Kiukweli vijana wanapitia changamoto nyingi sana mpaka huruma.
Nikikumbuka niliyopitia mimi ndani ya miaka sita bila ajira da mwingine hawezi.
Nimefanya vitu vingi nimelima ,nimekata mkaa, nimeuza dagaa ,nimesaidia fundi, nimeuza vyuma yaani naokota mtaani naenda kuuza.,nimetembeza njegere dar kwa kichwa, nimeuza ndizi natoa mabibo nakuja kuuza mbagara nadhani kuna baadhi humu wanaweza kunifahamu.
Hasa wale wanaoishi kongowe ya kuelekea vikindu,mbagala kibondemaji huko nimeuza sana ndizi mbichi natembeza kichwani, mitaa ya kurasini mji mpya kwa tesha, kiburugwa na mitaa mingi tu hapo dar.
Ila nimechojifunza vijana tusichague kazi na wala tusikate tamaa. Ipo siku mungu atawakumbuka.