Serikali: Kuna Jumuiya za Kidini zinatumika kutakatisha pesa, usafirishaji haramu wa binadamu, kufadhili ugaidi na kutoa mafunzo hatarishi

Serikali: Kuna Jumuiya za Kidini zinatumika kutakatisha pesa, usafirishaji haramu wa binadamu, kufadhili ugaidi na kutoa mafunzo hatarishi

Kajali maslahi ya nchi na sio cheo.

Kwa hizi akili zako sio rahisi kuwa na watu wanaoipenda nchi kuliko vyeo na kazi zao.
Angeonekana yuko siliasi na masilahi ya nchi iwapo angedhibiti kwanza ng`o zinazo fadhili ushoga na utoaji mimba zilizo jaa hapa nchini.
 

Utitiri wa nyumba za ibada katika makazi zinasababisha makelele na pia hutumika kuwezesha utakasishaji fedha na ugaidi..

Pia waziri Hamad Masauni asema taasisi na jumuiya ya kidini baadhi yao zinajihusisha na matendo ya kijinai ikiwemo ...

UN- Umoja wa Mataifa imeiweka Tanzania ktk buku jeusi ili ifuatiliwe kwa ukaribu kutokana na kutokuwepo mifumo bora ya ufuatiliaji.
---

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamadi Masauni aesema kumekuwa na utitiri wa nyumba za ibada kwenye makazi ya watu ambazo zinageuka kuwa kero kutokana na kelele katika nyumba hizo. Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Machi 26, 2024 wakati wa kampeni za ufunguzi wa jumuiya.

Waziri Masauni amezungumzia pia juu ya uwapo wa Taasisi ambazo zinafadhili shughuli za ugaidi, usafirishaji haramu wa binadamu, silaha haramu na uwepo wa taasisi za kidini zinazotoa mafundisho potofu ambayo ni hatarishi kwa usalama wa raia. Akiongelea mambo haya katika shughuli hiyo Masauni amesema:

"Zimebainika changamoto za uzalishaji holela za utitiri wa nyumba za ibada katika maeneo mbalimbali hapa nchini. Baadhi ya Jumuiya za dini hususani makanisa na misikiti zimebainika kujengwa katikati ya makazi ya watu.

Kuna mrundikano wa taasisi nyingi katika eneo dogo na baadhi ya taasisi kutumia sauti za juu na hivyo kusababisha adha."

Vilevile baadhi ya Jumuiya za Kiraia zimeripotiwa kushiriki katika kutendeka makosa ya jinai na vitendo vingine ambavyo vina madhara kwa jamii. Baadhi ya vitendo hivyo ni pamoja na Utakatishaji wa Fedha haramu, ugaidi, usafirishaji haramu wa binadamu, biashara haramu ya silaha na uwepo wa taasisi za kidini zinazotoa mafundisho potofu ambayo yanahatarisha usalama wa raia.


Kama ambavyo nimeeleza changamoto za aina hii zinahitaji ushirikiano wa pamoja atika ushughulikiwaji wake ili kuendelea kudumisha hali ya utulivu na usalama.

Hivyo ikiwa kama viongozi mliopewa dhamana ni vyema mkatambua mna wajibu mkubwa wa kuendelea kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika kuondoa changamoto hizi kwenye jamii
Mbona kelele zimekuwepo sana, kwanza wapige marufuku kuhusu misikiti inayopiga kelele saa 10 usiku maana hao ndo hatari sana
 
Hili la kelele NEMC wanastahili lawama amaaa kufutwa kabisa
Kingekuwa kiwanda kinachafua ardhi na maji wangewahi mno Mana Kuna ulaji.
Ila Sasa hili la majumba ya ibada ,hawapo mbele na huku ndilo linalochafua potential resources ever aka mental peace and calm.
Body rest Hakuna ili kesho ikafanye kazi izalishe kwa manufaa ya Taifa.
Yaani ningewaona wajanja Kama wangejikita katika noise pollution. Kuna hili la ma bar kutopiga miziki kwa sauti za juu mwanza walipiga beat Naona wale jamaa walijiunga baadaye Naona wanaendelea kupiga makelele.
Lindeni mental, physical and spiritual za watu.
 
Kuna taasisi hazifanyi kazi vizuri,makanisa hta USA yapo ya ajabu lakini jambo muhimu ni idara za usalamu kufanya kazi vyema
 
Katangaza Tanzania Kuna ugaidi hadharani kabisa!!

Maana yake Nini!!?serikali ya awamu hii imeshindwa kazi!!?isaidiwe na jeshi kupambana na ugaidi!!?

Kauli nzito sana itasababisha kizaa zaa!!

Mungu ibariki Tanzania!!
Si nzito na haiwezi kusababisha kizaa zaa, hakuna mahali serikali imeshindwa it just ime ainisha kuna national security threat kutoka kwenye nyumba za ibada. How wata deal nalo thats up to them
 
Viongozi wawe wana pima matokeo ya wanacho kitamka kabla ya kukitamka,hii kauli yake inaweza sababisha akapoteza cheo chake.
Kama Tanzania tayari imekuwa blacklisted na UN kwa kuwa na viashiria hatari vya ugaidi, matamko ya viongozi yapimwe vipi tena?!!
 
Angeonekana yuko siliasi na masilahi ya nchi iwapo angedhibiti kwanza ng`o zinazo fadhili ushoga na utoaji mimba zilizo jaa hapa nchini.
Hizo ngo's zinaathiri vipi uchumi wa nchi na maslahi ya mwanachi moja kwa moja.

Watu mnachizika na ushoga usiowaathiri chochote mnaacha rasilimali zenu na vitukuu vyenu kutumika hovyo.

Wewe shoga anakuathiri nini?? Haya Juma Lokole ni shoga wewe hapo umeathirika vipi? Nchi imeathirika vipi kwa Juma Lokole kua shoga??
 
Waziri
1. Ujenzi huzingatia kanuni za mipango miji. Inakuwaje Wizara husika inatoa kibali cha ujenzi wa nyumba za Ibada kinyume na taratibu? Wenye numba za ibada hawana tatizo, waliotoa vibali wana tatizo.
Kubadilisha matumizi ya ardhi ni kosa, waliofanya hivyo wamechukuliwa hatua gani!

2. Hakuna Taasisi za jamii, kuna Chama cha Siasa CCM kinasafirisha wahamiaji haramu. Ushahidi upo
Ingalikuwa gari ina alama za Chadema, ungemsikia '' Jaji '' akiandika barua Chama kijieleze

3. Utakatishaji pesa ni suala la Polisi na Takukuru, Mh huoni unatueleza ulivyoshindwa kazi? sisi tufanye sasa !

JokaKuu Pascal Mayalla
 
Yaani ningewaona wajanja Kama wangejikita katika noise pollution. Kuna hili la ma bar kutopiga miziki kwa sauti za juu mwanza walipiga beat Naona wale jamaa walijiunga baadaye Naona wanaendelea kupiga makelele.
Lindeni mental, physical and spiritual za watu.
Na hapa wangekusanya faini nyingi sana kupitia huu uchafuzi wa kelele
 
Arusha Misikiti imejazana sana Yani ukiwa na 8x8 kiwanja waarabu wanakujengea msikiti.. Yani Kila Kona Kwenye makazi ni msikiti..
Kuna hawa wananunua kakiwanja Katikati ya makazi wanajifanya kujenga madrasa mara ghafla ni msikiti.. Kila sentensi utasikia Kafirun ... Kafirun...
 
Back
Top Bottom