Serikali kuburuzwa mahakamani kuhusu wizara ya afya kubadili mitaala ya vyuo vya afya vya kati bila kufuata utaratibu

Travelogue_tz

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2010
Posts
855
Reaction score
1,224
Na Mwandishi Wetu

Jopo la Mawakili kumi na nne (14), wataalamu wa takwimu nane (8) na wataalamu wa mitaala watatu (3) kutoka katika kampuni za ushauri elekezi na uwakili zinapanga kuiburuza Serikali Mahakamani kutokana na uamuzi ya wizara ya afya kupitia kurugenzi yake ya mafunzo na rasilimali watu, na mabaraza yake ya taaluma (proffessional bodies) kubadili mitaala yake ya kufundishia kozi za afya bila kufuata utaratibu na kanuni zilizoainishwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET).

Katika nakala ya maelezo ya kesi ambayo chanzo chetu kimeweza kuiona, walalamikaji kupitia kwa jopo la mawakili wao, na wataalamu wanailalamikia Serikali kwa kitendo chake cha kushindwa kuzingatia kanuni na taratibu za uandaaji/upitiaji wa mitaala, na hivyo kusababisha kero kubwa kwa wananchi na wadau wa elimu ya mafunzo ya afya.

Fauzia Mashaka Kundecha na wenzake 120 katika kesi hiyo wanawashtaki Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya (mshtakiwa wa kwanza), Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) (mshitakiwa wa pili) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (mshtakiwa wa tatu).
Wawasilishaji wa maombi hayo ni wadau wanaotoa mafunzo kwa kada za afya ngazi ya kati kutoka katika zaidi ya Vyuo 170.

Hatua hiyo inafuatia mgogoro wa muda mrefu kati yake na Wizara ya Afya kuhusu kukiukwa kwa taratibu na kanuni za maandalizi ya mitaala na hivyo kuathiri hali ya utoaji wa mafunzo Nchini Tanzania.
Katika hatua ya awali walalamikaji watawasilisha notisi ya siku 90 kwa Serikali wakiitarifu kuhusu nia yao ya kutaka Mahakama iingilie kati suala la matumizi ya mitaala inayokinzana na taratibu na miongozo.

Kiongozi wa jopo la mawakili hao anayewawakilisha walalamikaji katika kesi hiyo ambaye ameiambia chanzo chetu cha habari kwamba nia ya kuishtaki Serikali imetokana na juhudi za kulitatua suala hilo kwa njia ya majadiliano kushindwa kuzaa matunda kwa takribani miaka sita (6).
“Hatua hii ni muhimu sana kwani utekelezaji wa mitaala hii unakwenda kuwazuia takribani watoto 15,000 wenye vigezo na sifa kutoka shule za kata kudahiliwa katika vyuo vya afya Nchini ,” Kiongozi wa jopo la mawakili alibainisha wakati wa mahojiano.

“Wadau mbalimbali wakiwemo Vyuo vya Afya, NACTVET, Wanafunzi waliohitimu kidato cha nne na wazazi walikuwa wamepanga kwamba kufikia katikati ya Mei 2024 wawe wameanza taratibu za udahili ,” aliongeza Wakili huyo.

“Pia, zoezi la mabadiliko ya mitaala na upandishwaji wa vigezo vya udahili linakusudiwa kutekelezwa katika kipindi ambacho wadau wamekwishajiandaa na zoezi la udahili na hakuna kozi mbadala ya afya ambayo Watoto hawa wanaweza kusoma kwa sasa,” Wakili alisema”. “Kitendo hiki kinawafanya wahitimu wa kidato cha nne kushindwa kudahiliwa katika kozi za afya.”

Alipoulizwa kama anafahamu chochote kuhusiana na mpango huo wa wadau wa vyuo vya afya kuishitaki Serikali, Mtumishi mmoja wa Wizara ya Afya ambaye hakutaka jina lake kutajwa alikiri kufahamu mpango huo, japo alidai kwamba wadau hao wamepewa fursa ya kujadiliana na Wizara ili kumaliza jambo hili. Mtumishi huyo alikiri kutambua kwamba malalamiko ya wadau hao yana mantiki kwa kuwa tathmini ya hali ya mahitaji ( situational analysis report) ilivyofanywa na timu ya wataalamu iliyoundwa na baraza la famasia na kutumia zaidi ya Tsh. 450,000,000 ilishindwa kubainisha sababu ya kubadili vigezo vya udahili kwa kada hiyo. Aidha chanzo hicho kilieleza kwamba wataalamu hao walizunguka nchi nzima na kuhoji watu 79 pekee ambapo wakufunzi walikuwa 15 na wahitimu (graduates) 15 idadi ambayo haiwezi kutoa matokeo jumuishi. Taarifa ya wataalamu pia ilibaini kwamba Mbinu iliyotumika katika kuchagua washiriki, idadi ya washiriki na kukusanya maoni ina wigo finyu wa kutoa matokeo jumuishi na ya kuaminiwa kupelekea kubadili maudhui na/au vigezo vya udahili katika mtaala, Ushirikishwaji hafifu au kutokushirikishwa kabisa kwa wadau muhimu kama wanafunzi, Kukosekana kwa sifa ya kuwa na mafunzo ya kufundisha mtaala wa umahiri ( CBET training) na usajili wa mabaraza (proffessional licences) kwa wakufunzi kumi na tano (15) waliotoa maoni, Kutumia neno “low quality students” kama kielekezo cha wanafunzi dhaifu wasioweza kumudu masomo yao, bila kufanya rejea ya mwenendo wa ufaulu wa wanafunzi hao kwa mitihani ya mwisho wa muhula na kushindwa kuonesha mahusiano thabiti ya mahitaji ya kubadili vigezo vya udahili na ongezeko ya somo la hisabati, fizikia na kiingereza.

Mvutano wa muda mrefu
Chimbuko la mgogoro wa mitaala na vigezo vya udahili lilianza mwaka 2018,mgogoro ulitokana na maamuzi ya Baraza la Uuguzi kupandisha vigezo vya masomo ya kujiunga kwa matokeo ya kidato cha nne kutoka Physics D kuwa C, Chemistry D kuwa C, Biology kutoka D kuwa C. Sababu za kupanda kwa vigezo hivyo hazikuanishwa bali ilionekana ni maamuzi bila utafiti wowote kwani ufaulu wa wanafunzi wa kozi hiyo katika mitihani ya mwisho ya masomo (Wizara) haukuwahi kuwa mbaya (Rejea kiambatanisho cha matokeo ya wahitimu wa kozi ya Ukunga na Uuguzi wa miaka tano mfululizo kwa vigezo vya awali). Hivyo kiliitishwa kikao cha wadau na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Jinsia Wazee na Watoto kikihusisha wawakilishi wa mabaraza, wamiliki wa vyuo vya binafsi, Wawakilishi wa Wakuu wa vyuo vya serikali na Chama Cha Wauguzi. Kufuatia majadiliano ya kikao kile ilionekana kuongeza vigezo hakukuwa na msingi wowote kitaaluma na kimahitaji hivyo vigezo vya awali viliendelea kutumika.

Mgogoro huu uliibuka tena mwaka 2021 sasa ukihusisha kozi ya Famasia. Kufuatia utengenezaji wa mtaala mpya ambao haukuhusisha wadau na hasa vyuo vya Afya. Vigezo vilipandishwa kutoka ufahulu wa kidato cha nne wa alama D (pass) wa masomo ya Chemistry, Biology na masomo mengine mawili yasiyo ya dini na kuwa ufaulu (pass) wa masomo ya Physics, Chemistry, Biology, Mathematics na English.
Mapema mwaka 2022 kufuatia vigezo hivi wadau walikutana na Mh. Naibu Waziri Afya na timu ya Wizara na baadae Mh. Waziri wa Afya. Kufuatia vikao hivyo Mheshimiwa Waziri aliagiza kuitishwa kikao cha wadau ili kujadili mtaala huu na vigezo hivyo vipya kabla ya utekelezaji wake. Kwa hatua ya majadiliano ilikofikia tulisubiria wito wa kikao cha wadau kama ilivyoagizwa na Mheshimiwa Waziri Mei 2022.

Mgogoro umeibuka upya sasa mwezi mei 2024 kufuatia kupandisha kwa vigezo katika fani za Ukunga na Uuguzi,Maabara,Famasia,Mazingira,Tiba ya Mazoezi ya viungo na Usimamizi wa Nyaraka za Afya (Health Records) kama inavyoonekana kwenye Kitabu cha Mwongozo wa Udahili cha Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) toleo la 2024/2025. Katika hatua hii upandaji wa vigezo umekuwa na tabia mtambuka,mabadiliko.mengine yakifanyika kwa mitaala hiyohiyo iliyopo na mabadiliko mengine yakionekana kuendana na mabadiliko ya mtaala. Kwa hatua hii ya ukuaji wa mgogoro huu ipo haja ya mjadala mpana kuhusu mtiririko wa mabadiliko yanayotokea,utaratibu,uhusishwaji wa wadau na utekelezaji wa maamuzi ya pamoja.

Mnamo Mei 04, 2024, Waziri wa Afya Ummy A. Mwalimu aliwakutanisha tena wadau hawa na Watendaji wa Wizara yake ambapo alisitisha utekelezaji wa mitaala hiyo na vigezo vya udahili na kuwataka kujadiliana ili kufikia muafaka, kikao ambacho kinatarajia kufanyika muda wowote kuanzia sasa.

Ombi la dharura
Hatua ya kuishitaki Serikali inaweza kufuata baada ya mikakati ya awali iliyochukuliwa na wadau hao kujikwamua na usumbufu huo kuchukua muda mrefu kutoa matokeo yaliyotarajiwa.
Wakili kiongozi anayewawakilisha wadau hao, alisema notisi ya kufungua kesi hiyo inaweza kuwasilishwa Mahakama Kuu Tanzania, Dodoma muda wowote kuanzia wiki ijayo.​
 
Wawaburuze tu kwakweli. Hawa serikali wanataka kuzoea kubadilibadili mitaala bila utaratibu maalum
 
Serikali hii ,watumishi wa hovyo sana wakishakuwa na madeni mtaani ya bia wanajiandalia project

Million, ,zotehizo wakahoji watu 47 tu ,kweli!!

Naomba niwe shahidi mahakani
 
Kwa tafsiri ndogo Kupandishwa kwa vigezo kwenye mtaala mpya kunamaanisha vyuo vingi vitakosa wanafunzi walio na sifa za kujiunga na hao watakaofanikiwa kuwa wahitimu bora kuliko sasa....mtaala wa sasa unatoa wahitimu wengi wenye ubora hafifu.....
Je, ubora wa mhitimu unapimwa na vigezo vya uudahili pekee ? ina maana wanaofaulu vizuri ndio wana ubora kazini na wasiofaulu vizuri wana ubora hafifu ?
 
Kwa tafsiri ndogo Kupandishwa kwa vigezo kwenye mtaala mpya kunamaanisha vyuo vingi vitakosa wanafunzi walio na sifa za kujiunga na hao watakaofanikiwa kuwa wahitimu bora kuliko sasa....mtaala wa sasa unatoa wahitimu wengi wenye ubora hafifu.....
Biashara za watu zinakufa watu wamekopa pesa wajawekeza kwa kujenga maghorofa wana daiwa na benki pesa, suala la kupandisha vigezo vya kujiunga na vyuo ni tishio kubwa kwa biashara zao, wala sio la Uzalenda au kielimu hayo yote ni kutishia wizara ekejeshe vigezo vya awali........
 
Hivi vyuo vimegeuza afya kuwa biashara
Hata shule za primary na sekondari ni biashara tayari watu kuwekeza pesa zao nyingi ila elimu inashuka kwasbb lengo lau ni kufaulu mitihani sio kuelimisha watoto, na serikali kama key regulator imeshindwa hata kusimamia shule zake yenyewe, inafaulisha tu kwa kuwapa marks za bure.
 
Je, ubora wa mhitimu unapimwa na vigezo vya uudahili pekee ? ina maana wanaofaulu vizuri ndio wana ubora kazini na wasiofaulu vizuri wana ubora hafifu
Ufaulu mzuri wa English, Hesabu, Biology na hayo mengine kwa ajili ya udahili wa kozi ya afya ni muhimu kwa kweli....yanayofanyika kwenye baadhi ya vyuo ili wanafunzi wafaulu ni ya aibu....hizi kozi si kwa ajili ya kila mtu....tuwaache wenye sifa wadahiliwe.....
 
Na Mwandishi Wetu

Jopo la Mawakili kumi na nne (14), wataalamu wa takwimu nane (8) na wataalamu wa mitaala watatu (3) kutoka katika kampuni za ushauri elekezi na uwakili zinapanga kuiburuza Serikali Mahakamani kutokana na uamuzi ya wizara ya afya kupitia kurugenzi yake ya mafunzo na rasilimali watu, na mabaraza yake ya taaluma (proffessional bodies) kubadili mitaala yake ya kufundishia kozi za afya bila kufuata utaratibu na kanuni zilizoainishwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET).

Katika nakala ya maelezo ya kesi ambayo chanzo chetu kimeweza kuiona, walalamikaji kupitia kwa jopo la mawakili wao, na wataalamu wanailalamikia Serikali kwa kitendo chake cha kushindwa kuzingatia kanuni na taratibu za uandaaji/upitiaji wa mitaala, na hivyo kusababisha kero kubwa kwa wananchi na wadau wa elimu ya mafunzo ya afya.

Fauzia Mashaka Kundecha na wenzake 120 katika kesi hiyo wanawashtaki Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya (mshtakiwa wa kwanza), Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) (mshitakiwa wa pili) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (mshtakiwa wa tatu).
Wawasilishaji wa maombi hayo ni wadau wanaotoa mafunzo kwa kada za afya ngazi ya kati kutoka katika zaidi ya Vyuo 170.

Hatua hiyo inafuatia mgogoro wa muda mrefu kati yake na Wizara ya Afya kuhusu kukiukwa kwa taratibu na kanuni za maandalizi ya mitaala na hivyo kuathiri hali ya utoaji wa mafunzo Nchini Tanzania.
Katika hatua ya awali walalamikaji watawasilisha notisi ya siku 90 kwa Serikali wakiitarifu kuhusu nia yao ya kutaka Mahakama iingilie kati suala la matumizi ya mitaala inayokinzana na taratibu na miongozo.

Kiongozi wa jopo la mawakili hao anayewawakilisha walalamikaji katika kesi hiyo ambaye ameiambia chanzo chetu cha habari kwamba nia ya kuishtaki Serikali imetokana na juhudi za kulitatua suala hilo kwa njia ya majadiliano kushindwa kuzaa matunda kwa takribani miaka sita (6).
“Hatua hii ni muhimu sana kwani utekelezaji wa mitaala hii unakwenda kuwazuia takribani watoto 15,000 wenye vigezo na sifa kutoka shule za kata kudahiliwa katika vyuo vya afya Nchini ,” Kiongozi wa jopo la mawakili alibainisha wakati wa mahojiano.

“Wadau mbalimbali wakiwemo Vyuo vya Afya, NACTVET, Wanafunzi waliohitimu kidato cha nne na wazazi walikuwa wamepanga kwamba kufikia katikati ya Mei 2024 wawe wameanza taratibu za udahili ,” aliongeza Wakili huyo.

“Pia, zoezi la mabadiliko ya mitaala na upandishwaji wa vigezo vya udahili linakusudiwa kutekelezwa katika kipindi ambacho wadau wamekwishajiandaa na zoezi la udahili na hakuna kozi mbadala ya afya ambayo Watoto hawa wanaweza kusoma kwa sasa,” Wakili alisema”. “Kitendo hiki kinawafanya wahitimu wa kidato cha nne kushindwa kudahiliwa katika kozi za afya.”

Alipoulizwa kama anafahamu chochote kuhusiana na mpango huo wa wadau wa vyuo vya afya kuishitaki Serikali, Mtumishi mmoja wa Wizara ya Afya ambaye hakutaka jina lake kutajwa alikiri kufahamu mpango huo, japo alidai kwamba wadau hao wamepewa fursa ya kujadiliana na Wizara ili kumaliza jambo hili. Mtumishi huyo alikiri kutambua kwamba malalamiko ya wadau hao yana mantiki kwa kuwa tathmini ya hali ya mahitaji ( situational analysis report) ilivyofanywa na timu ya wataalamu iliyoundwa na baraza la famasia na kutumia zaidi ya Tsh. 450,000,000 ilishindwa kubainisha sababu ya kubadili vigezo vya udahili kwa kada hiyo. Aidha chanzo hicho kilieleza kwamba wataalamu hao walizunguka nchi nzima na kuhoji watu 79 pekee ambapo wakufunzi walikuwa 15 na wahitimu (graduates) 15 idadi ambayo haiwezi kutoa matokeo jumuishi. Taarifa ya wataalamu pia ilibaini kwamba Mbinu iliyotumika katika kuchagua washiriki, idadi ya washiriki na kukusanya maoni ina wigo finyu wa kutoa matokeo jumuishi na ya kuaminiwa kupelekea kubadili maudhui na/au vigezo vya udahili katika mtaala, Ushirikishwaji hafifu au kutokushirikishwa kabisa kwa wadau muhimu kama wanafunzi, Kukosekana kwa sifa ya kuwa na mafunzo ya kufundisha mtaala wa umahiri ( CBET training) na usajili wa mabaraza (proffessional licences) kwa wakufunzi kumi na tano (15) waliotoa maoni, Kutumia neno “low quality students” kama kielekezo cha wanafunzi dhaifu wasioweza kumudu masomo yao, bila kufanya rejea ya mwenendo wa ufaulu wa wanafunzi hao kwa mitihani ya mwisho wa muhula na kushindwa kuonesha mahusiano thabiti ya mahitaji ya kubadili vigezo vya udahili na ongezeko ya somo la hisabati, fizikia na kiingereza.

Mvutano wa muda mrefu
Chimbuko la mgogoro wa mitaala na vigezo vya udahili lilianza mwaka 2018,mgogoro ulitokana na maamuzi ya Baraza la Uuguzi kupandisha vigezo vya masomo ya kujiunga kwa matokeo ya kidato cha nne kutoka Physics D kuwa C, Chemistry D kuwa C, Biology kutoka D kuwa C. Sababu za kupanda kwa vigezo hivyo hazikuanishwa bali ilionekana ni maamuzi bila utafiti wowote kwani ufaulu wa wanafunzi wa kozi hiyo katika mitihani ya mwisho ya masomo (Wizara) haukuwahi kuwa mbaya (Rejea kiambatanisho cha matokeo ya wahitimu wa kozi ya Ukunga na Uuguzi wa miaka tano mfululizo kwa vigezo vya awali). Hivyo kiliitishwa kikao cha wadau na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Jinsia Wazee na Watoto kikihusisha wawakilishi wa mabaraza, wamiliki wa vyuo vya binafsi, Wawakilishi wa Wakuu wa vyuo vya serikali na Chama Cha Wauguzi. Kufuatia majadiliano ya kikao kile ilionekana kuongeza vigezo hakukuwa na msingi wowote kitaaluma na kimahitaji hivyo vigezo vya awali viliendelea kutumika.

Mgogoro huu uliibuka tena mwaka 2021 sasa ukihusisha kozi ya Famasia. Kufuatia utengenezaji wa mtaala mpya ambao haukuhusisha wadau na hasa vyuo vya Afya. Vigezo vilipandishwa kutoka ufahulu wa kidato cha nne wa alama D (pass) wa masomo ya Chemistry, Biology na masomo mengine mawili yasiyo ya dini na kuwa ufaulu (pass) wa masomo ya Physics, Chemistry, Biology, Mathematics na English.
Mapema mwaka 2022 kufuatia vigezo hivi wadau walikutana na Mh. Naibu Waziri Afya na timu ya Wizara na baadae Mh. Waziri wa Afya. Kufuatia vikao hivyo Mheshimiwa Waziri aliagiza kuitishwa kikao cha wadau ili kujadili mtaala huu na vigezo hivyo vipya kabla ya utekelezaji wake. Kwa hatua ya majadiliano ilikofikia tulisubiria wito wa kikao cha wadau kama ilivyoagizwa na Mheshimiwa Waziri Mei 2022.

Mgogoro umeibuka upya sasa mwezi mei 2024 kufuatia kupandisha kwa vigezo katika fani za Ukunga na Uuguzi,Maabara,Famasia,Mazingira,Tiba ya Mazoezi ya viungo na Usimamizi wa Nyaraka za Afya (Health Records) kama inavyoonekana kwenye Kitabu cha Mwongozo wa Udahili cha Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) toleo la 2024/2025. Katika hatua hii upandaji wa vigezo umekuwa na tabia mtambuka,mabadiliko.mengine yakifanyika kwa mitaala hiyohiyo iliyopo na mabadiliko mengine yakionekana kuendana na mabadiliko ya mtaala. Kwa hatua hii ya ukuaji wa mgogoro huu ipo haja ya mjadala mpana kuhusu mtiririko wa mabadiliko yanayotokea,utaratibu,uhusishwaji wa wadau na utekelezaji wa maamuzi ya pamoja.

Mnamo Mei 04, 2024, Waziri wa Afya Ummy A. Mwalimu aliwakutanisha tena wadau hawa na Watendaji wa Wizara yake ambapo alisitisha utekelezaji wa mitaala hiyo na vigezo vya udahili na kuwataka kujadiliana ili kufikia muafaka, kikao ambacho kinatarajia kufanyika muda wowote kuanzia sasa.

Ombi la dharura
Hatua ya kuishitaki Serikali inaweza kufuata baada ya mikakati ya awali iliyochukuliwa na wadau hao kujikwamua na usumbufu huo kuchukua muda mrefu kutoa matokeo yaliyotarajiwa.
Wakili kiongozi anayewawakilisha wadau hao, alisema notisi ya kufungua kesi hiyo inaweza kuwasilishwa Mahakama Kuu Tanzania, Dodoma muda wowote kuanzia wiki ijayo.​
Mnaleta upuuzi wenu mpaka mambo ya elimu? Ulitaka ifuate utaratibu gani
 
Wawaburuze tu kwakweli. Hawa serikali wanataka kuzoea kubadilibadili mitaala bila utaratibu maalum
Kwa mahakama hizi?!! Hata hizo chache ambazo serikali imeshindwa wamekuwa wakikataa kutekeleza hukumu ya mahakama, na hakuna wa kuwafanya kitu!!
 
Na Mwandishi Wetu
.......Alipoulizwa kama anafahamu chochote kuhusiana na mpango huo wa wadau wa vyuo vya afya kuishitaki Serikali, Mtumishi mmoja wa Wizara ya Afya ambaye hakutaka jina lake kutajwa alikiri kufahamu mpango huo, japo alidai kwamba wadau hao wamepewa fursa ya kujadiliana na Wizara ili kumaliza jambo hili. Mtumishi huyo alikiri kutambua kwamba malalamiko ya wadau hao yana mantiki kwa kuwa tathmini ya hali ya mahitaji ( situational analysis report) ilivyofanywa na timu ya wataalamu iliyoundwa na baraza la famasia na kutumia zaidi ya Tsh. 450,000,000 ilishindwa kubainisha sababu ya kubadili vigezo vya udahili kwa kada hiyo. Aidha chanzo hicho kilieleza kwamba wataalamu hao walizunguka nchi nzima na kuhoji watu 79 pekee ambapo wakufunzi walikuwa 15 na wahitimu (graduates) 15 idadi ambayo haiwezi kutoa matokeo jumuishi. Taarifa ya wataalamu pia ilibaini kwamba Mbinu iliyotumika katika kuchagua washiriki, idadi ya washiriki na kukusanya maoni ina wigo finyu wa kutoa matokeo jumuishi na ya kuaminiwa kupelekea kubadili maudhui na/au vigezo vya udahili katika mtaala, Ushirikishwaji hafifu au kutokushirikishwa kabisa kwa wadau muhimu kama wanafunzi, Kukosekana kwa sifa ya kuwa na mafunzo ya kufundisha mtaala wa umahiri ( CBET training) na usajili wa mabaraza (proffessional licences) kwa wakufunzi kumi na tano (15) waliotoa maoni, Kutumia neno “low quality students” kama kielekezo cha wanafunzi dhaifu wasioweza kumudu masomo yao, bila kufanya rejea ya mwenendo wa ufaulu wa wanafunzi hao kwa mitihani ya mwisho wa muhula na kushindwa kuonesha mahusiano thabiti ya mahitaji ya kubadili vigezo vya udahili na ongezeko ya somo la hisabati, fizikia na kiingereza.
Hii ni Wizara inayoongozwa na Waziri asiyejali wala nini. yeye ni praise and chorus kila anapoenda. Hana tija
..........Mnamo Mei 04, 2024, Waziri wa Afya Ummy A. Mwalimu aliwakutanisha tena wadau hawa na Watendaji wa Wizara yake ambapo alisitisha utekelezaji wa mitaala hiyo na vigezo vya udahili na kuwataka kujadiliana ili kufikia muafaka, kikao ambacho kinatarajia kufanyika muda wowote kuanzia sasa.​
Waziri utadhani hajui kinachoendelea wakati yeye ndo muidhinishaji wa michakato yote.
Huyu mama Wizara anaiendesha bila ethics za utawala bora

Ombi la dharura
Hatua ya kuishitaki Serikali inaweza kufuata baada ya mikakati ya awali iliyochukuliwa na wadau hao kujikwamua na usumbufu huo kuchukua muda mrefu kutoa matokeo yaliyotarajiwa.
Wakili kiongozi anayewawakilisha wadau hao, alisema notisi ya kufungua kesi hiyo inaweza kuwasilishwa Mahakama Kuu Tanzania, Dodoma muda wowote kuanzia wiki ijayo.​
Serikali kushtakiwa ni aibu
 
Hii ni Wizara inayoongozwa na Waziri asiyejali wala nini. yeye ni praise and chorus kila anapoenda. Hana tija

Waziri utadhani hakui kinachoendelea wakati yeye ndo muidhinishaji wa michakato yote.
Huyu mama Wizara anaiendesha bila ethics za utawala bora

Serikali kushtakiwa ni aibu
Kwa Tanzania hakuna aibu kwanza ni kumpa activity AG
 
Hata shule za primary na sekondari ni biashara tayari watu kuwekeza pesa zao nyingi ila elimu inashuka kwasbb lengo lau ni kufaulu mitihani sio kuelimisha watoto, na serikali kama key regulator imeshindwa hata kusimamia shule zake yenyewe, inafaulisha tu kwa kuwapa marks za bure.
Tuna nchi ya kijinga sn, mtoto anapimwa kwa siku moja na amekaa darasani 7 years
 
Na anavyosoma maoni yetu humu mitandaoni ndo anazidi kuonesha roho mbaya yake kwa Watanzania.

Huwa ana moyo ambao ni aghalabu kumkuta mwanamke anao. yaani HAJALI wala HASHAURIKI
Ushosti unatuharibia nchi walah
Afya pale ni sehemu ya utakatishaji wa fedha za umma sababu ya usimamizi mbovu wa huyu ajuza, pale 90% ya staff wanavitambi hatari sn
 
Back
Top Bottom