Nkobe
JF-Expert Member
- Feb 17, 2013
- 2,204
- 3,277
Wadau hii ni tetesi yenye ukweli 95%.
Ukweli ni kwamba baada ya serikali kupandisha kodi katika utalii, sasa hali ni mbaya Arusha ambao ndio mkoa wa kitalii zaidi Tanzania.
Kuna taarifa kuwa mnamo tarehe 20 mwezi huu Septemba serikali itakutana na wadau wa utalii kuangalia jinsi ya kurejesha hali ya utalii.
Kwa sasa makampuni mengi yamefungia magari ya kitalii ndani maana hali ni tete, watalii wacheche, vikampuni vidogo vidogo vinapumua kwa Oxygen.
MADHARA YA KAULI YA RAIS
Pia kutokana na ile kauli ya Rais kuwa hatutaki watalii wengi wasio na uwezo wa kulipa, kwamba bora tupate wachache wenye kulipa kodi imesababisha madhara makubwa kwa vijana kwa sababu watalii wakiwa wengi hata kama wanalipa hela kidogo inasaidia vijana wengi kuajiriwa katika sekta hiyo kwa kuwa watalii wakiwa wengi watahitaji Tour guides wengi, wabeba mizigo wengi (Porters), wapishi wengi nk. Tofauti na maoni ya Rais kuwa bora waje wachache wanaotoa pesa nyingi, kimsingi mtalii hata kama ana pesa nyingi lakini idadi ya wapishi, wabeba mizigo nk watabaki kuwa walewale tu, hivyo kusababisha watu wengi kupoteza kazi.
Kama kweli serikali itakaa na wadau wa utalii basi ni jambo jema.