Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Vijana Taifa, Mhe. Amina Ali Mzee; Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Daniel Sillo amesema Serikali iko hatua za mwishoni kuleta Muswada wa Sheria Bungeni ili ifanyiwe marekebisho kwa lengo la kukabiliana na ajali za Barabarani zinazosababishwa na Madereva wazembe.
"Je, lini Serikali itaanza kuweka Sheria na Utaratibu mzuri wa kupunguza ajali za barabarani zinazotokana na uzembe wa Madereva" - Mhe. Amina Ali Mzee, Mbunge wa Viti Maalum Vijana Taifa
"Jeshi la Polisi kupitia kikosi cha Usalama Barabarani kwasasa kinasimamia masuala ya Usalama Barabarani kwa kutumia Sheria ya Usalama Barabarani Sura 168 ya mwaka 1973 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002 katika mkakati wa Kuboresha Sheria hii ili kupunguza ajali za Barabarani, Serikali imekusanya maoni kutoka kwa wadau na sasa inamalizia kuyafanyia kazi na baada ya hapo itawasilisha Muswada wa Sheria Bungeni" - Mhe. Daniel Sillo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
"Je, ni hatua zipi zinazochukuliwa na Serikali kuwadhibiti Madereva wazembe? Serikali haioni sasa iko haja ya kuhakikisha Sheria hii inakuja Bungeni ili kudhibiti ajali za Barabarani?" - Mhe. Amina Ali Mzee, Mbunge wa Viti Maalum Vijana Taifa.
Soma Pia: Tatizo la Ajali za Barabarani Litatumaliza Watanzania, Je Kweli Serikali Haiwezi Kufanya Kitu?
"Hatua stahiki ya kwanza kwa Madereva wazembe ni kuwafutia leseni kwa Dereva anayeendesha gari kwa uzembe na kusababisha ajali. Pili, ni kumfikisha Mahakamani na ikithibitika ni kufungwa Jela . Tatu, ni kulipa faini"
"Dhamira ya Serikali ni kuhakikisha ajali za Barabarani ama zinapungua ama zinakwisha kabisa. Tumekusanya maoni kutoka kwa wadau mbalimbali, lengo ni kuhakikisha tunarekebisha Sheria"