Serikali Kuendelea Kufanya Tathmini ya Maeneo Yaliyopata Athari za Mafuriko

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

SERIKALI KUENDELEA KUFANYA TATHMINI YA KINA KATIKA MAENEO YALIYOPATA ATHARI ZA MAFURIKO

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis akijibu maswali bungeni amesema Serikali kuendelea kufanya tathmini katika maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko.

Serikali imewataka wananchi wasijenge mabondeni ambayo huathiri maisha yao. Hayo yamesemwa bungeni Mei 08, 023 na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis wakati akijibu swali la Mbunge wa Mwera Mhe. Zahor Mohamed Haji.

Katika kudhibiti kutokea kwa mafuriko katika maeneo ya Magharibi A yakiwemo maeneo ya Jimbo la Mwera hatua zilichukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

"Kuunda Kamati ya kukabiliana na Maafa Wilaya ya Magharibi A yenye jukumu la kuratibu utekelezaji wa Mpango wa Wilaya wa kukabiliana na Maafa ya mwaka 2022 sambamba na kuwaelimisha wananchi lakini pia kuandaa mpango wa Wilaya wa kukabiliana na Maafa ambao umeainisha wadau, majukumu yao na mpango wa Utekelezaji" - Mhe. Khamis Hamza Khamis

"Aidha, katika mwaka wa fedha 2023/2024 Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais itaendelea kufanya tathmini ya kina katika maeneo yote yanayokumbwa na mafuriko nchini ikiwemo maeneo ya Jimbo la Mwera" - Mhe. Khamis Hamza Khamis
 

Attachments

  • FvoLjeHWYA8nAWY.jpg
    48.8 KB · Views: 3
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…