Acheni kulialia maisha hayajawahi kuwa maraisi, anzeni kunata na biti.
1.Badala ya kupoteza mamilioni ya pesa kuwasomesha watoto mashule ya English medium.Jitahidi watoto wako uwasomeshe shule zenye ada isiyofika million zipo shule nyingi tu wewe zingatia ufaulu uwe wa wastani kupanda juu.Kama unaona hata hizi laki huna mpeleke kayumba ila mfatilie na uzingatie apate mwalimu wa ziada kumboost.
2. Hakikisha mtoto wako akimaliza darasa la saba badala ya kukaa nyumbani na kula bure kulala na kuangalia sizoni, mpeleke VETA akasome fani yoyote ya mda mfupi akimaliza kama bado mda upo mpeleke akasome mambo ya CODING na computer awe fiti. Hii ni moja ya uwekezaji bora kuliko kwenda PRE-FORM ONE.
3.Msubiri tena mtotoa akimaliza form four mwendo ni ule ule asome shule za chini ya millioni au kama huna ni Kayumba tu.Akimaliza form 4 usipeleke mtoto PRE-FORM 5 unapoteza muda na pesa. Huu ni muda wa mtoto kupata ujuzi, mpeleke VETA akajifunze ufundi wowote wa muda mfupi, muda ukibaki asome na CODING na mambo ya computer tena..Huu ndo urithi na shortcut ya kujikwamua kwa watoto wa maskini na wale middle income.
4.Kama utampekeka collage💪💪💪na hapa wazazi wengi wanafeli( hapa mtoto akifika form 4 kabla ya mtihani wa taifa kuna OPTION zinatolewaga za wanafunzi wanaopenda kwenda TECHNICAL COLLEGES kujaza form,sasa kizaazaa ni kuwa wazazi hawashirikishwi na wanafunzi hawana exposure wala future ni kufata mkumbo tu na wao wanataka kwenda 5$6😄😄😄,hivi vyuo wanavyojaza huwa ni vya serikali na ada huwa ni nafuu sana. Hivyo mzazi mjanja na mwanafunzi GENIUS hapa anaangalia fursa kama hii anapita nayo,wale bendera fata mkumbo huwa wanajuta sana maana hii CHANCE ya kupata vyuo vya serikali huwa ONCE IN A LIFE TIME LABDA URISITI FORM-4) ilaKama ukiona form 5 ndo chaguo lenu akimaliza 6 mwendo ni huohuo peleka VETA akachukue ujuzi mwingine. Baada ya hapo huyu mtoto hawezi shindwa hata kujilipia ada ya chuo maana anakitu ambacho muda wa ziada anaweza fanya akajiingizia hela kuliko akiwa chuo muda wa ziada anawekeza kwenye ujinga ujinga na mapenzi.Pia wala hutasikia akianza kulialia kuhusu ajira baada ya chuo.
5.Sasa mtu atauliza ulikuwa unabania hela mtoto asisome shule nzuri, hela unapeleka wapi. Naam hela unapeleka kununua viwanja, kuwekeza kununua bond za serikali,UTT BONDS,HISA TBL,HISA TCC nk. Hivi ndio vitu mzazi unamuandalia mwanao au wanao ili kuvunjilia mbali mnyororo wa UMASKINI. Hata siku anamaliza shule anakosa kazi. Unaamua mtoto anataka mtajia wa kufungua let say WORKSHOP yake kulingana na ujuzi ni swala la kusukuma kiwanja kimoja au viwili unakuwa umemsaidia kuliko kuendelea kuimba ngonjera za kuwezeshwa kwa mikopo ya riba na upuuzi kama huo.
6.Hakikisha watoto wako wanamiliki passport na wanajua kuendesha gari. Maisha yakiwa hamna Bongo waweze kwenda hata huko duniani hawawezi kosa maisha maana kwanza wanaujuzi mbalimbali.
🚨🚨🚨Hii ni mbinu(LIFE HACK) ambayo mzazi akiitumia wala hawezi kujutia.
,#kupanga ni kuchagua!!!
LIKUD mzabzab Robert Heriel Mtibeli viongozi wapeni vijana wa kileo miongozo🤝