Serikali Kuajiri Walimu wapya 10,000 Mwaka Huu wa Fedha 2021/2022

Serikali Kuajiri Walimu wapya 10,000 Mwaka Huu wa Fedha 2021/2022

mhitimutz

Member
Joined
Jul 3, 2021
Posts
12
Reaction score
11
Ajira mpya zimepunguza uhaba wa Walimu wa Sayansi

Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Ummy Mwalimu amesema kwa Sasa hakuna Shule ya Sekondari ambayo haina Mwalimu wa Sayansi.

Waziri Ummy amesema katika ajira 6,949 zilizotewa Mwezi Juni 2021, Walimu wa Fizikia walioajiriwa ni 1,360 na Walimu wa Hisabati Ni 599 ambao wamesambazwa katika shule ambazo hazikuwa na Walimu hao hapo awali.

"Ni imani yangu sasa hakuna shule yoyote ya Sekondari nchini ambayo haina mwalimu wa sayansi hata mmoja,"amesema. Hata hivyo, ameiaagiza Mikoa kumleta taarifa iwapo kuna Shule ya Sekondari katika Halmashauri ambayo haina Mwalimu wa masomo ya Fizikia, Kemia, Baiolojia na Hisabati hata mmoja ili ufanyike msawazo wa walimu wa Sayansi.

Aidha, amesema katika mwaka huu wa fedha 2021/22 serikali inatarajia kuajiri walimu 10,000 na kipaumbele kitakuwa walimu wa Sayansi.

SOURCE:TAMISEMI FACEBOOK PAGE
 
𝐡𝐢𝐢 𝐜𝐨𝐮𝐫𝐬𝐞 𝐲𝐚 𝐮𝐚𝐥𝐢𝐦𝐮 𝐢𝐧𝐠𝐞𝐬𝐢𝐦𝐚𝐦𝐢𝐬𝐡𝐰𝐚 𝐤𝐰𝐚𝐧𝐳𝐚 𝐤𝐚𝐦𝐚 𝐦𝐢𝐚𝐤𝐚 𝐦𝐢𝐭𝐚𝐧𝐨 𝐢𝐧𝐠𝐞𝐩𝐞𝐧𝐝𝐞𝐳𝐚

𝐛𝐚𝐝𝐨 𝐤𝐮𝐧𝐚 𝐦𝐚𝐤𝐮𝐦𝐢 𝐞𝐥𝐟𝐮 𝐲𝐚 𝐰𝐚𝐚𝐥𝐢𝐦𝐮 𝐡𝐚𝐰𝐚𝐣𝐚𝐚𝐣𝐢𝐫𝐢𝐰𝐚
 
Back
Top Bottom