijaandika hii kwaajili yangu, nimejaribu kuandika yale nnayoyaona kwenye jamii yangu
 
Umedescribe very clear mfumo mzima wa maisha ya kijana wa tanzania. Hizo ndio sababu za kweli zinazomuweka mbali na mafanikio kijana kutoka kaya maskini. Safari ni ndefu na ngumu sana, kila mtu abebe msalaba wake na kila mtu aokoe nafsi yake.
Kuzaliwa kwenye kaya masikini ni changamoto Sana. Watu wengi hawaelewi kwasababu hawajazaliwa huko
 
27 lakini naelewa misoto niliyopitia. Kuna maisha Kama hujawahi kuishi huwez kuelewa hayo maandishi
Hujapitia msoto wewe. 27 umeajiriwa leo unawaandikia watu, mimi 28 sijui hili wala lile. Mzee chwaaaaa. Alafu ndio tegemezi, matokeo ya chuo ndio yametoka ijumaa, jumanne mzee chwaa presha. Sijui mbele wala nyuma. Madogo watatu wote wako shule. Mama haelewi. Msiba umeisha kila mtu na kwake. Hajira hakunaaaaa. Pesa hakuna. Sikiliza. Shukuru kama ulipenya ukaajiriwa early hivo. Wenzako tungekua hapo mpaka leo hata ajira hatujapata. 2 years down grinding na mabarua.
Ndugu. Vijana watajikwamua tu, hamna anayeenda jela. I am ot of figures in cash now.
Watapambana whatever the situations, usiwakatishe tamaa za jera sijui.
 
Sijamkatisha mtu tamaa Ila nimejaribu kuelezea changamoto za watoto masikini na ukisoma vizuri sijajizungumzia mimi. Ni uandishi, kwenye uandishi ni nadra sana kujizungumzia mwenyewe, Mara nyingi tunaandika yanayotuzunguka.
 
Nimeona uandishi wako wa kumuongelea yule si wewe mwenyewe ndio maana nimekuuliza na nikakupa uhalisia.
We local guys don't talk that. Hata uende ulaya msoto utapata ndio utatoka. Hamna anayemaliza alafu maskini paap kapata.
Hata bongo, utakua boda utakua winga kkoo, utakua dalali. Ila ipo siku, utatoka kama ulipitia elimu, ila sio jela wala serikali kuongeza magereza BIG NO.
unemployment problem is world wide. Haswa kwa kaya maskini. Kwa africa mateso nitoka mababu na mababu.
 
Tupo Pamoja. Ila mantiki ya andiko zima ni kutoona wasio fanikiwa kuwa ni wazembe, kuna vita wanapiga nying Sana.

Nimezungumzia kuhusu jera nikimaanisha mtu anayepitia changamoto nying hivyo ni rahisi hata kupata magonjwa ya afya ya akili. Kijana kubaka, ualifu nk.

Tunapopata nafasi, tusijione washindi kwa kuwaona wengine hawathubutu. Tupigane tafu
 
Unakuta kijana ana miaka 30+, ametumia miaka 28 au zaidi shuleni hadi kuhitimu shahada yake ya udaktari.

Anarudi nyumbani bila ajira. Hana mtaji na hana ujuzi zaidi ya alichosomea. Wazazi nao hawakuwa na ajira rasmi, walikuwa wanaungaunga tu ili mtoto wao apate elimu aje kuwaokoa. Kijana anaamka anakuta baba na mama hawana nguvu tena ya kumsapoti na yeye hana nguvu ya kuwasapoti. Kila akiwaangalia wazazi anapata stress.

Kijana huyo akienda kwenye vibarua vya kusaidia mafundi anaonekana hajui lolote hivyo watu wanamkwepa.

Akisema aende mjini kama kariakoo, kutafuta cha kufanya. Anaishia kuzurula na anakosa hata 500 ya maji. Anaishia kutamani hata kuomba maji kwa mtu.

Hawezi kuuza simu ili aanze biashara maana kwenye simu ndipo ajira zinatangazwa. Na kuna muda anapitwa na fursa kwasababu ya kukosa bando.

Siku akipata elfu 1 yake anunue kifurushi, anakutana na kelele za motivational speaker wakimwambia kuwa kukaa kutegemea ajira ni uzembe. Utakufa masikini.
Anazidi kuchanganyikiwa.

Kijana huyu alikuwa na girlfriend wake, lakini ameachwa kwasababu future yake haionekani. Kijana huyu anahisia na mwili wake pia kuna muda unahitaji tendo la ndoa. Pesa ya kununua dada poa haipo, pesa ya kumpeleka mdada lodge haipo.Anaishia kujichua.

Akiangalia waliofeli darasa la saba, wapo mtaani na viduku na vidread kichwani wanaendesha bodaboda zao kwa furaha na kutamba elimu sio kitu.

Ndugu yangu; Ukipata nafasi ya kumshika kijana mmoja mkono na kumuinua juu, usisite. Vijana tunapitia mengi. Mungu atakulipa.

Kuna vijana wengi wasomi ila watoto wao hawatakwenda shule. Hawaamini tena kwenye elimu, kwa uelekeo wa vijana wasomi wanavyoongezeka na kuaminishwa kwenye kazi za ujanja ujanja taifa litaanza kujenga magereza mengi sana siku zijazo.
Ma Vijana yenyewe yamekariri maisha hapa hapa Bongo hawawezi hata kwenda kupambana Nje ya Nchi kama wa mataifa mengine Wacha wajae jela.
 
Mbona serikali inatangaza ajira nyingi sana hususan katika awamu hii au tuwe tunakutag
 
Kiukweli vijana wanapitia changamoto nyingi sana mpaka huruma.
Nikikumbuka niliyopitia mimi ndani ya miaka sita bila ajira da mwingine hawezi.
Nimefanya vitu vingi nimelima ,nimekata mkaa, nimeuza dagaa ,nimesaidia fundi, nimeuza vyuma yaani naokota mtaani naenda kuuza.,nimetembeza njegere dar kwa kichwa, nimeuza ndizi natoa mabibo nakuja kuuza mbagara nadhani kuna baadhi humu wanaweza kunifahamu.

Hasa wale wanaoishi kongowe ya kuelekea vikindu,mbagala kibondemaji huko nimeuza sana ndizi mbichi natembeza kichwani, mitaa ya kurasini mji mpya kwa tesha, kiburugwa na mitaa mingi tu hapo dar.

Ila nimechojifunza vijana tusichague kazi na wala tusikate tamaa. Ipo siku mungu atawakumbuka.
 
Back
Top Bottom