Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amesema Serikali kupitia Bodi ya Taaluma ya Ualimu nchini (TTPC) imeanza maandalizi ya kuratibu na kutoa leseni rasmi za ufundishaji kwa walimu nchini.
Amesema hatua hiyo inalenga kuongeza thamani, heshima na nidhamu katika taaluma ya ualimu, huku ikihakikisha kuwa kila anayefundisha anatimiza vigezo vinavyotambulika kisheria.
Profesa Mkenda ameyasema hayo Bagamoyo mkoani Pwani, wakati akizungumza na watendaji wa Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM), ambapo pia ameeleza kuhusu mabadiliko ya mitaala na utekelezaji wa Elimu ya Lazima nchini.
Soma >>> Wahitimu wa ualimu kuongezewa mwaka mmoja wa 'Intern' kabla ya kupata leseni ya kufundisha rasmi, kama ilivyo kwa madaktari
Kwa upande wao, Mtendaji Mkuu wa ADEM, Dkt. Maulid Maulid, pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Shaibu Ndemanga wamesifu juhudi za Serikali katika kuwekeza kwenye mafunzo endelevu kwa walimu.
Wamesema mafunzo ya uongozi na utawala kwa walimu pamoja na wakuu wa shule yatasaidia kuongeza ufanisi katika usimamizi wa shule na hatimaye kuinua kiwango cha elimu nchini.