Serikali kuilipa Symbion Tsh Billion 356

Mpinzire

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2013
Posts
7,503
Reaction score
13,463
Serikali Kupitia Wizara ya Nishati (Tanesco) kuilipa kampuni ya Symbion Tsh Billion 356 baada ya kuvunja mkataba wake na Tanesco awamu ya 5.

Kampuni ya Symbion ni Kampuni iliyokuwa ya Kimarekani ambayo ilikuwa ikifua umeme na kuiuzia Tanesco! Kampuni ya Symbion ilifunguliwa rasmi awamu ya 4 na Rais wa Marekani wakati huo Mh. Barack Obama pamoja Rais wa awamu ya 4 Mh Jakaya Kikwete.

Pia soma



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ama kweli ulegelege siutaki kwenye maisha yangu!!

JPM umenipa somo kubwa sana,

Ujasiri wako na uthubutu wako uliwogofya waizi wote wa ndani na nje ya nchi, hata wazungu waliufyata, ila sasa upepo unasomeka kirahisi, eti wezi waliokuwa wakituibia kwa mikataba ya kipumbavu na mezani kwa watia sain kumewekwa dollar za rushwa, na sasa tunawalipa tena waizi wetu!

Kwa nini hawakudai fidia enzi yako!!? Nimegundua, hata biblia imesema, waoga wote hawaustahili ufalume wa mbinguni, Bali wenye nguvu ndio watakaouteka

Na nchi yetu bila watu majasiri, maendeleo tutayasikia tuu!
 
Hapo watawala wameweka za kwao kama 100B
 
Mleta mada bana. Yani wee mwenyewe unaona iyo billion 356 ni nyiiingiiiiiiiiiiiiii.
 
Yaan wabongo bana πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ mzungu gan ataufyata kwa muafrika? Mzungu ambae unategemea hela za ili ukidhi mahitaj yako kwa zaid ya nusu? Misaada chungu nzima tunawategemea weupe. Udhamini wa kisiasa tunawategemea weupe, kibaya zaid bado tupo under surveillance yao kiutawala!!
 
Hichi kitu watu uwa hawajui, Bajeti zetu zote zinamtegemea mzungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…