Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
SERIKALI KUJENGA BARABARA YA MUSOMA-MAKOJO-BUSEKERA KWA AWAMU MBILI
(Bajeti ya Wizara ya Ujenzi & Uchukuzi, 2023/2024)
Urefu wa barabara Kilomita 92
Sehemu zenye lami Musoma Mjini-Buhare: km 5.9 (Eneo lote hili liko ndani ya Manispaa ya Mji wa Musoma)
Kusenyi-Kwikonero: km 5 (Eneo lote hili liko Musoma Vijijini)
BAJETI YA MWAKA 2023/2024; Barabara letu limepewa KM 40 (Kilomita Arobaini, Awamu I)
Wananchi na Viongozi wote wa Chama na Serikali wa Jimbo la Musoma Vijijini wanaishukuru sana SERIKALI yetu kufanya maamuzi mazuri ya kukamilisha ujenzi wa barabara hili (Musoma-Makojo-Busekera) kwa awamu mbili. Ahsante sana Rais wetu, Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kusikiliza kilio chetu cha miaka mingi na hatimae kuamua kutatatua tatizo hili sugu. Tunashukuru sana!
AWAMU I (40 km)
Ujenzi wa barabara hili ulishaanza kwa kujenga KILOMITA 5 kuanzia Kijiji cha Kusenyi kuelekea Kijiji cha Makojo hadi Kijijini Busekera (mwisho wa barabara)
Ujenzi wa km 40 uendelee kwa mpangillio huo huo, yaani, kuanzia Kitongoji cha Kwikonero (Kijiji cha Suguti) kuelekea Kijijini Busekera - tusiache vipande vipande!
AWAMU II (km 40+)
Ujenzi utaanzia Kijijini Kusenyi kuelekea Musoma Mjini
USHAURI:
Achukuliwe Mkandarasi mzoefu, na anayejitosheleza kwenye vifaa vya ujenzi
Ujenzi uanze haraka baada ya Bajeti ya Serikali ya Mwaka 2023/2024 kuanza kutumika, yaani tarehe 1.7.2023.
Usisahau kutembelea TOVUTI ya Jimbo letu ambayo ni:
www.musomavijijini.or.tz
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
Tarehe:
Jumanne, 23.5.2023