Serikali kufungia Magazeti

Serikali kufungia Magazeti

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Posts
17,048
Reaction score
22,790
Katika kipindi cha miaka kumi iliyopita kumekuwapo tabia ya Serikali kufungia magazeti mbalimbali, ingawa katika kipindi kuanzia mwaka 2016 hadi 2020 kasi ya kufungia magazeti ilipanda sana.

Serikali inatumia sheria yake ya vyombo vya habari kufungia magazeti mbalimbali yanayovunja sheria hiyo.

Ningeshauri sana wadau mbalimbali waiwekee shinikizo Serikali iondoe adhabu hiyo ya kufungia vyombo vya habari.

Wanaweza kuweka utaratibu wa faini, au kifungo kwa mhariri mkuu bila kufunga chombo cha habari chenyewe kwa sababu vyombo hivyo hutoa ajira kwa watu wengi na mara vinapofungwa inakuwa ni adhabu siyo kwa gazeti tu bali hata familia ya za wafanyakazi wa chombo husikia.

Utaona kuwa habari zinazoeletea chombo cha habari kufungwa ni zile za kisiasa tu, ila vyombo hivyo pia hutoa habari za michezo, burudani na habari za jamii kwa jumla ambazo hazijawahi kukosolewa na serikali.

Kufungia vyombo vya habari ni sawa na kuchoma moto maghala yote ya chakula kijijini eti kwa sababu kiongozi wa kijiji alimslisha mtu chakula chenye sumu.
 
Kichuguu,

Tabia hii ndio huwa tunaita kiburi cha madaraka, au matumizi mabaya ya madaraka.
 
Mwenyeshibe hajui ilo la kukosesha wenye njaa chakula. Bahati mbaya au nzuri ni kua jamii ya kiTanzania wamejaa ujinga hawajui kua viongozi walichaguliwa kuwatumikia.

Mhariri anafanya kosa alafu mpaka fundi wa kutengeneza printa anakosa kazi. Ujinga wa namna hii inapatikana Tanzania pekee tena chini ya utawala wa Rais wa Wanyonge.
 
Mwenyeshibe hajui ilo la kukosesha wenye njaa chakula. Bahati mbaya au nzuri ni kua jamii ya kiTanzania wamejaa ujinga hawajui kua viongozi walichaguliwa kuwatumikia.

Mhariri anafanya kosa alafu mpaka fundi wa kutengeneza printa anakosa kazi. Ujinga wa namna hii inapatikana Tanzania pekee tena chini ya utawala wa Rais wa Wanyonge.
 
Asante kwa wito huu na tuendelee kumpinga NDULI MAGU anatupeleka pabaya sana.
 
Tanzania daima gazeti la kusambaza uongo uzushi uzandiki wa chadema afadhali wangelifungia maisha tu japo wauza mihogo na mandazi watapata tabu ya vifungashio
 
Tz daima ni mwanzo tu kuelekea uchaguzi ili yafanye biashara ni lazima yawe na chapa 666,magazeti yote na tv zote zisizo na chapa ya 666 na zitakazoonyesha kampeni na mikutano ya wapinzani vyote vitafungiwa.Njia pekee ni kutumia mitandao.
 
Back
Top Bottom