Serikali kuachia gesi kupanda bei namna hii maana yake imeruhusu miti ikatwe maporini mpaka ichakae.

Serikali kuachia gesi kupanda bei namna hii maana yake imeruhusu miti ikatwe maporini mpaka ichakae.

HOPEfull

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2021
Posts
1,882
Reaction score
2,313
Juzi tarehe 9 december uhuru day nimetoka nyumbani kwa uhuru na mtungi wangu wa gesi kwenda dukani kubadilisha au kujaza sijui wanavoita wenyewe nimepokewa na mdada ambaye siku zote namkuta hapo baada ya salamu akaniambia kuwa "gesi imepanda'. 'Leo nakuuzia kwa bei ya zamani ukija next time utakuta bei mpya' Na hapo amenifanyia kwa sababu ni mteja wake kama angekuwa mwingine angemuuzia kwa bei mpya.

Kwa kipindi kifupi bei ya gesi imepanda karibu mara 2 au 3 kila ukienda unakuta bei mpya sijui ni wapi kuna shida.Sijui kama serikali inaangalia upande wa pili wa kitu au bidhaa jinsi zinavyoweza kuathiri jamii au mazingira.

Kwa nishati ya gesi kupanda namna hii maana yake serikali imeruhusu miti iendelee kuchakazwa.Wananchi wa kawaida ambao na wenyewe walikuwa wameanza kujitutumua kutumia gesi sasa wanarudisha mitungi stoo.Ukikaa mjini huwezi ona jinsi misitu inavochakaa.

Serikali ilitakiwa itilie mkazo suala la matumizi ya gesi huko wilayani ambako miti inachakaa.Kutilia mkazo kwa kuweka bei rafiki ya gesi.

Hivi sasa tunalalamika mvua hakuna ukame mara mgawo wa umeme na maji lakini ujue habari ndio hiyo vitu vinaonekana vidogo lkn athari zake ni kubwa.

Ushauri wangu ni kuwa serikali iwe makini sana na iangalie athari ya upande wa pili inapofanya mambo yake.


Zipo bidhaa nyingine ambazo ni senstive kama sukari mafuta ya kula vitu ambavyo mwananchi wa chini anatumia kila siku.Wanapojadili vitu hivi macho yao yasiwe front page tu bali waangalie pia beyond the page.
 
kwani wana jari sasa sisi tukate tu miti ndo kilicho bakia
 
Back
Top Bottom