Serikali kuburuzwa mahakamani kuhusu wizara ya afya kubadili mitaala ya vyuo vya afya vya kati bila kufuata utaratibu

Kwa tafsiri ndogo Kupandishwa kwa vigezo kwenye mtaala mpya kunamaanisha vyuo vingi vitakosa wanafunzi walio na sifa za kujiunga na hao watakaofanikiwa kuwa wahitimu bora kuliko sasa....mtaala wa sasa unatoa wahitimu wengi wenye ubora hafifu.....
Una uhakika na unachokihisi?
 
Ufaulu mzuri wa English, Hesabu, Biology na hayo mengine kwa ajili ya udahili wa kozi ya afya ni muhimu kwa kweli....yanayofanyika kwenye baadhi ya vyuo ili wanafunzi wafaulu ni ya aibu....hizi kozi si kwa ajili ya kila mtu....tuwaache wenye sifa wadahiliwe.....
Unaweza kuwa na point ila ni hisia.

Malalamiko ya wahitimu yana mantiki na hapo ndipo suala la kuwepo na taasisi ambazo hazitimizi wajibu wake. Nchi hii kuna Professional bodies kama Pharmacy Council ambayo inatakiwa kuregulate Pharmacists lakini inajiingiza kuregulate mafunzo. Inashindwa kufanya kazi yake ya kuregulate Profession. Hapo ndipo tunapata wasio stahili. Ni kosa kufikiria kuwa kila mwanachuo atafaulu. Maana ya mtihani ni kuchuja; kuna watakaofaulu na watakaoshindwa.

Ili unielewe nitatumia mfano wa Chai (Mfamasia aliyewiva). Chai hupikwa katika sufuria (Chuo) na ikishaiva kabla ya kuinywa huchujwa (Chujio ni Mabaraza ya Taaluma kama Pharmacy Council). Kwa mnywaji (wateja wa Pahrmacy) anataka kupata chai iliyochujwa bila machicha (Mfamasia).

Swali ni je, kama chai ina machicha, nani wa kulaumu? Sufuria au chujio.

Kwa muktadha huo, kama Mabaraza yangekuwa yanafanya kazi yake ya kuchuja, kusingekuwa na tatizo la wafamasia vihiyo. Hivyo kulaumu Chuo kwa mfamasia mbovu ni kosa maana chuo hakisajili wafamasia, kinaandaa wafamasia na baraza linasajili wafamasia.
 
Hapo kwa vigezo vipunguzwe ili waingie wengi vyuoni. Natamani kuona hilo likitokea.
 
Umeongea vizuri sana...ahsante....kwa mfano huohuo wa chujio ukifuatilia matokeo ya mitihani ya leseni ya Baraza la Famasi ndio utaona chujio linavyofanya kazi......mpaka unajiuliza huko vyuoni kulikoni.....inawezekanaje mtu anafaulu mitihani ya chuo na anafeli vibaya mitihani ya leseni???? Na ukifuatilia kwa ukaribu sababu utakuta ni hizo...hesabu, english n.k....fuatilia masomo wanayofeli zaidi utagundua kitu......ndio maana nakubali bila shaka ufaulu kwenye masomo ya hesabu na Kiingereza ni muhimu sana sana.....na ufaulu wenyewe ni alama ya D.......wa chini kabisa.....yaani sielewi mwanafunzi mwenye F ya hesabu na kiingereza anakubaliwaje kusoma kozi ya CO, Nursing au ufamasia......
 
Tatizo wasomi wengi wa kitanzania hawatumii akili zao vizuri.Unaweza ukashangaa sana watu wameshupaa na vigezo kupandishwa lakini hawajali mchakato wa kuwatengeneza hawa wataalamu.
Huku kwenye mchakato ndiko kuna utusitusi mwingi sana.
Aina ya mitaala,malengo yake,upimaji wake na hatimaye zao la mchakato wote.
Mtu anaandaliwa kukariri sehemu za mitambo ya kutengeneza dawa kwa njia ya picha badala ya kufundishwa kuitumia,au anafundishwa sehemu za jani la mmea badala ya kumfundisha mimea tiba aione kwa macho,au unamwambia ajieleze jinsi anavyoweza kumhudumia mgomjwa badala ya kumpima akimhudumia mgonjwa.
Unakuta chuo kina darasa la wanafunzi 500 ila hakuna walimu wa kutosha na hata sehemu za mafunzo kwa vitendo hazitoshi( chuo hakina hospitali)
Sasa uhuni huu ambao serikali iliruhusu,umewafanya wamiliki wanogewe kupata mihela ya bure,huku wao wakifanya kila namna halali na haramu kufaulisha wanafunzi.
Ukweli sio serikali hasa bali baadhi ya watumishi wala rushwa wa nactvet wanaoruhusu hujuma hii ya kudahili wanafunzi wengi zaidi ya 500 kwa darasa moja,huku wao wakineemeka bila kujali madhila yanayolikumba taifa.

Baraza linapaswa kudhibiti usajili wa watu wasio na sifa.Na hawa wapo hadi ngazi ya shahada ya kwanza.Kuna vyuo vinaongoza kwa hizi hujuma.Ukiuliza kwani wadhibiti hawaoni haya?unaambiwa eti rais fulani ana hisa humo.Kumbe huenda hata ni uongo tu.
 
Sijakuelewa kabisa mkuu....vipunguzwe mpaka wapi....alama ya F? Kwa maana nyingine kigezo kibaki kuwa kumaliza form 4 tu regardless ya performance ya level hiyo???
 
Tatizo wasomi wengi wa kitanzania hawatumii akili zao vizuri.Unaweza ukashangaa sana watu wameshupaa na vigezo kupandishwa lakini hawajali mchakato wa kuwatengeneza hawa wataalamu.
Huku kwenye mchakato ndiko kuna utusitusi mwingi sana.
Aina ya mitaala,malengo yake,upimaji wake na hatimaye zao la mchakato wote.
Mtu anaandaliwa kukariri sehemu za mitambo ya kutengeneza dawa kwa njia ya picha badala ya kufundishwa kuitumia,au anafundishwa sehemu za jani la mmea badala ya kumfundisha mimea tiba aione kwa macho,au unamwambia ajieleze jinsi anavyoweza kumhudumia mgomjwa badala ya kumpima akimhudumia mgonjwa.
Unakuta chuo kina darasa la wanafunzi 500 ila hakuna walimu wa kutosha na hata sehemu za mafunzo kwa vitendo hazitoshi( chuo hakina hospitali)
Sasa uhuni huu ambao serikali iliruhusu,umewafanya wamiliki wanogewe kupata mihela ya bure,huku wao wakifanya kila namna halali na haramu kufaulisha wanafunzi.
Ukweli sio serikali hasa bali baadhi ya watumishi wala rushwa wa nactvet wanaoruhusu hujuma hii ya kudahili wanafunzi wengi zaidi ya 500 kwa darasa moja,huku wao wakineemeka bila kujali madhila yanayolikumba taifa.

Baraza linapaswa kudhibiti usajili wa watu wasio na sifa.Na hawa wapo hadi ngazi ya shahada ya kwanza.Kuna vyuo vinaongoza kwa hizi hujuma.Ukiuliza kwani wadhibiti hawaoni haya?unaambiwa eti rais fulani ana hisa humo.Kumbe huenda hata ni uongo tu.
Neno zito mkuu....ukweli mchungu huu.....
 
Umeongea vizuri sana...ahsante....kwa mfano huohuo wa chujio ukifuatilia matokeo ya mitihani ya leseni ya Baraza la Famasi ndio utaona chujio linavyofanya kazi......mpaka unajiuliza huko vyuoni kulikoni.....inawezekanaje mtu anafaulu mitihani ya chuo na anafeli vibaya mitihani ya leseni???? Na ukifuatilia kwa ukaribu sababu utakuta ni hizo...hesabu, english n.k....fuatilia masomo wanayofeli zaidi utagundua kitu......ndio maana nakubali bila shaka ufaulu kwenye masomo ya hesabu na Kiingereza ni muhimu sana sana.....na ufaulu wenyewe ni alama ya D.......wa chini kabisa.....yaani sielewi mwanafunzi mwenye F ya hesabu na kiingereza anakubaliwaje kusoma kozi ya CO, Nursing au ufamasia......
Kitu unasahau ni kuwa matokeo ya form four yanaakisi mafunzo ya NTA4 tu. Mtihani wa Wanafunzi wa vyuo vya Afya hutungwa na Wizara. Hapo utalaumu vyuo au waliotunga mtihani.
Kama inaonekana kuna tatizo la English na Mathematics, kwanini kusiwe na prerequisite module specific ili kusaidia hao wanafunzi. Unamfahamu tofauti ya CBET na KBET katika mafunzo. Mhitimu wa CBET anapimwa kwa Vitendo! Kupandisha vigezo si haki kwa Wanafunzi. Ni mtindo wa wanataaluma wa afya kujenga madaraja wakati wao wakiwa ng’ambo na kuyaondoa wakiwa ng’ambo ya pili. Mtimanyongo
 
Na Mwandishi Wetu

Jopo la Mawakili kumi na nne (14), wataalamu wa takwimu nane (8) na wataalamu wa mitaala watatu (3) kutoka katika kampuni za ushauri elekezi na uwakili zinapanga kuiburuza Serikali Mahakamani kutokana na uamuzi ya wizara ya afya kupitia kurugenzi yake ya mafunzo na rasilimali watu, na mabaraza yake ya taaluma (proffessional bodies) kubadili mitaala yake ya kufundishia kozi za afya bila kufuata utaratibu na kanuni zilizoainishwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET).

Katika nakala ya maelezo ya kesi ambayo chanzo chetu kimeweza kuiona, walalamikaji kupitia kwa jopo la mawakili wao, na wataalamu wanailalamikia Serikali kwa kitendo chake cha kushindwa kuzingatia kanuni na taratibu za uandaaji/upitiaji wa mitaala, na hivyo kusababisha kero kubwa kwa wananchi na wadau wa elimu ya mafunzo ya afya.

Fauzia Mashaka Kundecha na wenzake 120 katika kesi hiyo wanawashtaki Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya (mshtakiwa wa kwanza), Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) (mshitakiwa wa pili) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (mshtakiwa wa tatu).
Wawasilishaji wa maombi hayo ni wadau wanaotoa mafunzo kwa kada za afya ngazi ya kati kutoka katika zaidi ya Vyuo 170.

Hatua hiyo inafuatia mgogoro wa muda mrefu kati yake na Wizara ya Afya kuhusu kukiukwa kwa taratibu na kanuni za maandalizi ya mitaala na hivyo kuathiri hali ya utoaji wa mafunzo Nchini Tanzania.
Katika hatua ya awali walalamikaji watawasilisha notisi ya siku 90 kwa Serikali wakiitarifu kuhusu nia yao ya kutaka Mahakama iingilie kati suala la matumizi ya mitaala inayokinzana na taratibu na miongozo.

Kiongozi wa jopo la mawakili hao anayewawakilisha walalamikaji katika kesi hiyo ambaye ameiambia chanzo chetu cha habari kwamba nia ya kuishtaki Serikali imetokana na juhudi za kulitatua suala hilo kwa njia ya majadiliano kushindwa kuzaa matunda kwa takribani miaka sita (6).
“Hatua hii ni muhimu sana kwani utekelezaji wa mitaala hii unakwenda kuwazuia takribani watoto 15,000 wenye vigezo na sifa kutoka shule za kata kudahiliwa katika vyuo vya afya Nchini ,” Kiongozi wa jopo la mawakili alibainisha wakati wa mahojiano.

“Wadau mbalimbali wakiwemo Vyuo vya Afya, NACTVET, Wanafunzi waliohitimu kidato cha nne na wazazi walikuwa wamepanga kwamba kufikia katikati ya Mei 2024 wawe wameanza taratibu za udahili ,” aliongeza Wakili huyo.

“Pia, zoezi la mabadiliko ya mitaala na upandishwaji wa vigezo vya udahili linakusudiwa kutekelezwa katika kipindi ambacho wadau wamekwishajiandaa na zoezi la udahili na hakuna kozi mbadala ya afya ambayo Watoto hawa wanaweza kusoma kwa sasa,” Wakili alisema”. “Kitendo hiki kinawafanya wahitimu wa kidato cha nne kushindwa kudahiliwa katika kozi za afya.”

Alipoulizwa kama anafahamu chochote kuhusiana na mpango huo wa wadau wa vyuo vya afya kuishitaki Serikali, Mtumishi mmoja wa Wizara ya Afya ambaye hakutaka jina lake kutajwa alikiri kufahamu mpango huo, japo alidai kwamba wadau hao wamepewa fursa ya kujadiliana na Wizara ili kumaliza jambo hili. Mtumishi huyo alikiri kutambua kwamba malalamiko ya wadau hao yana mantiki kwa kuwa tathmini ya hali ya mahitaji ( situational analysis report) ilivyofanywa na timu ya wataalamu iliyoundwa na baraza la famasia na kutumia zaidi ya Tsh. 450,000,000 ilishindwa kubainisha sababu ya kubadili vigezo vya udahili kwa kada hiyo. Aidha chanzo hicho kilieleza kwamba wataalamu hao walizunguka nchi nzima na kuhoji watu 79 pekee ambapo wakufunzi walikuwa 15 na wahitimu (graduates) 15 idadi ambayo haiwezi kutoa matokeo jumuishi. Taarifa ya wataalamu pia ilibaini kwamba Mbinu iliyotumika katika kuchagua washiriki, idadi ya washiriki na kukusanya maoni ina wigo finyu wa kutoa matokeo jumuishi na ya kuaminiwa kupelekea kubadili maudhui na/au vigezo vya udahili katika mtaala, Ushirikishwaji hafifu au kutokushirikishwa kabisa kwa wadau muhimu kama wanafunzi, Kukosekana kwa sifa ya kuwa na mafunzo ya kufundisha mtaala wa umahiri ( CBET training) na usajili wa mabaraza (proffessional licences) kwa wakufunzi kumi na tano (15) waliotoa maoni, Kutumia neno “low quality students” kama kielekezo cha wanafunzi dhaifu wasioweza kumudu masomo yao, bila kufanya rejea ya mwenendo wa ufaulu wa wanafunzi hao kwa mitihani ya mwisho wa muhula na kushindwa kuonesha mahusiano thabiti ya mahitaji ya kubadili vigezo vya udahili na ongezeko ya somo la hisabati, fizikia na kiingereza.

Mvutano wa muda mrefu
Chimbuko la mgogoro wa mitaala na vigezo vya udahili lilianza mwaka 2018,mgogoro ulitokana na maamuzi ya Baraza la Uuguzi kupandisha vigezo vya masomo ya kujiunga kwa matokeo ya kidato cha nne kutoka Physics D kuwa C, Chemistry D kuwa C, Biology kutoka D kuwa C. Sababu za kupanda kwa vigezo hivyo hazikuanishwa bali ilionekana ni maamuzi bila utafiti wowote kwani ufaulu wa wanafunzi wa kozi hiyo katika mitihani ya mwisho ya masomo (Wizara) haukuwahi kuwa mbaya (Rejea kiambatanisho cha matokeo ya wahitimu wa kozi ya Ukunga na Uuguzi wa miaka tano mfululizo kwa vigezo vya awali). Hivyo kiliitishwa kikao cha wadau na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Jinsia Wazee na Watoto kikihusisha wawakilishi wa mabaraza, wamiliki wa vyuo vya binafsi, Wawakilishi wa Wakuu wa vyuo vya serikali na Chama Cha Wauguzi. Kufuatia majadiliano ya kikao kile ilionekana kuongeza vigezo hakukuwa na msingi wowote kitaaluma na kimahitaji hivyo vigezo vya awali viliendelea kutumika.

Mgogoro huu uliibuka tena mwaka 2021 sasa ukihusisha kozi ya Famasia. Kufuatia utengenezaji wa mtaala mpya ambao haukuhusisha wadau na hasa vyuo vya Afya. Vigezo vilipandishwa kutoka ufahulu wa kidato cha nne wa alama D (pass) wa masomo ya Chemistry, Biology na masomo mengine mawili yasiyo ya dini na kuwa ufaulu (pass) wa masomo ya Physics, Chemistry, Biology, Mathematics na English.
Mapema mwaka 2022 kufuatia vigezo hivi wadau walikutana na Mh. Naibu Waziri Afya na timu ya Wizara na baadae Mh. Waziri wa Afya. Kufuatia vikao hivyo Mheshimiwa Waziri aliagiza kuitishwa kikao cha wadau ili kujadili mtaala huu na vigezo hivyo vipya kabla ya utekelezaji wake. Kwa hatua ya majadiliano ilikofikia tulisubiria wito wa kikao cha wadau kama ilivyoagizwa na Mheshimiwa Waziri Mei 2022.

Mgogoro umeibuka upya sasa mwezi mei 2024 kufuatia kupandisha kwa vigezo katika fani za Ukunga na Uuguzi,Maabara,Famasia,Mazingira,Tiba ya Mazoezi ya viungo na Usimamizi wa Nyaraka za Afya (Health Records) kama inavyoonekana kwenye Kitabu cha Mwongozo wa Udahili cha Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) toleo la 2024/2025. Katika hatua hii upandaji wa vigezo umekuwa na tabia mtambuka,mabadiliko.mengine yakifanyika kwa mitaala hiyohiyo iliyopo na mabadiliko mengine yakionekana kuendana na mabadiliko ya mtaala. Kwa hatua hii ya ukuaji wa mgogoro huu ipo haja ya mjadala mpana kuhusu mtiririko wa mabadiliko yanayotokea,utaratibu,uhusishwaji wa wadau na utekelezaji wa maamuzi ya pamoja.

Mnamo Mei 04, 2024, Waziri wa Afya Ummy A. Mwalimu aliwakutanisha tena wadau hawa na Watendaji wa Wizara yake ambapo alisitisha utekelezaji wa mitaala hiyo na vigezo vya udahili na kuwataka kujadiliana ili kufikia muafaka, kikao ambacho kinatarajia kufanyika muda wowote kuanzia sasa.

Ombi la dharura
Hatua ya kuishitaki Serikali inaweza kufuata baada ya mikakati ya awali iliyochukuliwa na wadau hao kujikwamua na usumbufu huo kuchukua muda mrefu kutoa matokeo yaliyotarajiwa.
Wakili kiongozi anayewawakilisha wadau hao, alisema notisi ya kufungua kesi hiyo inaweza kuwasilishwa Mahakama Kuu Tanzania, Dodoma muda wowote kuanzia wiki ijayo.​
Naipongeza Serikali kupandisha Alama tena ikiwezekana Waweke "B" kabisa kwenyr masomo ya Physics, Biology na Chemistry halafu hayo mengine waweke "C"..

Tumekuwa na wimbi la watumishi wa afya Waliofeli makazini huku wakijisifu kufeli kwao ns kuingia Kusomea CO au Nursing sasa Naipongeza Wizara ya Afya Tanzania na napongeza Juhudi zao hizo..

Ili tupate Cream Inayostahili Huwezi kutegemea Kuja Kutibu Mgonjwa wakati alama zKo zenyewe za Mitihani zinahitaji kutibiwa..

Hao walioenda kushtaki wanajisumbua Bure tu
 
Ufaulu mzuri wa English, Hesabu, Biology na hayo mengine kwa ajili ya udahili wa kozi ya afya ni muhimu kwa kweli....yanayofanyika kwenye baadhi ya vyuo ili wanafunzi wafaulu ni ya aibu....hizi kozi si kwa ajili ya kila mtu....tuwaache wenye sifa wadahiliwe.....
Very good umeongea point
 
Na Mwandishi Wetu

Jopo la Mawakili kumi na nne (14), wataalamu wa takwimu nane (8) na wataalamu wa mitaala watatu (3) kutoka katika kampuni za ushauri elekezi na uwakili zinapanga kuiburuza Serikali Mahakamani kutokana na uamuzi ya wizara ya afya kupitia kurugenzi yake ya mafunzo na rasilimali watu, na mabaraza yake ya taaluma (proffessional bodies) kubadili mitaala yake ya kufundishia kozi za afya bila kufuata utaratibu na kanuni zilizoainishwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET).

Katika nakala ya maelezo ya kesi ambayo chanzo chetu kimeweza kuiona, walalamikaji kupitia kwa jopo la mawakili wao, na wataalamu wanailalamikia Serikali kwa kitendo chake cha kushindwa kuzingatia kanuni na taratibu za uandaaji/upitiaji wa mitaala, na hivyo kusababisha kero kubwa kwa wananchi na wadau wa elimu ya mafunzo ya afya.

Fauzia Mashaka Kundecha na wenzake 120 katika kesi hiyo wanawashtaki Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya (mshtakiwa wa kwanza), Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) (mshitakiwa wa pili) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (mshtakiwa wa tatu).
Wawasilishaji wa maombi hayo ni wadau wanaotoa mafunzo kwa kada za afya ngazi ya kati kutoka katika zaidi ya Vyuo 170.

Hatua hiyo inafuatia mgogoro wa muda mrefu kati yake na Wizara ya Afya kuhusu kukiukwa kwa taratibu na kanuni za maandalizi ya mitaala na hivyo kuathiri hali ya utoaji wa mafunzo Nchini Tanzania.
Katika hatua ya awali walalamikaji watawasilisha notisi ya siku 90 kwa Serikali wakiitarifu kuhusu nia yao ya kutaka Mahakama iingilie kati suala la matumizi ya mitaala inayokinzana na taratibu na miongozo.

Kiongozi wa jopo la mawakili hao anayewawakilisha walalamikaji katika kesi hiyo ambaye ameiambia chanzo chetu cha habari kwamba nia ya kuishtaki Serikali imetokana na juhudi za kulitatua suala hilo kwa njia ya majadiliano kushindwa kuzaa matunda kwa takribani miaka sita (6).
“Hatua hii ni muhimu sana kwani utekelezaji wa mitaala hii unakwenda kuwazuia takribani watoto 15,000 wenye vigezo na sifa kutoka shule za kata kudahiliwa katika vyuo vya afya Nchini ,” Kiongozi wa jopo la mawakili alibainisha wakati wa mahojiano.

“Wadau mbalimbali wakiwemo Vyuo vya Afya, NACTVET, Wanafunzi waliohitimu kidato cha nne na wazazi walikuwa wamepanga kwamba kufikia katikati ya Mei 2024 wawe wameanza taratibu za udahili ,” aliongeza Wakili huyo.

“Pia, zoezi la mabadiliko ya mitaala na upandishwaji wa vigezo vya udahili linakusudiwa kutekelezwa katika kipindi ambacho wadau wamekwishajiandaa na zoezi la udahili na hakuna kozi mbadala ya afya ambayo Watoto hawa wanaweza kusoma kwa sasa,” Wakili alisema”. “Kitendo hiki kinawafanya wahitimu wa kidato cha nne kushindwa kudahiliwa katika kozi za afya.”

Alipoulizwa kama anafahamu chochote kuhusiana na mpango huo wa wadau wa vyuo vya afya kuishitaki Serikali, Mtumishi mmoja wa Wizara ya Afya ambaye hakutaka jina lake kutajwa alikiri kufahamu mpango huo, japo alidai kwamba wadau hao wamepewa fursa ya kujadiliana na Wizara ili kumaliza jambo hili. Mtumishi huyo alikiri kutambua kwamba malalamiko ya wadau hao yana mantiki kwa kuwa tathmini ya hali ya mahitaji ( situational analysis report) ilivyofanywa na timu ya wataalamu iliyoundwa na baraza la famasia na kutumia zaidi ya Tsh. 450,000,000 ilishindwa kubainisha sababu ya kubadili vigezo vya udahili kwa kada hiyo. Aidha chanzo hicho kilieleza kwamba wataalamu hao walizunguka nchi nzima na kuhoji watu 79 pekee ambapo wakufunzi walikuwa 15 na wahitimu (graduates) 15 idadi ambayo haiwezi kutoa matokeo jumuishi. Taarifa ya wataalamu pia ilibaini kwamba Mbinu iliyotumika katika kuchagua washiriki, idadi ya washiriki na kukusanya maoni ina wigo finyu wa kutoa matokeo jumuishi na ya kuaminiwa kupelekea kubadili maudhui na/au vigezo vya udahili katika mtaala, Ushirikishwaji hafifu au kutokushirikishwa kabisa kwa wadau muhimu kama wanafunzi, Kukosekana kwa sifa ya kuwa na mafunzo ya kufundisha mtaala wa umahiri ( CBET training) na usajili wa mabaraza (proffessional licences) kwa wakufunzi kumi na tano (15) waliotoa maoni, Kutumia neno “low quality students” kama kielekezo cha wanafunzi dhaifu wasioweza kumudu masomo yao, bila kufanya rejea ya mwenendo wa ufaulu wa wanafunzi hao kwa mitihani ya mwisho wa muhula na kushindwa kuonesha mahusiano thabiti ya mahitaji ya kubadili vigezo vya udahili na ongezeko ya somo la hisabati, fizikia na kiingereza.

Mvutano wa muda mrefu
Chimbuko la mgogoro wa mitaala na vigezo vya udahili lilianza mwaka 2018,mgogoro ulitokana na maamuzi ya Baraza la Uuguzi kupandisha vigezo vya masomo ya kujiunga kwa matokeo ya kidato cha nne kutoka Physics D kuwa C, Chemistry D kuwa C, Biology kutoka D kuwa C. Sababu za kupanda kwa vigezo hivyo hazikuanishwa bali ilionekana ni maamuzi bila utafiti wowote kwani ufaulu wa wanafunzi wa kozi hiyo katika mitihani ya mwisho ya masomo (Wizara) haukuwahi kuwa mbaya (Rejea kiambatanisho cha matokeo ya wahitimu wa kozi ya Ukunga na Uuguzi wa miaka tano mfululizo kwa vigezo vya awali). Hivyo kiliitishwa kikao cha wadau na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Jinsia Wazee na Watoto kikihusisha wawakilishi wa mabaraza, wamiliki wa vyuo vya binafsi, Wawakilishi wa Wakuu wa vyuo vya serikali na Chama Cha Wauguzi. Kufuatia majadiliano ya kikao kile ilionekana kuongeza vigezo hakukuwa na msingi wowote kitaaluma na kimahitaji hivyo vigezo vya awali viliendelea kutumika.

Mgogoro huu uliibuka tena mwaka 2021 sasa ukihusisha kozi ya Famasia. Kufuatia utengenezaji wa mtaala mpya ambao haukuhusisha wadau na hasa vyuo vya Afya. Vigezo vilipandishwa kutoka ufahulu wa kidato cha nne wa alama D (pass) wa masomo ya Chemistry, Biology na masomo mengine mawili yasiyo ya dini na kuwa ufaulu (pass) wa masomo ya Physics, Chemistry, Biology, Mathematics na English.
Mapema mwaka 2022 kufuatia vigezo hivi wadau walikutana na Mh. Naibu Waziri Afya na timu ya Wizara na baadae Mh. Waziri wa Afya. Kufuatia vikao hivyo Mheshimiwa Waziri aliagiza kuitishwa kikao cha wadau ili kujadili mtaala huu na vigezo hivyo vipya kabla ya utekelezaji wake. Kwa hatua ya majadiliano ilikofikia tulisubiria wito wa kikao cha wadau kama ilivyoagizwa na Mheshimiwa Waziri Mei 2022.

Mgogoro umeibuka upya sasa mwezi mei 2024 kufuatia kupandisha kwa vigezo katika fani za Ukunga na Uuguzi,Maabara,Famasia,Mazingira,Tiba ya Mazoezi ya viungo na Usimamizi wa Nyaraka za Afya (Health Records) kama inavyoonekana kwenye Kitabu cha Mwongozo wa Udahili cha Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) toleo la 2024/2025. Katika hatua hii upandaji wa vigezo umekuwa na tabia mtambuka,mabadiliko.mengine yakifanyika kwa mitaala hiyohiyo iliyopo na mabadiliko mengine yakionekana kuendana na mabadiliko ya mtaala. Kwa hatua hii ya ukuaji wa mgogoro huu ipo haja ya mjadala mpana kuhusu mtiririko wa mabadiliko yanayotokea,utaratibu,uhusishwaji wa wadau na utekelezaji wa maamuzi ya pamoja.

Mnamo Mei 04, 2024, Waziri wa Afya Ummy A. Mwalimu aliwakutanisha tena wadau hawa na Watendaji wa Wizara yake ambapo alisitisha utekelezaji wa mitaala hiyo na vigezo vya udahili na kuwataka kujadiliana ili kufikia muafaka, kikao ambacho kinatarajia kufanyika muda wowote kuanzia sasa.

Ombi la dharura
Hatua ya kuishitaki Serikali inaweza kufuata baada ya mikakati ya awali iliyochukuliwa na wadau hao kujikwamua na usumbufu huo kuchukua muda mrefu kutoa matokeo yaliyotarajiwa.
Wakili kiongozi anayewawakilisha wadau hao, alisema notisi ya kufungua kesi hiyo inaweza kuwasilishwa Mahakama Kuu Tanzania, Dodoma muda wowote kuanzia wiki ijayo.​

Hii tume ilikuwa ya Wafamasia tupu kwanini hakuna wawakilishi kutoka fani zingine? Na walizunguka Tanzania muzima na kuhoji watu 79 tu kwa Tsh mil 450? Kweni tume ilikuwa ya watu wangapi ili tufanye mahesabu kabla ya CAG hajaja...I smell a rat!
 
Kwa maoni yangu nikiwa muumini mzuri wa "meritocracy" naona elimu inachezewa hasa na hao wamiliki wa vyuo ambao wametanguliza maslahi yao binafsi tu!

Leo hii mwanafunzi anaendaje kusoma pharmacy katika ngazi ya diploma bila kigezo cha ufaulu wa hesabu wala fizikia?

Hesabu za kukotoa dose, isotonicity , compunding preparations , na kadhalika atazifanya kwa ufanisi au ni kubahatisha?

Niliwahi kupitia kiongozi cha mwalimu "facilitator guide" cha kozi ya pharmacy NTA level 4 &5&6 ni mambo ya kushangaza sana na ndio maana sikushangaa matokeo yanapotoka ufaulu huwa ni duni kama yale ya mwezi October ambapo ufaulu ulikuwa asilimia 23 tu !

Wamiliki wa vyuo wakae na kufahamu hilo bomu wanalolitengeza litawalipukia mbeleni kwani wazazi, ndugu, jamaa na marafiki zao wataenda kutibiwa hospitali hizo hizo walipo hao wenye uwezo duni.

Mfano mdogo tu kuna chuo pale Morogoro mwanafunzi alitoa topical medication(dawa ya kupaka kwenye ngozi) kwa mgonjwa akimpa maelekezo kuwa dawa hiyo itumike kwa kunywa (oral route) hali iliyoleta shida kubwa na baraza lilitoa tamko tu ila hakuna ripoti au hatua zilizowahi kuchukuliwa kwa chuo hicho wala kuangalia uendeshaji mafunzo chuoni hapo pengine chuo pia hakikuwa na walimu waliokidhi vigezo au lah?

Kwa mwanafunzi aliyesoma route of administration na pharmacology juu hawezi kutoa maelekezo sahihi je tusione hapo kuna shida??

Tujifunze kwa wenzetu leo hii US huwezi kuingia tu kwenda kusoma Doctor of Medicine (M.D ) au kozi zingine bila kuwa na shahada nyingine ihusuyo afya kama Biochemistry na kadhalika.

Hii ni kiashiria licha ya kuwa na kigezo ila unyeti wa kozi fulani unapaswa upewee kipaumbele hasa afya maana bila afya hakuna maisha.

AQN-1.png
 
Hii tume ilikuwa ya Wafamasia tupu kwanini hakuna wawakilishi kutoka fani zingine? Na walizunguka Tanzania muzima na kuhoji watu 79 tu kwa Tsh mil 450? Kweni tume ilikuwa ya watu wangapi ili tufanye mahesabu kabla ya CAG hajaja...I smell a rat!
Kwa maelezo niliyoyapata ni kuwa kozi zingine za afya zilibadili vigezo kabla na kwa vigezo hivyo ilipelekea kozi hizo kuwa na wanafunzi wachache.

Kozi pekee iliyokuwa imebaki na vigezo vya "chini" ambazo ni alama D 2 ilibaki ni pharmacy pekeyake hivyo kozi hii ndio ilijikuta ina wanafunzi wengi ambao ni "mtaji " kwa vyuo hivyo.

Sasa mtaala uko tayari tangu 2022 na huku kozi zingine wakiwa wamebadili mtaala tangu 2021 kasoro pharmacy tu maana mtaala wa mwanzo ulikwisha muda wake 2021 sababu ulipangwa utumike (2016-2021)

Sasa chini ya mtaala mpya lazima vigezo viongezeke maana kuna maboresho mengi tu ila hapo ndio kuna mgongano wa kimaslahi kati ya vyuo kadhaa hasa wamiliki na baraza ambalo linasimamia taaluma.

Ukweli ni kuwa vyuo vina wanafunzi wengi wa pharmacy katika kozi zote za afya sababu ya vigezo vya chini na licha ya kuwa na wanafunzi wengi bado vyuo vina ujanja ujanja mfano nyenzo za kujifunzia, mahali pa kusomea, maabara hazijitoshelezi , mchakato mzima wa ufanyaji mitihani ya ndani una dosari kubwa .

Haya yote sio rahisi kuyajua kama huna taarifa halisi kwa wanaoangalia taifa kwa maslahi mapana na sio katika mizania ya kibiashara.
 
Hizi ndio akili za watanzania sasa unaishitaki vipi serikali yenye mamlaka ya kusimamia ubora wa huduma za afya, kutunga sera, sheria na regulations.

Proffesional bodies ndio washauri wakuu wa serikali kwenye maswala ya quality na zinashirikiana na serikali kutunga kanuni na waajiriwa wa afya wanakuwa chini yao na kutekeleza majukumu yao kwa kufuata miongozo yao.

Wao ndio wanafanya quality assessment ya huduma na watoa huduma na kuweka viwango vya standards.

Sasa how on earth unaweza ishitaki serikali inapofanya maamuzi yake, kwanza sidhani kama kozi za afya zinatakiwa kutolewa na vyuo vya hovyo.

Hili ndio tatizo kubwa la watanzania watu awapendi mabadiliko, nchi zingine taasisi zikikutana na changamoto mabadiliko wana adapt haraka na mazingira mapya vinginevyo unapotea. Tanzania ni kinyume sasa PEST analysis ya nini kama watu awategemei mabadiliko ya ghafla.

Wazimu zaidi ni hizi mahakama zetu, yaani unapoteza muda wa mahakama kuifungulia serikali yenye mandate ya kupanga sera na kutunga sheria hata kesho na wakisema inaanza mwezi ujao kila mtu inaemgusa anatakiwa afuate hizo ni powers zao kikatiba.

Waste of court time na malalamiko yaliyojaa upuuzi mtupu.
 
Kwanza hivyo vyuo vinatakiwa vikakaguliwe ubora wa elimu inayotoa.

Haiwezekani taasisi ya kutoa elimu isielewe nani anajukumu la kuweka viwango vya ubora wa elimu wanayotoa, god know quality ya elimu.

Ndio madhara ya kutoa vibali vya kiholela vya watu kujifungulia vyuo hovyo, wenye vyuo wengine awaelewi hata role ya serikali katika shughuli zao.

The whole thing is pathetic, unaishitaki serikali kwa kuweka new bench mark, huu wazimu unawezekana Tanzania tu.
 
Back
Top Bottom