Serikali: Kila mwanafunzi atatakiwa Kusoma somo la Maadili

Serikali: Kila mwanafunzi atatakiwa Kusoma somo la Maadili

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Fuatilia yanayojiri kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 11, Kikao cha 9 leo Aprili 18, 2023.

Serikali yasisitiza wazee wapewe vitambulisho vya huduma ya afya bila malipo
Naibu Waziri Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Dkt. Festo Dugange amewakumbusha viongozi wa Mikoa na Halmashauri kuwapatia vitambulisho vya matibabu bila malipo wazee wasio na uwezo ambao wana umri wa miaka 60 na kuendelea, kutenga dirisha kwa ajili ya Wazee na kuhakikisha dawa zote muhimu zinapatikana.

Kila mwanafunzi atatakiwa kusoma somo la maadili
Akijibu swali Bungeni kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe kuwa Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mohammed Mwinjuma maarufu kwa jina la Mwana FA, amesema “Kutakuwa na somo la maadili kwenye mitaala mipya na kila Mwanafunzi lazima atalazimika kulisoma."
 
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma amesema Serikali ina lengo la kuingiza somo la Maadili kwenye Mtaala wa Elimu ili kukabiliana na Changamoto ya mmomonyoko wa maadili katika jamii.

Amesema hayo leo Aprili 18, 2023 Bungeni Dodoma alipokua akijibu swali la Mhe. Bahati Ndingo (Viti Maalum).

20230418_122226.jpg
 
Haitasaidia, mtoto atalelewa nyumbani, akija mtaani anakutana na wenzake wanamfundisha matusi.
Tembelea uswahili uone
 
Watakuwa wanafundishwa maadili shuleni halafu wakirudi mtaani wanakutana na nyimbo za kina mondi Chomoa nijambe, jamii husika ndiyo inayofundisha maadili watoto sio shuleni.
 
Wanafunzi wanaohimizwa kusoma maadili watawauliza wazazi maadili yapi?
Maana kama hao baadhi wanaohimizwa uadilifu, report ya CAG imewakuta wamekwiba bn of dollar! Au maadili yatajikita kujiepusha na bendera na matendo ya upinde wa mvua ila deals za ukwapuaji zikija Ruksa???
 
Nyimbo zake pia zinazoonesha uchi wa Mwanamke zianze kwenda hewani Katika television kuanzia saa tano usiku na singeli zipigwe Muda huo.
 
Maadili yepi... Mtaani, singeli akina Diamond chomoa nijambe. Huku juu, serikali ukikwapua mabilioni unaonekana mjanja. Maadili yaanze kwanza kwao. Uwizi wa kura pia ndyo upotofu mkubwa wa maadili.
 
Maadili yanaanza nyumbani na mazingira yake. Wanapinga rushwa wakiwa majukwaani, ndani ya ofisi zao wanashindana kula rushwa na kuiba.
 
Sisi walimu tunasubiri kwa haamu sana hilo some tuwafundishe wanafunzi maadili mema.
Tukiwa tunafundisha tunatoa na mifano wanafunzi Hampaswi kuwa Majizi kama majizi haya ya Ccm
Tunawaambia hapaswi kuwa wauaji na makatili kama Jiwe na malaika zake.
 
Hapo labda waajiri walimu wa ushauri na nasihi wengi tofauti na hapo ni kupoteza muda. Na pia waweke vipindi vya maadili kwenye vyombo vya habari ili ujumbe ufikie jamii nzima mana kama wazazi wao na jamii inayowazunguka haina maadili ni kupoteza muda.
 
Fuatilia yanayojiri kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 11, Kikao cha 9 leo Aprili 18, 2023.

Serikali yasisitiza wazee wapewe vitambulisho vya huduma ya afya bila malipo
Naibu Waziri Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Dkt. Festo Dugange amewakumbusha viongozi wa Mikoa na Halmashauri kuwapatia vitambulisho vya matibabu bila malipo wazee wasio na uwezo ambao wana umri wa miaka 60 na kuendelea, kutenga dirisha kwa ajili ya Wazee na kuhakikisha dawa zote muhimu zinapatikana.

Kila mwanafunzi atatakiwa kusoma somo la maadili
Akijibu swali Bungeni kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe kuwa Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mohammed Mwinjuma maarufu kwa jina la Mwana FA, amesema “Kutakuwa na somo la maadili kwenye mitaala mipya na kila Mwanafunzi lazima atalazimika kulisoma."

Safi sana na ianzie Chekechea Hadi Chuo Kikuu na iwe compulsory bila kufaulu Hilo hakuna kuendelea na mengine
 
Waalimu wa hayo maadili wapo? Chuo gani kinafundisha maadili nami niende? Au kanyaga twende?

Waalimu wenyewe hawana maadili[emoji968][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom