Serikali kuanza kuwawekea umeme wa REA wananchi Masikini kwa kutumia Mabavu

Serikali kuanza kuwawekea umeme wa REA wananchi Masikini kwa kutumia Mabavu

Kuna mama mmoja alifanya wiring miezi minne iliyopita mpaka Leo anasumbuliwa kuingiziwa umeme.Mama wa watu kauza mboga mboga watu wakajitolea kumfanyia wiring baada ya yeye kununua Vifaa,lakini mpaka Leo yupo gizani.anajutia sana hela Yake
 
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nishati Mh Kalemani akiwa ziarani kikazi huko mkoani Tabora , Mh Kalemani amesema kwamba haiwezekani mtu yeyote kushindwa kulipa gharama ya kuwekewa umeme huo ambayo ni Tsh 27, 000/= kwa kisingizio chochote kile.

Mh Waziri amedai serikali inafikiria kuwawekea umeme watu wote kwa gharama hata ya kuuza mifugo yao au sehemu ya mashamba yao ili kufidia .
Akimaliza kwetu anakuja kwenu. haya makulima kazi yao ni kukenua meno acha ayasulubu!
 
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nishati Mh Kalemani akiwa ziarani kikazi huko mkoani Tabora , Mh Kalemani amesema kwamba haiwezekani mtu yeyote kushindwa kulipa gharama ya kuwekewa umeme huo ambayo ni Tsh 27, 000/= kwa kisingizio chochote kile.

Mh Waziri amedai serikali inafikiria kuwawekea umeme watu wote kwa gharama hata ya kuuza mifugo yao au sehemu ya mashamba yao ili kufidia .
Ufipa bhana..hapa naona mkilia lia mtakosa mtaji wa serikali haijaleta umeme...
 
Ulikuwepo kipindi kile kuna kodi fulani ilikuwa inaitwa development levy? Au unakumbuka kipindi cha nyuma, Kuna jamii fulani kijana akitaka kuoa alikuwa anaalika vijana wenzake mabaunsa, halafu wanamvizia binti akiwa na wenzake anaenda kuchota maji mtoni/kisimani. Wanamnyakua na kumpeleka geto kwa jamaa yao, halafu
wazazi wa kijana wanaenda kutoa taarifa kwa mzazi wa binti.
Nadhani utakuwa umepata picha binti yangu.
Nilisikia kuna watu waliliwa na mamba baada ya kukimbilia kwenye mito ili kukwepa kodi ya kichwa
 
Mwambie tanesco wanauza nguzo hadi leo,kuna maeneo watu wameshindwa kuweka umeme wa shilingi 27000/=sababu wanaambiwa walipie nguzo moja hadi shilingi 330000/=
Hata hapa Morogoro mjini nguzo zinauzwa ingawa viongozi wametoa maelekezo wazi kabisa. Viongozi TANESCO wanapata wapi nguvu ya kukataa kutekeleza maagizo ya viongozi. Ombi viongozi wetu wafuatilie.
 
Kuna gharama za wiring, brackets, hiyo elfu 27 ni ya kuunganishiwa tu.

Ni jambo zuri sema changamoto ni hadhi ya nyumba zenyewe ni mtihani
 
Mimi nazani hii ni fursa ambayo tutakuja ikumbuka...

Mababu zetu walichalazwa bakora ili shule zijengwe, kwa wakati huo waliona ni mateso au manyanyaso...shule zilipo jengwa watoto wao ambao ni wazee wetu wali lazimishwa kwenda shule kwa bakora kwa fine mbali mbali nayo ilikuja onekana ni kero unyanyasaji lakini Leo wao ndio wakwanza wana jutia fursa ile na wamekuwa walimu wazuri wa kuipenda elimu na wana furaha kuona vijana wao wanasoma... Hawataki uzao wao uje kujuta kama wao wanavyo juta sasa...
Historia hii unaijua wewe peke yako, huenda isiwe ni historia ya Tz, ama labda ni ya Omani
 
Ni mkakati Mzuri hata Kama Ni wa lazima. Umeme Ni mhimu na Hicho kiwango kwakweli Ni kidogo Sana.

Lakini: Serikali itambue pia Kuna raia wake hata 10000 kuipata tu Ni shida kwahiyo suala la ulazima wangeliangalia kwa makini Sana. Pia isisahau kuwa Kuna gharama ya matengezo ya vifaa vya umeme pindi vinapo haribika na bili ambazo Kuna baadhi ya wananchi hawezi kumudu gharama zake.
 
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nishati Mh Kalemani akiwa ziarani kikazi huko mkoani Tabora , Mh Kalemani amesema kwamba haiwezekani mtu yeyote kushindwa kulipa gharama ya kuwekewa umeme huo ambayo ni Tsh 27, 000/= kwa kisingizio chochote kile.

Mh Waziri amedai serikali inafikiria kuwawekea umeme watu wote kwa gharama hata ya kuuza mifugo yao au sehemu ya mashamba yao ili kufidia .
Yani hata kama mtu mila za kwao zinakataza umeme serikali itamuwekea umeme kwa nguvu?

Haya si sawa na mambo ya mkoloni ya kodi ya kichwa kweli?
 
Ni mkakati Mzuri hata Kama Ni wa lazima. Umeme Ni mhimu na Hicho kiwango kwakweli Ni kidogo Sana.

Lakini: Serikali itambue pia Kuna raia wake hata 10000 kuipata tu Ni shida kwahiyo suala la ulazima wangeliangalia kwa makini Sana. Pia isisahau kuwa Kuna gharama ya matengezo ya vifaa vya umeme pindi vinapo haribika na bili ambazo Kuna baadhi ya wananchi hawezi kumudu gharama zake.

LUKU LUKU LUKU
wenyewe kwa elfu 10 WANAPEWA units nyingi kuliko wa mjini.
 
Leo hii nimelipa 696,700 kama gharama ya nguzo 2 na service line. nilimuuliza mfanyakazi wa Tanesco mbona Waziri amesema nguzo ni bure? akanijibu ni matamko tu ya kisiasa hayo.
 
Wanaharakati wengi hapa mnawaongelea watu wa vijijini ila asilimia kubwa hawa watu ni wazinguaji na ni chenga sana. Kuna raia kibao unakuta wana rasrimali kibao(mifugo mara nyingi) ila unakuta anaenjoy tu kuona wanapandana na madume kuangukia migongo wanapopiga bao.

Badala wawatumie kujikwamua katika changamoto mbalimbali za kiuchumi. Hapa tunaongelea mtu kushindwa kulipia 27,000 aunganishiwe umeme ila ana beberu la mbuzi limekomaa anafurahia linavozidi kuwa na harufu na kukesha linapiga kelele na kusumbua majike usiku kucha au unakuta hawezi kulipia umeme ila ana dume la ng'ombe ambalo ana enjoy linavozalisha ng'ombe kijiji kizima ni sifa tu kila ndama anaempita anakwambia unaona ile, ni kazi ya kamanda langu mixa ameliita hadi jina.

Watu wana mifugo hadi imezidi idadi utakuta mfano wanalazimika kulala na vitoto vya mbuzi magetoni kwa kuwa zizi limekuwa dogo sometimes umelala usiku unashangaa kitoto cha mbuzi kimekupigia chafya usoni au kinakukokojolea ukiwambia uzeni hata mbuzi mmoja fanya kitu cha msingi maishani wanaanza ngonjera za ujamaa na azimio la Arusha. Kwa kweli mi namsupport waziri afanye tu vijijini watu ni wapuuzi sana.

Unakuta mwanae anaenda kupigwa mimba shule za town kwa kuhongwa kiepe yai wakati nyumbani kwa wamepanda viazi mviringo migombani na wana kuku kibao wanataga ila hajawahi kula kiepe.

Kijijini watu sio maskini kama wengi tunavoamini ila mindset zao ndo za kipuuzi tu
 
unayasema haya na huku hujawahi fika vijijini. acha zile center zenu. vijijini.
Wanaharakati wengi hapa mnawaongelea watu wa vijijini ila asilimia kubwa hawa watu ni wazinguaji na ni chenga sana. Kuna raia kibao unakuta wana rasrimali kibao(mifugo mara nyingi) ila unakuta anaenjoy tu kuona wanapandana na madume kuangukia migongo wanapopiga bao. Badala wawatumie kujikwamua katika changamoto mbalimbali za kiuchumi. Hapa tunaongelea mtu kushindwa kulipia 27,000 aunganishiwe umeme ila ana beberu la mbuzi limekomaa anafurahia linavozidi kuwa na harufu na kukesha linapiga kelele na kusumbua majike usiku kucha au unakuta hawezi kulipia umeme ila ana dume la ng'ombe ambalo ana enjoy linavozalisha ng'ombe kijiji kizima ni sifa tu kila ndama anaempita anakwambia unaona ile, ni kazi ya kamanda langu mixa ameliita hadi jina. Watu wana mifugo hadi imezidi idadi utakuta mfano wanalazimika kulala na vitoto vya mbuzi magetoni kwa kuwa zizi limekuwa dogo sometimes umelala usiku unashangaa kitoto cha mbuzi kimekupigia chafya usoni au kinakukokojolea ukiwambia uzeni hata mbuzi mmoja fanya kitu cha msingi maishani wanaanza ngonjera za ujamaa na azimio la Arusha. Kwa kweli mi namsupport waziri afanye tu vijijini watu ni wapuuzi sana. Unakuta mwanae anaenda kupigwa mimba shule za town kwa kuhongwa kiepe yai wakati nyumbani kwa wamepanda viazi mviringo migombani na wana kuku kibao wanataga ila hajawahi kula kiepe. Kijijini watu sio maskini kama wengi tunavoamini ila mindset zao ndo za kipuuzi tu
 
Mwambie tanesco wanauza nguzo hadi leo,kuna maeneo watu wameshindwa kuweka umeme wa shilingi 27000/=sababu wanaambiwa walipie nguzo moja hadi shilingi 330000/=
Ukiuziwa dai risiti ya nguzo. TANESCO wanacharge umbali na sio nguzo.
 
Back
Top Bottom