Badala ya kuendelea kuwa na mawazo au fikra potofu kila wakati za kununua ndege mpya kutoka ktk viwanda vya nchi za nje, nadhani umefika wakati sasa wa kufikiria kuwa na kiwanda au viwanda vyetu weyewe vya kuunda ndege hapa hapa nchini kwetu Tanzania. Tuwe na wazo kama hili, hata kama sisi wenyewe bado akili zetu hazijawa kubwa kuweza kuwa na viwanda vya namna hii, basi tuanze hata kwa kuwakaribisha wawekezaji kutoka nje ya nchi, tunaweza kuingia nao mikataba maalumu ya uwekezaji wa namna hii. Viongozi wa nchi hii wawe na Maono Mapana ili wayaone haya mambo mazuri kwa mustakabali mwema wa nchi hii.