Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,048
- 22,790
Katika kipindi cha miaka kumi iliyopita kumekuwapo tabia ya Serikali kufungia magazeti mbalimbali, ingawa katika kipindi kuanzia mwaka 2016 hadi 2020 kasi ya kufungia magazeti ilipanda sana.
Serikali inatumia sheria yake ya vyombo vya habari kufungia magazeti mbalimbali yanayovunja sheria hiyo.
Ningeshauri sana wadau mbalimbali waiwekee shinikizo Serikali iondoe adhabu hiyo ya kufungia vyombo vya habari.
Wanaweza kuweka utaratibu wa faini, au kifungo kwa mhariri mkuu bila kufunga chombo cha habari chenyewe kwa sababu vyombo hivyo hutoa ajira kwa watu wengi na mara vinapofungwa inakuwa ni adhabu siyo kwa gazeti tu bali hata familia ya za wafanyakazi wa chombo husikia.
Utaona kuwa habari zinazoeletea chombo cha habari kufungwa ni zile za kisiasa tu, ila vyombo hivyo pia hutoa habari za michezo, burudani na habari za jamii kwa jumla ambazo hazijawahi kukosolewa na serikali.
Kufungia vyombo vya habari ni sawa na kuchoma moto maghala yote ya chakula kijijini eti kwa sababu kiongozi wa kijiji alimslisha mtu chakula chenye sumu.