Serikali kuanza usajili wa watu wenye umri chini ya miaka 18 kuwapatia Jamii namba

Serikali kuanza usajili wa watu wenye umri chini ya miaka 18 kuwapatia Jamii namba

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251

Serikali imepanga kuanza usajili na utambulisho wa watu wenye umri chini ya miaka 18 kwa lengo la kuwapatia Jamii Namba. Hiki kimekuwa kilio cha muda mrefu sana.

Mpango huu utawezesha kila mtu kuwa na namba ya utambulisho wa kipekee kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali za kijamii na kiuchumi tangu kuzaliwa hadi mwisho wa maisha ya mtu hapa duniani.

Katika kufanikisha hili, katika kipindi cha mwaka 2026/2027, serikali imepanga kufanya majaribio ya usajili wa watoto katika Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa, Rungwe mkoani Mbeya, na Kusini mkoani Kusini Zanzibar.

Jamii Namba itakuwa chachu ya mabadiliko makubwa katika utoaji wa huduma kwa watu wenye umri wa chini ya miaka 18 ambapo maeneo yote ya utoaji wa huduma yatahusika ikiwemo utoaji wa mikopo ya elimu ya juu, bima ya afya kwa wote, ujumuishi wa kifedha, kufungua akaunti za benki, na usajili wa laini za simu.
 
Ni jambo zuri maana vijana wa nchi jirani ni wengi hapa Dar wanajifanya Waha, kazi yao kubwa ni biashara ndogondogo ya kuuza karanga, pipi, pita Kariakoo na Karume kila anayefanya iyo biashara sio raia serikali ipo bize sijui kama wanajua maana hatua hazichukuliwi.
 
Mpango huu utawezesha kila mtu kuwa na namba ya utambulisho wa kipekee kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali za kijamii na kiuchumi tangu kuzaliwa hadi mwisho wa maisha ya mtu hapa duniani.
Chai,
Lengo ni kutumia hizo data kwenye kuchakata na kuiba kura kiweledi zaidi
 
Back
Top Bottom