Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Hao watakuwa wanawapa waalimu leseni, wao Wana leseni zinazowawezesha kuwapa wengine leseni?Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amesema Serikali kupitia Bodi ya Taaluma ya Ualimu nchini (TTPC) imeanza maandalizi ya kuratibu na kutoa leseni rasmi za ufundishaji kwa walimu nchini.
Amesema hatua hiyo inalenga kuongeza thamani, heshima na nidhamu katika taaluma ya ualimu, huku ikihakikisha kuwa kila anayefundisha anatimiza vigezo vinavyotambulika kisheria.
Profesa Mkenda ameyasema hayo Bagamoyo mkoani Pwani, wakati akizungumza na watendaji wa Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM), ambapo pia ameeleza kuhusu mabadiliko ya mitaala na utekelezaji wa Elimu ya Lazima nchini.
Soma >>> Wahitimu wa ualimu kuongezewa mwaka mmoja wa 'Intern' kabla ya kupata leseni ya kufundisha rasmi, kama ilivyo kwa madaktari
Kwa upande wao, Mtendaji Mkuu wa ADEM, Dkt. Maulid Maulid, pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Shaibu Ndemanga wamesifu juhudi za Serikali katika kuwekeza kwenye mafunzo endelevu kwa walimu.
Wamesema mafunzo ya uongozi na utawala kwa walimu pamoja na wakuu wa shule yatasaidia kuongeza ufanisi katika usimamizi wa shule na hatimaye kuinua kiwango cha elimu nchini.
Baadhi ya mipango ya serikali hushindwa kuleta tija kutokana na ushirikishwaji hafifu usiozingatia walengwa halisi badala yake wamekuwa wakitumia wawakilishi wachache sana ambao nao ni viongozi wasio na uhalisia wa kiuzoefu wa wakati huo uliopo.
Chama cha walimu kinaongozwa na walimu wenye elimu ndogo na release mdogo sana! Wizi pia mkubwa wa michango!Baadhi ya mipango ya serikali hushindwa kuleta tija kutokana na ushirikishwaji hafifu usiozingatia walengwa halisi badala yake wamekuwa wakitumia wawakilishi wachache sana ambao nao ni viongozi wasio na uhalisia wa kiuzoefu wa wakati huo uliopo.
Mifano ipo mingi ktk sekta tofauti tofauti ikiwemo hii ya elimu. Uboreshaji wa Mtaala ni mojawapo ya mfano huu ambao hadi sasa zipo changamoto nyingi ambazo zingeweza kutokea kama kungekuwepo ushirikishwaji halisi kwa walengwa wa utekelezaji wa Mtaala huo.
Ama lipo suala hili la "leseni kwa walimu" na bidii ya ualimu. Ni kweli kabisa huenda serikali ikawa na nia njema ya ufanisi wa kazi na pengine isiwe kwa manufaa ya walimu kutokana na kasoro mbalimbali ikiwemo ushirikishwaji kabla ya utekelezaji wake.
Ktk suala hili la bodi ya walimu na leseni upo uelewa mdogo sana juu ya mambo hili kwa walimu walio wengi huko makazini kwao hivyo kuleta taharuki na uelewa hasi juu ya jambo lenyewe. Hii pia huenda ikapelekea ugumu ktk utekelezaji wake.
Ni ombi langu kubwa sasa serikali ishuke kule kwa walengwa na kutoa elimu shirikishi juu ya suala hili ili kukidhi matarajio ya serikali na manufaa tarajiwa kwa walimu hao
Yaani hii serikali badala ya kuwaza mambo ya msingi na yenye tija kwa walimu, wanawaza ujinga tu?Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amesema Serikali kupitia Bodi ya Taaluma ya Ualimu nchini (TTPC) imeanza maandalizi ya kuratibu na kutoa leseni rasmi za ufundishaji kwa walimu nchini.
Amesema hatua hiyo inalenga kuongeza thamani, heshima na nidhamu katika taaluma ya ualimu, huku ikihakikisha kuwa kila anayefundisha anatimiza vigezo vinavyotambulika kisheria.
Profesa Mkenda ameyasema hayo Bagamoyo mkoani Pwani, wakati akizungumza na watendaji wa Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM), ambapo pia ameeleza kuhusu mabadiliko ya mitaala na utekelezaji wa Elimu ya Lazima nchini.
Soma >>> Wahitimu wa ualimu kuongezewa mwaka mmoja wa 'Intern' kabla ya kupata leseni ya kufundisha rasmi, kama ilivyo kwa madaktari
Kwa upande wao, Mtendaji Mkuu wa ADEM, Dkt. Maulid Maulid, pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Shaibu Ndemanga wamesifu juhudi za Serikali katika kuwekeza kwenye mafunzo endelevu kwa walimu.
Wamesema mafunzo ya uongozi na utawala kwa walimu pamoja na wakuu wa shule yatasaidia kuongeza ufanisi katika usimamizi wa shule na hatimaye kuinua kiwango cha elimu nchini.
Nani kasema hayo mkuu?Chama cha walimu kinaongozwa na walimu wenye elimu ndogo na release mdogo sana! Wizi pia mkubwa wa michango!
Bodi itawakomboa walimu na kuwapunguzia makato ya kila mwezi.
Imagine mwalimu mshahara ni 1,200,000 kwa mwezi anakatwa 2% kila mwezi hadi atakapo staafu.
Bora kulipa mara moja Tsh 120.000 kwa mwaka!