Kwenye nchi yoyote inayoongozwa kwa misingi ya kidemokrasia, wananchi ndio wenye sauti juu ya kumchagua kiongozi atakayeunda serikali na wawakilishi wao bungeni. CCM imekuwa ikiwahadaa wananchi kwa kupitia kivuli cha kudumaza elimu vijijini ambapo ndipo kuna high level of illiteracy kuendelea kujipatia kura za wizi kwa kisingizio cha kuwajaza kwa lazima kwenye mikutano yao na kuchukua picha ili kuihadaa dunia kuwa inapendwa sana alafu wanatoa maelekezo kwa wakurugenzi ambao wamewachagua wasimamizi wa chaguzi na mawakala kuingiza kura feki vituoni na kujitangaza wameshinda kwa kishindo.
Tanzania ya sasa sio ya miaka 2010 wala 2015 bali ni ya kizazi kipya kinachoongozwa na telnolojia. Mama Samia alisema kwenye press yake na wale wazee eti " Hamkuona mikutano yangu ilivyokuwa ikijaza watu?" Akifikiria kuwa atawahadaa watanzania na maneno yake ile siku. Ushahidi upo wa kuwa watu wachache sana walijitoke?a kupiga kura na kuna baadhi ya maeneo wananchi hawakwenda kabisa vituoni. Dunia nzima inashangaa hizo 97% of votes for her zilitokea wapi.