Tunaweza fanikisha hata kwa wakati huu wa sasa. Siyo lazima tufanye sisi, kwenye comment yangu hiyo nimeshauri kwamba tunaweza kuwa na Viwanda hivyo hata kwa Kupitia Wawekezaji, ambao tayari Wana uwezo wa kujenga viwanda vya kuunda ndege.
Zitauzwa wapi?
Wasichojua wengi ni kuwa hizi kampuni kubwa za uundaji ndege (Boeing, Airbus) shughuli zao kubwa ni za biashara, masoko na fedha. Wana kampuni tanzu kubwa za maeneo hayo. Huko ndiko wanakokutana na wateja wa kila aina: wanaokopa, wanaokodi, wanaoazima, wanaodunduliza, wanaonunua kwa mali kauli na wachache wanaonunua kwa cash. Kazi kubwa ndiko inakofanyika. Wateja wa cash si wa kawaida na order zao ni ndogo; hazisumbui. Zinawasilishwa viwandani chap chap. Wateja wazito ndio mijadala inafanyika kwa undani ikihusisha namna mbalimbali (complex) za manunuzi ndipo order ziwasilishwe viwandani. Ndege hazinunuliwi kama V8. Hakuna showroom kiwandani wala kwenye matawi ya kampuni.
Kwa mfano, Ethiopian Airlines mwaka huu wameweka order ya Boeing 777X ishirini (20). Mwaka jana 2023 ET waliagiza Boeing 787-10 kumi na moja (11) na Boeing 737-Max ishirini (20). Wanachofanya ni kuandaa mpango wa biashara uliohakikiwa na kuuwasilisha kwenye kampuni ya biashara, masoko na fedha ya Boeing na kujadili mahitaji ya ndege, aina zake, namna ya manunuzi na ratiba ya upatikanaji. Pesa inayotolewa cash ni kidogo sana. Marejesho makubwa yanatarajiwa kutoka kwenye mtiririko wa mapato kibiashara. Boeing wana uzoefu wa miaka mingi ya biashara na ET. Hawana tatizo na marejesho yao kibiashara.
Sisi labda kama tunataka kuwa factory mojawapo ya Boeing, Airbus, Embraer n.k. Kitu ambacho si rahisi. Hizo kampuni zinaangalia hali ya nchi na mfumo wake mzima wa kiuchumi, kibiashara, kielimu, kiteknolojia, kisiasa, n.k. Siioni Tanzania hata kufikirika katika jambo kubwa hivi.
Tupambane kwanza kuondoa aibu ya kujengewa matundu ya vyoo kwa msaada wa watu wa Marekani.